Soko zuri la Tangawizi

Kwa mwenye taarifa(za karibuni) kuhusu bei ya zao hili au/na mawasiliano na wanunuzi tafadhali ntashukuru kama atanisaidia.
 
Kwa mwenye taarifa(za karibuni) kuhusu bei ya zao hili au/na mawasiliano na wanunuzi tafadhali ntashukuru kama atanisaidia.
Bei ni kati ya sh 500 na sh 700 kigoma vijijini, Wateja wengi wanapatikana Mwanza,Shinyanga na Tabora, Wateja wakubwa ni Wanyarwanda, Kwa hiyo unaweza kuwauzia hapahapa nchini au ukapeleka kiwandani Rwanda.
 
Ahsante mkuu kwa taarifa,swali moja la ufahamu je bei hiyo ni kwa kilo au kipimo gani!?
 
Gharama hutegemeana na vitu vingi, mfano Ardhi ni ya kwako au umekodi, mbegu umepata kwa gharama gani, usimamizi ni wa kuajiri au ni wewe mwenyewe, unakolima ni karibu na unapoishi au utalazimika kuhamia karibu na je utafikia kwa mwenyeji au utapanga. Kulima na palizi utafanya mwenyewe au utaajiri. Kwa mambo haya, gharama hutofautiana toka MTU mmoja na mwingine na toka eneo moja na jingine.

Ila katika kilimo hiki, gharama kubwa hubebwa na gharama za mbegu pamoja na palizi. Ekari moja hutumia kati ya kilo 600 hadi 800 kama mbegu. Itategemea mbegu umepata kwa bei gani kutegemeana na upatikanaji wa Hiyo mbegu katika eneo ulilopo.

Sio chini ya palizi 3 zinahitajika, palizi la kwanza kabla tangawizi haijaota vizuri, Mara nyingi hufanyika kwa kutumia kijiti na mikono. Kazi hii huitaji hela ya kutosha kutegemeana na upatikanaji wa vibarua na gharama zao kwa eneo ulilopo.
 
Habari wakuu. Hivi eka moja inaweza kutoa mazao wastani wa gunia au kilo ngapi?

Ekari moja ya maandishi inatajwa kutoa kilo 8,000 hadi 10,000. Katika hali halisi, kwa uzoefu wangu, ekari moja hutoa kati ya kilo 4000 hadi 6,000. Kutegemeana na kama umeandaa shamba kwa wakati, umefanya palizi kwa wakati, uwepo wa mvua za kutosha na hali ya rutuba ya shamba lako.
 
Honda XL maelezo mazuri sana kutofautisha maandishi na halisi. Naweza kukupaje kwa ushauri zaidi
 
Kwa mwenye taarifa(za karibuni) kuhusu bei ya zao hili au/na mawasiliano na wanunuzi tafadhali ntashukuru kama atanisaidia.
Wajaribu hawa kiongozi
Taha_Information_System_.jpg
 
  • Thanks
Reactions: 911

Similar Discussions

Back
Top Bottom