Huwezi kuwa ughaibuni halafu unarudi na sh. laki tatu ambayo ndiyo unayoitegemea kuanzisha biashara. Hauko serious. Hili jukwaa siyo la fictional stories. Watu kama nyie mtasababisha jukwaa hili lipoteze maana yake. Habari kama hizi peleka kwenye hoja mchanganyiko au jokes, sio hapa.
Duh sijawahi ona mtu mwenye roho kama ya kwako...Wewe una maisha gani haswa yanayokufanya udharau wengine wenye kidogo?Kama hauwezi msaidia ndugu yetu kuwa na busara kidogo.. Kwenye jamii watu kama wewe ni kikwazo sana
pole sana mkuu, ukifika nyumbani hebu ni-PM tuongeze huo mtaji tuungane tufanye biashara.
nimeona mtu kama wewe UNAEJIAMINI sio bure, kuna kitu cha zaidi ndani yako, ni zaidi ya binadamu wa kawaida!.
labda mleta mada hajaeleweka laki tatu hela za kitanzania au usd? hakika sikufikirii vibaya ila mkuu hicho ni kiasi kidogo sana cha kuanzia biashara kama umeshakuwa mtu mzima na unafamilia labda kama bado inachemka unaweza kuuza hata maji, sigara au kibanda cha kiti moto(inategemea na imani yako) au hata duka la taka taka linalipa kwa hiyo biashara ila kma age imeenda kidogo please usirudi, halafu una nauli ya kurudi, una uhakika wa kufikia?? je uko peke yako huna mtegemezi?? una hela ya kujikimu tofauti na hiyo laki tatu?? think twice mkuu before hujamwaga manyanga.
Duh sijawahi ona mtu mwenye roho kama ya kwako...Wewe una maisha gani haswa yanayokufanya udharau wengine wenye kidogo?Kama hauwezi msaidia ndugu yetu kuwa na busara kidogo.. Kwenye jamii watu kama wewe ni kikwazo sana
ndio...Na Ndizo Hizo Nilizozichanga Toka Mwaka Jana!
Hiyo pesa ni mtaji mkubwa sana kakangu kama upo tayari kufanya kazi yoyote.kwa huo mtaji nakushauri kitakacholipa haraka ni biashara ya chakula achana na habari ya mazao ulime upande na upalilie kwa sh ngapi?ni mabadiliko y hali ya hewa,Sasa ingekuwa mimi wewe hiyo pesa ningenunua nusu gunia la viazi vya chips ambalo najua mbeya halizi 50 elfu,mafuta ndoo moja haizidi 30 elfu japo sina hakika,jiko refu la mkaa lenye plate tatu na moja ndogo.na hapo biashara ingeanza.tena huitaji longolongo mtu mja tu unaanza nae kama kuna chuo fanya karibu na chuo usiku na mchana wiki tu utaniambia.All the best