Hapana!
Huu ni umeme wa form TWO! Usinambie umeme ni kitu very complicated! Unapokutana na mtu kwenye mtandao mimi huwa naogopa sana kumwambia hicho kitu ni kigumu, kigumu kwako, hujui yeye amesahihisha dissertation ngapi za umeme!
Hebu tuone unatuuzia nini hapa. Umesema kwamba nikitaka naweza kununua bulb za energy saver za watts 12, badala ya 60w. Kwa hiyo chochote nitakachofanya hii mashine itawasha taa ndogo ndogo za watts 12 zisizozidi jumla watts 60, mwisho! I said as much! Nilisema hivyo awali. Na mtu mwenye bulb ya watts 60 kama anazo mbili itabidi azime ya sebuleni akawashe ya jikoni apike akimaliza azime akawashe radio. Na akiwasha taa ya chumbani huku sebuleni wageni kiza! You can't escape that fact, au nieleze nakosea wapi.
In other words siwezi kuthubutu kuwasha jokofu la watts 600!
Siwezi kuwasha hata ka flat panel TV kadogo dogo ka nchi 27 ka watts 130.
Siwezi kuthubutu kuwasha jiko la umeme.
Kwa hiyo hii mashine sana sana ni ya kwenda nayo camp nje ya mji kucharge mashine ya kunyolea ndevu na kisimu kidogo cha Techno.
Huwezi kutengeneza watts ambazo hazipo, simple physics, I mean, there is no physics here at all here. Usinambie umeme ni kitu complicated kana kwamba nachemka halafu siwezi kuelewa unachosema, which is smokescreen anyway. Ndio maana nchi yetu tunalea jamii inayojinyima elimu, hatuna elimu, tunaingizwa mikenge na makampuni ya kufua umeme kwa sababu tunashindwa kudadavua mambo madogo ya megawatt hours ya ma mashine zao hafifu wanazotuletea!