esther mashiker
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 616
- 555
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amemtaka mkandarasi anayejenga stendi na soko la kisasa la kimataifa jijini Dodoma, kutekeleza miradi hiyo vizuri kwa kufuata mkataba na kuwa hakutakuwa na muda wa kuongezwa kukamilisha kazi hiyo.
Amesema hayo alipotembelea eneo inakojengwa stendi hiyo Nzuguni, ambalo sasa mkandarasi yuko katika maandalizi ya awali ya kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo, ambayo itachukua miezi 15 ili kukamilisha.
“Hadi hapa nimeridhishwa na namna mnavyoanza maandalizi ya awali, ikiwa ni muda mfupi tangu tutie saini makubaliano, lakini hakutakuwa na nafasi ya kuongeza muda, hivyo jengeni kwa ubora unaotakiwa na ndani ya muda ili Oktoba mwakani Rais aje azindue mradi huu,” amesema Waziri Jafo.
Mhandisi wa Jiji la Dodoma, Emmanuel Manyanga amesema eneo lililotengwa kwa ajili ya kujenga soko hilo lenye ghorofa moja ni ekari 30 wakati stendi ya kisasa imetengewa eneo la ekari 87. Shilingi bilioni 77.8 zimetengwa kwa ujenzi wa stendi ya kisasa, soko na uboreshaji wa miundombinu ya barabara hizo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema jiji limezungumza na kampuni ya Kikorea kuweka taa na kamera za usalama katika barabara kuu za Iringa, Singida, Arusha na Dar es Salaam.
“Umefika wakati sasa askari wa barabarani hawahitaji kuwepo barabarani. Tunatarajia kuweka taa za barabarani na kamera za usalama ambazo Polisi watakuwa wakizifuatilia wakiwa ofisini,” amesema.

Last edited by a moderator: