jamani naomba kuuliza nataka nikasome sheria najua soko lake gumu lakini vitu gani vya ziada ambavyo vinaweza kunisaidia kupata ajira haraka(kufikiriwa pale nitakapoomba kazi),mfano nilisikia watu wanao soma international relations ni vizuri kujua ligha za kigeni kama french,arab.madiodo gani yanahitajika kwenye sheria?
Unaweza kuwa na GPA nzuri lakini je, unajua nini kuhusu kile ulichokisomea hasa linapokuja suala la ajira?
mhhhhhhhhhhhhh! vichwa vya panzi tumetulia tuliiiiiiiiiiiiii tunangoja muanze na kukoti baadhi ya vifungu tubaki tunacheka tu humu.
Fayamario,
asikudanganye mtu hakuna wakati soko la ajira ya wanasheria litapungua! idadi ya wanasheria tulio nao ni ndogo mno! we piga shule uwe wakili. For your information upto August 2011 nchi hii ina mawakili 2300 tu wanaohudumia watu karibu milioni 40. Tatizo lililopo ni kuwa wanasheria wengi wako mjni hasa dar, Mwanza na Arusha. Inategemea ni kwa kiasi gani wanasheria wanabadilika na kuamua kwa makusudi kwenda pale huduma yao inapohitajika zaidi.
Nitakupa mifano:
1. Mkoa wa Mtwara una High Court Zone na majaji wawili lakini wakili ni mmoja tu. Hapa panahitaji mawakili zaidi ya kumi (at least). Demand ipo.
2. Mkoa wa Mara una kesi za mauaji za kutosha na border post ya Sirari. Hapa pana hitaji mawakili zaidi ya 15 lakini yupo mmoja. Migori iliyopo 5 km from Sirari on the Kenyan side wako advocates 15 na hawawezi kuhandle cases.
3. Mkoa wa Tanga una High Court Zone lakini una advocates 5. Mombasa which is only 3 hours from tanga ina advocates 70 na hawatoshi. (Mind you hakuna tofauti san ya cultures kati ya Tanga na Mombasa).
4. Tabora ina High Court Zone inayohudumia mikoa ya Tabora, Kigoma. Kuna kesi za mauaji zaidi ya 3000 hazijaanza kusikilizwa kwa kukosa mawakili. Mawakili wako 5. Wako busy kweli.
5. Lindi, Manyara hazina mawakili,
6. Mikoa ifuatayo ina mawakili (roughly) kama ilivyoainishwa Singida (4), Pwani (2), Dodoma (10), Mbeya (5).
Hapo nimetaja mawakili. Sikuongea suala kwamba wilaya 80 Tanzania Bara hazina mahakimu wakazi hata mmoja (ili uwe RM unahutaji LLB). Normally kila RM's court inatakiwa iwe na at least 3.
Kwa hiyo demand ipo ya kutosha na soko lipo.
what we need to do as lawyers:-
1. Get out of mentality kuwa ili uwe sucessfull lazima uwe katika miji mikubwa
2. Forget the dreams za kutaka kuajiriwa na kuembrace ujasiriamali
3. Seek how you can develope the passion to help poor people and middle income earners who will glady be your clients forever
4. MOST IMPORTANTLY - create the demand for legal services. Charge reasonably. let people know that you are a person they can turn to. I can assure you that many people fear lawyers n they dont come to them for assistance.
Jiulize watanzania wangapi wasomi kabisa wa digrii hapa mjini including lawyers wanasaini mikataba ya upangaji wa nyumba au ya ajira bila kushirikisha wanasheria. Ukipata hiyo idadi utaelewa demand ni kubwa na supply for the next ten years haitatosha.
You've painted a rosy picture but I doubt if it squares with the actual realities on the ground.
And you say people fear lawyers. What's there to fear about them? Are you talking about their affordability or something else?
You've painted a rosy picture but I doubt if it squares with the actual realities on the ground.
And you say people fear lawyers. What's there to fear about them? Are you talking about their affordability or something else?
usiogope mdogo wangu waambie nyumbani wakulipie ada then chakula ntakuwekea bili kwa CHACHA au DADA GIFTI,stationery utaenda pale KYUNGU napo ntwaweka bili,bia utakunywa GREEN au kwa BAUNSA, watto wazuri pale MATOLA na NYERERE hall
hakuna course bora kuliko nyingine..cha msingi utoke na GPA nzuri. Thats it.
Nani aliyekwambia siku hizi tunaajiri GPA ha ha ha ha ha ha!!! Mkuu siku hzi is all about altitude,even if you have GPA of 4,kama uwezi ku-prove altitude yako,your going to hell,imegundulika kuwa GPA za wanafunzi wa vyuo vingi kuwa ni za kuchakachua hasa za wanafunzi wa kike,Nilikuwa naongea na HR Manager wa Tanesco Arusha region,aliniambia watoto wa kike wanajifanya wanaongea slung sana,lakini kwenye kazi ni upupu mtupu...achana na propaganda za 1947 kuhusu GPA...soma huku ukijenga altitude yako lakini pia hakikisha GPA inakuwa nzuri...
ni gharama asilimia kubwa ya watanzania ni maskini na ignorance kwa hiyo tunakosa confidence...ushauri wa kisheria sio chini ya sh 20,000 kwa hapa mjini ambako mawakili wanapatikana kwa wingi je huko rural kwenye scarce ya lawyers
Hii ni kweli kabisa, nimeenda kwa ma lawyers fulani wa land law ofisi kuuubwa Mkapa Towers, shida yangu ndogo tu, wani failie application za Certificate of Ocupancy mimi nina letter of offer na ma risiti yote ya kodi ya kiwanja. Wakadai laki tano. Nusu milioni ku file papers na kugonga mihuri ya notary public na kumpa messenger wao apeleke Ardhi kwa mguu? Nita file mwenyewe, najua wazito kibao Ardhi pale ila huwa napenda kufata mistari na huwa sipendi kuomba omba favor za ndugu na jamaa maofisini. Hawa ma lawyer wananilazimisha nifanye hivyo.4. MOST IMPORTANTLY - create the demand for legal services. Charge reasonably. let people ....
jamani naomba kuuliza nataka nikasome sheria najua soko lake gumu lakini vitu gani vya ziada ambavyo vinaweza kunisaidia kupata ajira haraka(kufikiriwa pale nitakapoomba kazi),mfano nilisikia watu wanao soma international relations ni vizuri kujua ligha za kigeni kama french,arab.madiodo gani yanahitajika kwenye sheria?
Hapo sasa nimekupata mkuu. Ni bora mara mia uwe na LLB halafu uwe paralegal kuliko kuwa nayo halafu usiwe na ajira kabisa.
Marekani nadhani ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na ma lawyer wengi hapa duniani. Yaani huwezi amini idadi yao. Idadi hiyo kubwa ndiyo inayosabisha watu wai despise hii fani kwa sababu soko la ajira limekuwa over saturated kiasi kwamba wengi wao wanaishia kuwa matapeli tapeli.
Kwenye county courthouses kwa mfano, utawakuta wamejazana lundo wakisubiri dei waka. Wanavizia watu wenye kesi zao walioenda kusomewa mashitaka/ mashauri yao. Wakikuona tu uko peke yako bila counsel...hao wanaanza kukuzonga na kukupa vi business cards vyao na kukuomba contact particulars zako. Wanatia aibu kwa kweli.
usiogope mdogo wangu waambie nyumbani wakulipie ada then chakula ntakuwekea bili kwa CHACHA au DADA GIFTI,stationery utaenda pale KYUNGU napo ntwaweka bili,bia utakunywa GREEN au kwa BAUNSA, watto wazuri pale MATOLA na NYERERE hall