Solar Technician available

Solar Technician available

Kontelo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
571
Reaction score
161
Habari zenu wanajamvi,

Mimi ni fundi mwenye ujuzi wa umeme wa mionzi ya jua(Solar Power) kwa zaidi ya miaka 8 sasa. Nina elimu ya ufundi wa umeme wa majumbani ngazi ya cheti niliyoipata VETA Dar es salaam, na baada ya hapo nikapata mafunzo ya umeme wa nishati jadidifu(Renewable Energy) kupitia kozi mbalimbali nilizopitia km Sida-Mem 2008 na ya DIT(Dar es salaam Institute of Technology) mwaka 2009.
Nimefanya kazi kupitia makampuni kadhaa hapa Dar es Salaam na pia nimeshiriki project kubwa kubwa kadhaa ikiwemo ya USAID kupitia mradi wa TUNAJALI wa kuhudumia wagonjwa wa Ukimwi kwa mikoa ya Dodoma, Iringa na Morogoro mwaka 2011, na mradi wa kusaidia Elimu Tanzania ujulikanao km Tz21 chini ya USAID kwa shule 900 za Mtwara na Zanzibar kuanzia mwaka 2012, pia nimeshiriki ktk mradi wa kuzalisha umeme wa Solar kwa Mwiba Safari Tour Camp ya 40kw na tumeongezea 10kw na kufanya jumla ya 50kw kwa sasa kwa matumizi ya camp yote kwa kampuni ya TGT(Tanzania Game Trucker) mwaka 2012.

Pia nafunga umeme wa Solar kwa mtu binafsi kwa gharama nafuu kabisa.

Km kuna kampuni au mtu binafsi aliye tayari kufanya kazi na mimi tunaweza kuwasiliana kupitia address hapo chini.

+255 684 908 097
+255 766 249 797
hamadi360@gmail.com.
Dar es Salaam.

Nawasilisha.
 

Attachments

  • 1408869148446.jpg
    1408869148446.jpg
    79.5 KB · Views: 343
Pia nafanya system designing na cost estimation kulingana na bajeti yako. La kuzingatia kabla ya kufanya designing ni kujua utahitaji kutumia nini kwa umeme wa solar? Ukishajua hilo hakikisha unajitahidi kuwa na data ya kila kifaa kinachotakiwa kuunganishwa na huo umeme. Kila kifaa kinachotumia umeme kina rate interms of power(P), voltage(V) na current(A) hii haijalishi ni umeme wa solar au Tanesco. Hakikisha unasoma vizuri kifaa chako kisha uelezee. Unapokosea kutaja power ya kifaa/vifaa vyako cost estimation huwa kubwa au ndogo. Na hili huweza kusababisha system kufanya vizuri au kuwa under performance. Km hutoweza kujua au kusoma izo rated power niite nitakusaidia.
 
Watu wengi wanapenda rough cost( bei za makisio), hii ni nzuri lkn pia ni mbaya. Kwasabab designer wa mfumo wako wa solar anaweza kupatia au kukosea kwasabab ametoa jibu la kubahatisha bila kujua ukubwa na matumizi ya vifaa vyako. Ht ukienda Tanesco unapoomba kufungiwa mita ni lazima ifanyike hesabu kwa maana designing na mchoro unaoonyesha jinsi vifaa vitavyokuwa kuwa na kufanya kazi. Kupitia designing na mchoro wako ndipo Tanesco huamua ni tariff gani inakufaa. Hakuna kupiga simu kusema ntahitaji kutumia friji na taa tu. Lazima uonyeshe kwa mchoro. Hivyo hivyo kwenye solar lazima designing kwanza ifanyike ndio itoe jibu muafaka. Watu wengi huogopa kufunga systems za solar kwasabab ya cost estimation za kwenye simu.
Tujitahidi ktk hili ili tuweze kuifahidi nishati hii vizuri.
 
Battery za BAE za volt 2 zilizoungwa mfumo wa volt 24.
 

Attachments

  • 1409040766110.jpg
    1409040766110.jpg
    63.7 KB · Views: 136
unaposema utafunga umeme wa solar kwa bei nafuu sana unamaanisha gharama zako za ufundi au unauza vifaa???
 
unaposema utafunga umeme wa solar kwa bei nafuu sana unamaanisha gharama zako za ufundi au unauza vifaa???

Mkuu gharama nafuu ni za ufundi. Mimi sina kampuni ya kuuza vifaa vya solar ila najua vifaa bora na vyenye gharama nafuu kwa mteja km nilivyotangulia kueleza kwenye uzi hapo juu.
 
Solar kwa ajili matumizi ya TV, jiko, redio, jokovu pamoja na taa. Kwa makadirio, gharama yake itakuwa kiasi gani?
 
Battery za BAE za volt 2 zilizoungwa mfumo wa volt 24.

Watu wachache wasio na elimu kuhusu battery na cell watashangaa ukubwa wa izo battery km zilivyozoeleka. Ila kitaalam zinaitwa cell km cell za radio ambazo watu wachache wanaziita battery. Battery kwa ufafanuzi ni mjumuiko(connection) ya cell zaidi ya moja zilizoungwa parallel au series. Ila kwa bank ya hapo kwenye picha tunaita ni battery kwasabab zimeungwa pamoja kwa mfumo wa series.

BAE cell au battery ni brandy ya Germany na ni well known kwenye matumizi ya mifumo ya Renewable Energy duniani kote. Product zao zinaanzia za Volt 2, Volt 6 na 12.
 
Solar kwa ajili matumizi ya TV, jiko, redio, jokovu pamoja na taa. Kwa makadirio, gharama yake itakuwa kiasi gani?

ni ngumu kujua gharama mpaka useme ivyo vifaa vinatumia nguvu kiasi gani
mfano TV ya chogo au flat?
taa watt ngapi?
radio volt ngapi?
 
ni ngumu kujua gharama mpaka useme ivyo vifaa vinatumia nguvu kiasi gani
mfano TV ya chogo au flat?
taa watt ngapi?
radio volt ngapi?

Hapo umemjibu vizuri. Na ni kati ya vitu nilivyoanza kuvieleza kwenye uzi hapo juu. Muuliza swali km angesoma vizuri thread angeweka vizuri swali lake.
 
Mkuu maelezo hayajanitosheleza kukuelewa unataka kumaanisha nn? Unaweza kufafanua unachomaanisha. Nipo tayari kukujibu

Kuna mdau apo juu alitaka kujua roughly, gharama za kufunga hiyo solar kama ulivoelezea, lakini mkambana na maswai mengi yanayohitajika ili kumpigia gharama-maswali ambayo kama wewe sio mtaalam/mzoefu wa mambo hayo huwezi kujibu. mfano wa swali aliloulizwa ni unataka taa za kiwango gani sijui aina gani (kwamba zipo taa za aina nyingi na zinatofautiana bei)
Sasa kwakua na mimi nataka kujua na hayo maswali ya kiufundi madogo madogo siyajui. Ndiyo nikaomba utoe mfano wewe mwenyewe, say kufunga solar katika nyumba ya vyumba vitano, yenye fridge 2, pasi 1, taa 8...n.k aina ya taa na vitu vingine utaje wewe mwenyewe kwa kua unajua plus gharama ya ufundi kwa aina ya ufungaji utakaoelezea uitaje pia (maana umesema gharama zako ni nafuu).
Lengo la swali langu lilikua hilo nafkiri nimeeleweka
 
Nadhani nimeelezea hapo juu kuwa niliposema gharama nafuu sijahusisha gharama za vifaa vinavyofungwa, mfano solar panel, battery, charger controller, inverter na accessories zingine. Gharama nilizozizungumzia ni za Istallation kuanzia panel mpk battery na mpk vifaa viwe vinafanya kazi/vinawaka. Kwa gharama za makisio hivyo vitu ulivyovitaja ili uweze kupata umeme wa solar wa uhakika ni vema ukaandaa bajeti ya kuanzia 14milioni. Friji zako 2 na pasi ndizo zinazopandisha gharama.
 
Picha zaidi[
 

Attachments

  • 1409908635494.jpg
    1409908635494.jpg
    79 KB · Views: 98
Picha zaidi
 

Attachments

  • 1409908700870.jpg
    1409908700870.jpg
    36.8 KB · Views: 91

Similar Discussions

Back
Top Bottom