Sokoine, 22/7/1983:’ Chama sharti kiwe ni chombo cha watu cha kujikomboa na kujijengea neema’. CCM kimejijenga katika msingi huo mpaka sasa.

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,601
Edward Sokoine aliyasema maneno hayo kwa nia ya kutuonesha njia tunayopaswa kupita na CCM inavyotakiwa iwe. Nyerere na Sokoine kama viongozi wa juu wa awali ndani ya CCM, walikuwa na nia na kukifanya CCM kuwa chombo cha watu kwa ajili ya kujikomboa na kupata neema.

Mwendelezo wa kujenga CCM katika msingi huu uliachwa na waasisi hao ulikuwa ni kama roho ndani ya CCM, upo na unaendelea kuwepo. Licha ya miaka kupita lakini CCM kuacha kuwa katika msingi huu haiwezekani.

CCM kimekuwa ni dira na maono ya taifa katika kuhakikisha makundi yote ya kijamii na watanzania wote wananufaika na rasilimali zilizopo bila kujali dini, rangi , kabila na chama chake na hii inafanya CCM kuwa chama chenye nia ya kumkomboa na kumnufaisha kila mtanzania

Miaka itapita lakini Imani ya watanzania kwa CCM hasa kwenye mambo yahusiyo maendeleo na kuiona CCM kama chombo pekee chenye nia ya kumkomboa na kumneemesha mtanzania haitopita. Uwepo wa CCM kunafanya watu waneemeke kwa uongozi bora na uzalendo wa kulinda rasimali zetu.

Nina hakika kama Sokoine angepata nafasi ya kuja kuiona walau maramoja CCM yake, angefurahi sana kuona ukombozi wa mtanzania kiuchumi na kisiasa na wananchi wananeemeka sasa chini ya CCM ileile aliyoiacha.

Pumzika kwa Amani, Mzee Edward Sokoine lakini naomba utambue tangu uondoke aliingia Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa, Mzee Kikwete na sasa yupo Mzee Magufuli na wote wamefanyia kazi kauli yako kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.
 
Back
Top Bottom