Soko la makampuni ya simu limejaa au ukiritimba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Soko la makampuni ya simu limejaa au ukiritimba?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JAYJAY, Mar 30, 2012.

 1. JAYJAY

  JAYJAY JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 2,495
  Likes Received: 824
  Trophy Points: 280
  nauliza swali hili kwa kuwa nimesikia kuna makampuni ya simu ambayo yapo lakini kama yamekufa au huduma zao hazijulikani sana labda kwa sababu ya ushindani au ni vigezo vya mamlaka ya mawasiliano ndivyo vinadumaza sekta yenyewe maana nasikia kuna sheria inayolazimisha makampuni mapya kutumia mitambo (minara) ya makampuni yaliyopo, je hili si litawapa kiburi makampuni yaliyopo kuyanyonya yale mapya kwa kuyatoza gharama kubwa kiasi cha kuyafanya yasihimili ushindani?
   
 2. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Kitalaamu minara ya simu ina mipaka na sheria zake ss inapokuja suala la kujenga minara mpya kwanza iliopo tu wanadai ni hatari kwa afya ya wanadamu hvy serikali imesitisha zoezi la kujenga mingine itatumika iliyopo mpaka hapo mpango wa mkongo utakapo kuwa ok nchi nzima!
   
 3. Primitive

  Primitive JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kinachotetewa ni uchafuzi wa mazingira imagine makampuni kumi Kila moja na minara Yake! Suala la gharama za utumiaji wa minara linasimamiwa na tcra wenyewe na ndio walioamua mfumo huo! Btw hata kampuni zenyewe zikifanya cost benefit analysis zinagundua it is cost efficient kutumia. Minara ambayo tayari ipo!
   
Loading...