Soma Hii Mpaka Mwisho Kama Unataka Kupata Hili SOMO Kutoka kwa Huyu Professa!..

Seif Mselem

JF-Expert Member
Oct 16, 2023
257
441
Mwaka 1960s Professa “Jerry Uelsmann” alienda kufundisha Chuo Kikuu cha Florida huko Marekani.

Siku ya kwanza Akiwa Darasani aliwa Gawanisha Wanafunzi wake wa...

"Film Photography"

Kwenye Makundi Mawili...Na lengo ilikuwa ni kwa ajili ya Majaribio (Experiment) kipindi Semista Inaendelea.

Na mgawanyo Ulikuwa Kama Hivi...

Wanafunzi waliyopo upande wa kushoto mwa darasa watafanya Jaribio kulingana na WINGI wa Picha

Afu siku ya mwisho MAKSI zita Gawanyishwa kama ifuatavyo...

Picha

100...A

90...B

80...C

70...D

N.k...

Kwahiyo hapo ili upate Banda (A) lako Wewe kazi yako ni Kupiga Picha nyingi tu

Umeona Jinsi Ilivyo Rahisi?..

Yeah!

Wakati huo huo...

Wanafunzi wa Upande wa kulia mwa Darasa watafanya Jaribio kulingana na UBORA wa Picha

Inamaanisha ili upate A Yako kali basi Lazima uwe na Picha kali Moja (Nzuri)

Kama kawaida yetu wanafunzi na wale ikawa vile vile

Kuna walioko Serious na kazi wakapiga Picha zao za kutosha ili kupata Matoke mzuri...

Na kuna wale kama Mimi na Wewe Si Unajua... Hahaaa (Am Just Kidding)!

Kiufupi malengo yalifanikiwa na ikawa kama hivi...

Mwisho wa Semista Professa alishangazwa na Matokeo aliyoyapata kutoka kwa Wanafunzi

Kabla sijaendelea Labda nikuukize Swali...

"Unadhani ni kikundi gani kilitoa picha BORA Zaidi?"

Yeah uko Sahihi...

Picha zote Bora zilitokea kikundi cha watu wa WINGI/IDADI (Quantity)!

Unadhani ni Kwanini?..

Kwasababu kikundi cha watu wa IDADI wakati wa Semista ikiendelea

Walikuwa busy kupiga Picha kutafuta Position Nzuri ya Mwanga

Kujaribu Mbinu mbali mbali kama kupiga ndani na nje ya Vyumba

(Indoor & Outdoor Pictures)

Vile Vile...

Walipata Muda wa kujifunza kutokana na Makosa waliokuwa wanafanya Katika...

Mchakato wa kuitafuta “A” Walijikuta wame Boresha UJUZI wao wa upigaji Picha

Wakati huo huo kikundi cha watu wa UBORA (Quality) wao walikuwa...

Wakibahatisha picha moja moja kwa Lengo la kutafuta Perfection (Ukamilifu)!

Mwisho wa Siku hawakuwa na Chochote kizuri cha kuonesha zaidi ya Picha Moja ya... Kawaida!

Labda Nikuulize Swali...

"Umejifunza nini Kutoka kwenye hili Jaribio?"

Kama ulikuwa na mimi toka Mwanzo mpaka sasa Basi kuna kitu utakuwa Umekigundua...

Ngoja Tukione hapa Chini

Watu wengi Wamekuwa wakijaribu kutafuta Njia Bora katika Maisha yao

Mfano...

Njia ya Haraka zaidi ya Kupunguza Uzito...

Njia Bora na Rahisi ya Kujenga Misuli na kuwa na Six Packs...

Wazo la uhakika la kufanya Biashara ya Nguo...

Umejikita sana kwenye kutafuta Njia BORA za kukupa matokeo badala ya Kuchukua Hatua (Taking Action)!

Kuna Usemi Unasema—"The Best is the Enemy of the Good"

Na hapa ndipo unapokuja utofauti kati ya kuwa kwenye "Motion" na kuchukua "Action"

Haya maneno kwa haraka haraka utadhani ni sawa ila SIO!

Nitakwambia hapa...

Being on "Motion"—Ina maanisha unapangilia na kupangilia mikakati wakati huo huo unajifunza

Hayo yote ni mambo mazuri kufanya LAKINI hayakupi Matokeo

Na ndio maana haijalishi unaenda mara ngapi kwa mwalimu wako wa Gym kama hutofanya unachosema huwezi kupata Shape unayoitaka

Ndo maana huwa Nasema...

"If Preparation Becomes a form of Procastination, You need to change Something"

Kwasababu kujianda kujianda Bila kuchukua hatua ni sawa na...

Kupata ushauri wa Daktari afu usiufanyie kazi (Hiyo ndio Maana ya kuwa in Motion)

Motion unakufanya uhisi kama Unafanya mambo kumbe hamna kitu Unafanya

ILA...

Being In Action...Ni kufanya vitu ambavyo vinakuletea Matokeo

Mfano...

Ukianza kuanda nguo, sabuni na beseni lako ili Ufue hiyo ni—"Motion"

Ila ukikaa chini ya kivuli ukaanza kufua na kuanika hiyo ni—"Action"

Huhitaji kupangilia (Mipango) vitu tena Unahitaji Kuanza kuvitekeleza

Ukitaka kufanyikiwa Usianze na kutaka kuwa Mkamilifu ANZA Na Kufanya na Kurudia rudia Mpaka utakuwa KAMILI!

Na hilo Ndilo SOMO la Professa kwenye hayo Majaribio yake mawili...

Uwe na Siku Njema!

Gracias

Seif Mselem
 
Back
Top Bottom