W
Habari Honda xl ivi kwa mikoa ya kanda ya ziwa tofauti na Kigoma tangawizi haiwezi kukubali?
Wakati mwingine ni vizuri kujaribisha tu, ukipata kwenye udongo tifutifu wenye mfinyanzi kwa mbali au mfinyanzi uliochanganyikana na mchanga unaotunza maji ( simaanishi kutuamisha maji, Bali unaotunza unyevunyevu kwa muda, usiwe ule mkavu, ambao mvua ikikatika tu, likapita jua dakika kadhaa, pashakua jiwe)
Unaweza kujaribu!
Watu walidhani parachichi zinastawi kwenye mvua na baridi kama vile, mbeya, Bukoba, moshi, nk. Baada majaribio ya watu wachache maeneo ya kanda ya ziwa, yamefanya vizuri!
Hivyo Fanya majaribio kwa kutafuta eneo kama hilo, ila kwa kuwa tangawizi pia huitaji mvua nyingi kidogo kwa msimu wote wa mvua, maeneo ya sengerema, geita kidogo, ukerewe na wilaya za kagera, panaweza kuwa right choice, otherwise uwe una mwagiria, lakini kwa mvua chache za maeneo mengine ya ukanda huo, haiwezi Fanya vizuri.