Soko Ubungo kuiua Kariakoo

Wakiua viwanda, watu wasio na kazi wataongezeka , na panya road pia.. sasa hapo ndio kimbembe kitaanza, hawa viongozi wa bongo wanawaza matumbo yao na vizazi vyao, hawajui kua kwa kufanya hivyo hawatakua salama. Nchi ngumu sana hii.
Na ndicho kitafanyika

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Mimi sioni shidA Sana kwa sababu watanzania tumelala sana, wakileta viwanda wakituajiri tunawaibia, kutegea, kulalamika n.k nafikiri walete tu wauze kwa jumla bei rahisi wale wanaouza kariakoo waswahili wenzzetu simu ya laki naa nusu anakuuzia laki nne au tano. sisi tulishaambiwa tuhamie burundi
 
Nahisi itakuwa ni one stop centra ya waagizaji wakubwa. Yaani mizigo mikubwa mikubwa lengo likiwa inchi za maziwa makuu na inchi zisizo na bahari. Halitakiwa ku- compete na kkoo.
Hivi unawajua wachina au wawasikia? Watapeleka mizigo KKOO

Kwanini wasingejenga viwanda?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Hawawezi andamana sababu treni haitaweza beba abiria wote

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
🤣 🤣 🤣 🤣 train ya umeme??? kwa umeme upi??? huu huu wa kipara ??? train ya umeme sio ya mchezo mchezo mpaka sasa hivi inajengwa reli lakini mabehewa ya Escape from Sobibor. Nchi ngumu sana hii
 
Hiyo si sawa maana wataua kabisa viwanda vya ndani.

Wao walipaswa waje kujenga viwanda ili wananchi wapate ajira, na sio kuleta ready made items

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Usiseme wapate ajira sema wapate vibarua. Kuna mchina anatoa ajira ya maana hapa Tanzania.

Mtu anafanya kazi tokea saa mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili kwa ujira wa 5000,huu si ni umasikini wa wazi kabisa.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Sio kwamba tutakuwa tumeletewa China Ubungo ili wafanyabiashara wakanunue hapo bidhaa zao kwaajili ya kuuza?
Wachina wanauza jumla na reja reja. Hata uwawekee sheria kali watauza. Na raia hawataona umuhimu wa kwenda kariakoo wakati anapata bidhaa ya 10,000 kariakoo kwa 4 hapo ubungo, wadhani raia wanataka huu upuuzi wa kujaziwa bei.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Sio kwamba tutakuwa tumeletewa China Ubungo ili wafanyabiashara wakanunue hapo bidhaa zao kwaajili ya kuuza?
Wachina hawakutakiwa kupewa nafasi kuja kuuza bidhaa zao hapa nchini. Wabaki kwao watengeneze kisha wafanyabishara wetu ndio waagize ili ile chain wawe na nafasi ya kuongeza mzunguko wa pesa kwetu na kutengeneza ajira. Kitendo cha Wachina kuja maana yake serikali yao inawakopesha mitaji, wananunua kwa quantity kubwa na makampuni yao kule kwao yanawakopesha na kuwasaidia kuliko wageni hatimaye wanaua ushindani wa kibiashara kwetu.

Majirani zetu kina Congo, Rwanda, Zambia na wengine wanaochukua bidhaa kwetu na kuacha angalau fedha za kigeni kwenye transaction watakuwa wanachukua direct kwa Wachina, ambapo thamani iliyoongezeka itaenda China. Miaka ijayo kutokana na wafanyabishara wetu kuondolewa kwenye uagizaji bidhaa tutabaki na Wachina tu na watakuwa huru kuongeza bei za bidhaa.

Marekani na nchi za Ulaya zilipoenda kuwekeza China hazikwenda kuchuuza bidhaa zao bali kufanya uwekezaji kwenye sekta na kujenga viwanda. Wachina wao wanakuja kuuza hata mabeseni na yeboyebo. Sisi tunafanywa uchochoro
 
Rais Samia anapita humu wakae wafikirie hili swala sio zuri kwa usalama wa nchi.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Sasa wewe hutaki vitu vishuke bei? Au unataka vya wakulima tu ndiyo vishuke bei?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…