Siku tatu nyuma JF walitoa update ya app yao. Ilikua imeboreshwa mno, yaani robo ya faida ya kuingilia JF kupitia web ilikua kwenye hii update.
Mfano ile kuona sticky contents, nilivutiwa sana na hii kitu.
Pia wakahama rangi, kutoka ile dark blue mpaka light blue.
Lakini baada ya kuupdate nikagundua notifications haziingii. Mbaya zaidi imekariri notifications za nyuma ila inaniambia ni za siku mbili nyuma..
Nikauniinstall na kuinstall upya.
Bado ikawa haileti notifications.
Nikaclear data, nikalog out na kulog in tena.
Bado notifications haziji.
Kisha jana siku nzima ikawa inanidai password kila muda. Kufikia hapo nikaona hii update ina vitu vya kufix.
Bahati nzuri, hua naback up apps zangu mara nyingi na last time niliupdate hadi app ya JF hivyo nimeitoa hii mpya na kurudisha ya zamani.
Narudisha tu ya zamani na notification inaingia.
JamiiForums mna kazi ya kuiweka sawa hii update.