soma hizi sheria

SI unit

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
1,953
Reaction score
767
ZIFUATAZO NI ADHABU ZITOLEWAZO KWA UVUNJAJI WA SHERIA ZA CHAMA CHA WANYWAJI POMBE:

  1. Kosa la kumtoroka mlevi mwenzako kwenye Bar – Jela miezi tisa.
  2. Kuacha kunywa pombe na fedha unazo – Kifungo cha maisha.
  3. Kuvunja chupa ya beer – Jela miaka miwili.
  4. Kumkaribisha mume au mke wa rafiki yako bila idhini yake – Viboko ishirini vya makalio na kufungiwa kunywa nusu siku.
  5. Kumchukulia dhamana mtu asiyepiga gambe/mma (pombe) – Adhabu yake ni kutolewa chamani.
  6. Kumwibia pombe mlevi mwenzako ni kosa kubwa – Jela mwaka mmoja.
  7. Kukataa kunywa wakati umekaribishwa – Jela miaka mitano.
  8. Kukwepa ulevi wa aina yoyote adhabu ni – Kunyang’anywa mume au mke, kama huna utaozwa mume au mke kwa nguvu.
  9. Kupita Bar au Grocery na kujifanya huoni hilo ni kosa kubwa faini yake ni – Kuwanunulia wanywaji wote waliokuwa kwenye Grocery au Bar kila mtu kinywaji anachokunywa na kukaa ukiwaangalia mpaka wamalize.
  10. Kumcheka mnywaji mwenzako akiwa amelewa ni kosa la jinai, unachotakiwa kufanya ni kumpongeza kwa kazi nzito aliyoifanya adhabu yake ni – Kutolewa kwenye Bar muda wa dakika moja.
 
Kujipimia mwenyewe bila izini ya mama muuza,
KUNYONGWA.
 
Kunywa pombe mpaka ukazimia -unazuiliwa kunywa miaka 8 na utatakiwa kuhudhuria baa kuhudumia alevi wenzako tu
 
Vipi kuhusu wa2 wanaolewa viloba ambao hawakai baa, m2 ananunua anakunywa huku anatembea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…