Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 2,283
- 3,011
Soka la Italy lilitawala sana barani Ulaya, lakini kuanzia kuporomoka kwa timu ya Ac Milan baada ya msimu wa 2007 kutokana na sababu mbali mbali ikiwepo za uchumi, kisiasa na mipango mibovu ya kutowaanda vijana. Ndipo ikawa mwisho wa utawala wa Serie A kwenye michuano ya UEFA.
Kuna wakati wakapoteza hadi nafasi ya kutoa wakilishi wanne kwenye champions league. Timu za Italy zimekuwa na muendelezo wa kuwa viwango vya chini sana kwa sasa, yaani siyo Italy ya kipindi kile. Leo hii Juventus wakufungwa na Maccabi Haifa, Ac Milan imepoteza ubora kabisa, wamekuwa wabovu kupindukia.
Intermilan nayo tia maji tia maji. Msimu huu kidogo Napoli kaonesha ushindani japo haijulikani safari yao itaishia wapi.
Kushuka kwa soka la Italy shida ni nini wadau?