( Soma hapa tafadhari )

( Soma hapa tafadhari )

kibataz

New Member
Joined
Aug 5, 2013
Posts
2
Reaction score
1
Shukrani kwako uliyekubali kuingia ili usome ninachotaka ukisome. Tafadhali soma hadi mwisho.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23. Nimemaliza kidato cha nne mwaka 2010. Nilijitahidi sana kusoma. Darasani tangu nikiwa kidato cha kwanza hadi cha nne sikuwahi kutoka nje ya kumi bora. Nikaamini kwa bidii yangu nitafauru kwenda A level.
Lakini mambo hayakuwa hivyo. Kwenye kile kimbunga cha kufeli kilichotokea mwaka 2010 na mimi kilinikumba. Hata sikujua kwanini nilifeli namna ile. Nilipata division 0 ( zero ). Nilisikia tu eti imeundwa tume kuchunguza kilichotokea ila sikujua mwisho ilikuwaje. Nikawaza sana lakini mwisho nikajipa moyo kwani niliona kufeli siyo mwisho wa maisha.
Kwakuwa nilikuwa nina kipaji cha uchoraji nikaamua kuanza kuchora katuni ( VIBONZO ) ili niwe napeleka kwenye magazeti ili japo nipate fedha ya kuendeshea maisha kwani nyumbani hali ilikuwa ngumu mno. Mzee hakuwa amejenga, tulikuwa tumepanga kachumba kamoja tu. Na kwa kusema ukweli mimi hadi nafika kidato cha tatu nilikuwa bado nalala chumba kimoja na mama na baba pamoja na dada. Vitanda vilikuwa viwili. Hivyo mimi nililala na baba arafu dada akalala na mama. Mtaani mimi na dada yangu tulichekwa lakini sasa tungefanyaje wakati hakujenga?.
Nakumbuka pale NEW HABARI ( sinza ) nilisha kwenda kila mara kupeleka katuni lakini nilikataliwa kwani niliishia tu pale nje ambapo secretary aliniambia kuwa magazeti ya pale yote yana watu wao maalum wanaowachorea katuni, hivyo mimi sihitajiki. Nikaanza kutunga story nikaenda tena pia nikaishia pale pale kwa secretary akaniambia kuwa mtu anayehusika na hadithi yupo safari. Nikaamua kuondoka na wiki iliyofuata nikaenda tena akanimbia kuwa bado hajarudi.
Nikapiga mahesabu nikaamua nipeleke hadithi yangu kwenye gazeti la SANI. Huko nashukuru ilipokelewa nikaambiwa watanijulisha kwa simu. Lakini hata hivyo haikuwa hivyo.
Mwaka 2011 kwa bahati nikapata magazeti mawili ya dini. Nikawa nachora VIBONZO arafu nawapelekea. Gazeti moja walinipa elfu nane kwa kibonzo kimoja na lingine walinipa elfu tatu. Kwa wiki yalitoka mala moja hivyo kwa wiki nilikuwa naingiza elfu kumi na moja. ( Hapo toa nauli ( kutoka Kimara Bonyokwa hadi kimara mwisho nilikuwa natembea kwa miguu, arafu kutoka kimara mwisho hadi kuyafuata hayo magazeti ni magari mawili. Hivyo kwenda na kurudi ni magari manne. kula nilikuwa sili. Nilikuwa naondoka nyumba na nauli ).

Japo malipo yalikuwa madogo lakini angalau kidogo niliona yananisaidia kwa kiasi fulani. Hata hivyo gazeti moja kati ya hayo mawili walikuwa wakinilipa kwa shida sana. Yani ilikuwa hadi nifuatirie sana ndo nilipwe. Nikavumilia tu.

Mama yangu alikuwa akisumbuliwa na presha kwa muda mrefu sana. Ni hivi mwezi wa sita tu presha ikamsababishia apalalaizi. Sasa dada nayeye ikabidi asiende kibaruani ili akae na mama. Wakati huo Mzee naye kazi yake yenyewe ni ya kubangaiza kariakoo. Maisha yakazidi kuwa magumu.
Nikafuatriria malipo yangu kama kawaida nikawa nazungushwa tu. Mara jumatano, mara ijumaa, wiki ijayo, ooh mara kesho.

Nakumbuka siku hiyo usiku wa saa kumi mama alizidiwa. Tukampeleka hospitali palestina ( SINZA ). Mzee alikuwa ameshaenda kwenye mihangaiko yake. Hivyo ni mimi na dada yangu tu ndiyo tuliyokuwa tukihangaika na mama yetu usiku huo. Nikampigia simu Muhariri mkuu wa gazeti ili angalau anitumie malipo yangu akasema atanitumia lakini niliamini asingetuma kwani nilishamzoea. Hivyo ikanibidi nimueleze hali hali halisi kuwa nipo hospitali mama yangu ndipo akanitumia elfu kumi na moja kwenye simu.

Yani manesi walikuwa wakituangalia tu kama vile hawatuoni wakati wanatuona kabisa kuwa tupo na mgonjwa. Siku hiyo ndo niliamini kuwa Masikini huwa wanapata shida sana kwenye mahospitali. ( Hatuthaminiki kwa kuwa hatuna kitu ). Kila nesi tuliye mgusa alituangalia tu arafu alisema " mwambieni nesi fulani. Mi nina kazi ". Nakumbuka mama alituangalia tulivyokuwa tunalalamika kisha alisema kwa sauti ya chini kabisa ya maumivu " Wanangu, ndiyo mambo ya hospitali hayo "

Saa tatu ndo mama akapewa kitanda na saa nne ndipo huduma ya matibabu ikaanza. ( Nashukuru alihudumiwa )

Nikapiga mahesabu nikaamua niache kuchora VIBONZO nitafute kibarua sehemu nyingine. Nikapata kibarua kwenye kiwanda cha soda ( kipo mwenge ). Wastani wa kipato kwa siku ni 4500. Tunalipwa kwa wiki. Sasa hivi naishi KIVULE ( Gongo la mboto ). Nauli kwa siku ni 2200. Mimi ni kibarua tu, hivyo sitakiwi kupanda STAFF BUSS. Hapo bado sijala kitu. Humu kiwandani kwenye kitengo ambacho mimi nipo huwa hatupewi chakula ( ila wapo ambao wanapewa coupon za kulia chakula ). Ukitaka kula inabidi umpate mtu akuuzie coupon yake ili ukale wewe badala yake. Ila kwa mimi huwa nashindia maji tu. Ule muda wa kula huwa nakunywaga soda tu basi imetoka.

Sasa hivi hii ni wiki ya tatu nipo nyumbani. Kiwandani kazi hakuna hadi tutakapo taarifiwa ndipo twende. Nimekwama sana jamani na ukizingatia mama yu mgonjwa amepalalaizi. Mwenye kuweza kunisaidia kazi nitamshukuru sana. Hata kama siyo kazi ila hata angalau ukinielekeza tu ninapoweza kupata Kibarua nitakushukuru.

Nisaidieni jamani 0715553166
 
Pole, jipe moyo Mwenyezi Mungu ni muweza wa vyote Inshallah utafanikiwa, usikate tamaa coz despair is a moral suicide
 
pole sana kwa kweli kazi kupatikana kwa siku hizi ni ngumu sana nakushauri anzisha hata kibiashara kidogo cha kukuingizia uku ukiendelea kutafuta kazi usikaa ivi ivi hata kigenge kidogo weka barazani kwenu,
 
Pole sana,kuwa mvumilivu wewe unakipaji cha kuchora tatizo kwenye vyombo vya habari vingi hapa bongo vimetawariwa na rushwa ya ngono ila nakushauri jaribu kuwa unachora picha nyingi kwa ubunifu zaidi halafu nenda IPP MEDIA kwani pale kuna magazeti mengi natumaini utaziuza kama fleerance cartunist utatoka siku mmoja
 
unajua tatizo letu watanzania tunatumia watatizo ya familia zetu kama added advantage, hapa mie naona ulitakiwa kusema kipaji chako na uzoefu ulionao kwenye fani gani, kuna watu wakiongea matatizo yao unaweza ukakimbia.... inawezekana ungesema naomba kazi yeyote mtu akakupa, ila akiskia matatizo uliyonayo anajua akikupa nafasi utakua kabeba matatizo ya familia nzima, Baba, mama na Dada ..... au ukipata mafanikio ndani ya mwaka anajua umeiba coz anajua background yako yote......

Just thinking ....
 
unajua tatizo letu watanzania tunatumia watatizo ya familia zetu kama added advantage, hapa mie naona ulitakiwa kusema kipaji chako na uzoefu ulionao kwenye fani gani, kuna watu wakiongea matatizo yao unaweza ukakimbia.... inawezekana ungesema naomba kazi yeyote mtu akakupa, ila akiskia matatizo uliyonayo anajua akikupa nafasi utakua kabeba matatizo ya familia nzima, Baba, mama na Dada ..... au ukipata mafanikio ndani ya mwaka anajua umeiba coz anajua background yako yote......

Just thinking ....

mkuu, kumsaidia mtu ni moyo . Msaidie tu huyu dogo kama unakaopotunity kokote.
 
Nimesikitishwa sana na kisa chako. Kubaliana na hali uliyonayo, mwombe Mungu kila wakati, nyakati na nusu wakati. Amini tu kwamba ipo siku utatoka. Mi naelewa kwamba unapitia kipindi cha mpito naam kitambo kidogo kijacho Mungu atakufungulia njia mpaka ushangae.
JIPE MOYO KIJANA-there is ADAY for you!
 
pole sana,hzo nı changamoto za maısha,naamın Mungu anakusud na maısha yako,pıa elewa kıla jarbu lına mlango wa kutokea.Mkabıdh Yesu maısha yako ksha kla tatzo mpe yeye hakıka atakupa mlango wa kutokea na ww utashangaa.maomb ndıo njıa pekee ya jarbu lako.ubarıkıwe
 
Back
Top Bottom