Marcelo Lippi, mtaalamu wa soka aliyeaamini timu ni zaidi ya wachezaji wazuri

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
MARCELO LIPPI , MTAALAMU WA SOKA ALIYEAMINI TIMU NI ZAIDI YA WACHEZAJI WAZURI

Kua na wachezaji wazuri na bora haikufanyi uwe na timu bora ila mifumo na mipango ndio kila kitu, kupitia huo mfumo na mbinu zako kwanza kabisa utafanya mchezaji watumie kila chembe ya uwezo wao kwa ajili ya timu pili utamfanya mchezaji afurahie game na mengine mengi.

Italy haijawahi kuyumba kutuletea vichwa vya mpira tena vinakua World Class. Kina Arigo Sacchi , Fabio Capello, Antonio Conte , Masimilliano Allegri, Carlo Ancelloti, Marcelo Lippi, Sarri na wengine wengi. Marcelo Lippi..

Italy kule ndiko linapatikana soka la kilinzi kama ni kulinda tu kule umefika, kuna stori ilisambaa kwamba Giorgio Chellini na wenzake walihitaji goli moja tu kuitoa Barca, kwamba walikua na uwezo wa kuwazuia MSN kwa mechi mbili bila kuruhusu goli.

Tangu Helenio Herrera awalishe matango poli ya Catenaccio basi imekua kama desturi, alikuja Arigo Sacchi kuuzima huu ujinga lakini ikaishia kwa Ac Milan tu.

Marcelo Lippi kilikua kichwa kingine kutoka Italy na kilikuja na usataratibu wake na kuchukua makombe yake likiwemo la dunia , siku zote utamu wa makocha huja katika mbinu zao na namna ya uongozi wao.

Lippi alitawala kwa mifumo ya kigumu sana alitumia sana 4-4-2 na 4-5-1 ( hii 4-5-1 ina weza kua 4-2-3-1 au 4-2-3-1 au 4-1-4-1 ) na( huu wa 4-4-2 unaweza kuja na 4-4-1-1 ). Marcelo Lippi hakutoka nje ya hapa kabisa , atabadilika kulingana na hali ya mechi na mpinzani wake….

Dunia ilianza kufaidi shoo za huyu mzee baada ya kuipaisha sana na kuipeleka Napoli michuano ya UEFA msimu wa 1993/1994, Juventus wakamtwaa kama unavyojua mwenye kisu kikali ndo hula nyama nyingi kule alikutana na minofu ivo alikula sana makombe Ginaluca Vialli , Roberto Baggio , Alsandro Del Piero , Didier Deschamps , Antonio Conte na wengine wengi.

Aliwakosha watu wa mpira baada ya ujio wa Zinadine Zidane mwaka 1996, ikumbukwe alikua anatumia 4-3-3 lakini akahamia kwenye 4-4-2 hii ilitokea sababu Zidane alikua kiungo mshambuliaji anayetokea katikati ivo ilibidi abadilike tu, jamaa akaja na 4-3-1-2 huyo mmoja hapo ndo alikua Zidane .

Marcelo Lippi hakukariri maisha wala hakukariri mifumo na alibadilika kulingana na mpinzani na aina ya mechi pia aina ya wachezaji alionao, pale Ujerumani katika kombe la dunia 2006 alidunda karibu na mifumo kadhaa kuna watu aliwapiga na 4-5-1 tena wapo waliofia katika 4-4-2 au 4-4-1-1.

Jamaa kama atakumbana na timu zinazoshambulia kwa kasi basi 4-4-2 ilikua kimbilio lake mfano ilikua mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani

Marcelo Lippi atakumbukwa sanaa sio tu kwa uwezo wake wa kufundisha pia uongozi wake ulikua mzuri, ikumbukwe mkononi wamepitia makocha wazuri tu kama Antoine Conte, Zinadine Zidane, Didier Deschamps na wengine wengi.

Italy ni kama kitako cha soka mifumo na mbinu nyingi za utawala zimetumika sanaa kule , inaweza isiwe ligi inayovutia pia haina mashabiki wengi lakini ni moja ya nchi zilizoleta mapinduzi makubwa katika soka. Soka ni kama somo la uchumi huwezi kulifafanua kwa namna moja, ndio maana zimekuja mbinu nyingi sanaa mpaka leo.

Fulltime page
 
Labda utata unakuja katika tafsiri ya mchezaji mzuri, timu lazima iwe na wachezaji wazuri.
Kwenye soka zinaanza mbinu za kocha kisha wachezaji ndio wanachukua nafasi.
Na si kila mchezaji anaweza kuonesha ubora ule ule katika mifumo tofauti tofauti. Ni wachezaji wachache mnoo ambao wanaweza kuonesha ubora wao ule ule katika mifumo tofauti.
 
Hivi ile United ya Sir Alex Ferguson ilikuwa na wachezaji wazuri?? Naomba ufafanuzi kidogo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
United ya ferguson ipi!? Kuna vizazi tofauti, ila nakutajia wachache kwa mjumuiko utachagua united ya fergie ipi.
Cantona, ince, beckham, giggs, schmeichel, rooney, scholes, ferdinand, van der sar, ferdinand, vidic, cole, Mark Hughes, cr7, rud van Nistelrooy, patrive evra nakadharika nakadharika.
 
Cantona, ince, beckham, giggs, schmeichel, rooney, scholes, ferdinand, van der sar, ferdinand, vidic, cole, Mark Hughes nakadharika nakadharika.
Ebu tupe ya rooney mkuu.

Sent using motorola
 
Rooney, cr7, tevez, giggs, ferdinand, vidic, patrice evra, scholes na michael carrick zaidi ya nusu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza ni wachezaji wazuri!
Hapo golini yupo van de sir.
Sahihi mkuu. Ajabu kipindi hiki tunawategemea kina rashford.

Sent using motorola
 
United ya ferguson ipi!? Kuna vizazi tofauti, ila nakutajia wachache kwa mjumuiko utachagua united ya fergie ipi.
Cantona, ince, beckham, giggs, schmeichel, rooney, scholes, ferdinand, van der sar, ferdinand, vidic, cole, Mark Hughes, cr7, rud van Nistelrooy, patrive evra nakadharika nakadharika.
Mbona hwataji akina Fretcher,Park, Brown, O'Shea, Sylvester,Bebe, Obertan, John Evans na Maceda je hao ni wachezaji wazuri mkuu?? Lkn walibeba ndoo,bila kuwasahau Berbatov, Anderson Fortune

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona hwataji akina Fretcher,Park, Brown, O'Shea, Sylvester,Bebe, Obertan, John Evans na Maceda je hao ni wachezaji wazuri mkuu?? Lkn walibeba ndoo,bila kuwasahau Berbatov, Anderson Fortune

Sent using Jamii Forums mobile app

Unataka kuniambia lippi alichukua vikombekwa wachezaji kikosi cha kwanza, wamejazana wachezaji wa kiwango cha kina maceda!
Hapo sana sana berbatov na park! Anderson kwa mbaali na wes brown!

Mie nimekutajia wachezaji wazuri ambao wangeweza kupata namba kwenye vikosi vingi vya timu kubwa! Kauli ya kusema wachezaji wazuri hawana msaada naipinga! Umeniuliza babu fergie alikuwa na wachezaji wazuri nimekuorodheshea, bado unawaleta wachezaji wako, halafu unaniambia mambo ya makombe, kwakuwa maceda alipata kombe ndio umuite mchezaji mzuri, wakati mwingine makombe ni kama kunguru kumnyea binadamu sio kwamba ana shabaha!

Haya ndio unataka kusemaje mzee?
 
Nilitaka kukuamisha kuwa unaweza kuwa na wachezaji wazuri sana lkn ukakosa kikosi bora,kikosi bora kinatengenezwa na mwl na hicho Ferguson alifaulu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda utata unakuja katika tafsiri ya mchezaji mzuri, timu lazima iwe na wachezaji wazuri.
Kwenye soka zinaanza mbinu za kocha kisha wachezaji ndio wanachukua nafasi.
Na si kila mchezaji anaweza kuonesha ubora ule ule katika mifumo tofauti tofauti. Ni wachezaji wachache mnoo ambao wanaweza kuonesha ubora wao ule ule katika mifumo tofauti.
Hivi ile United ya Sir Alex Ferguson ilikuwa na wachezaji wazuri?? Naomba ufafanuzi kidogo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app

Tafauti ya Lippi na makocha wengine ni kua hategemei individual skills za wachezaji kwenye mchezo wake, kila attack inakwenda kwa mujibu wa mfumo wake sio kutegemea mchezaji Fulani apewe mpira maeneo Fulani afanye mambo. Na ndio mana katika mfumo wake anahitaji Zaidi mchezaji hata wakiwango cha chini lakini awe anatii na kufata maelekezo yake vizuri kuliko individual talent ambaye hatii vizuri.kwa lugha nyepesi anaweza hata mueka bench messi mbele ya Muntari kwenye timu yake kwa kua tu muntari anafata vizuri maelekezo yake. kwa sababu anaamini maelekezo yake ndio ushindi wa timu na si kipaji cha mchezaji.
 
Hivi ile United ya Sir Alex Ferguson ilikuwa na wachezaji wazuri?? Naomba ufafanuzi kidogo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
United ya ferguson ipi!? Kuna vizazi tofauti, ila nakutajia wachache kwa mjumuiko utachagua united ya fergie ipi.
Cantona, ince, beckham, giggs, schmeichel, rooney, scholes, ferdinand, van der sar, ferdinand, vidic, cole, Mark Hughes, cr7, rud van Nistelrooy, patrive evra nakadharika nakadharika.

wachezaji wa Man UTD wa miongo yote ya mafanikio ya Ferguson hawakua wachezaji wabaya ila hawakuwa wachezaji wa viwango vikubwa kwa viwango vya ulaya. ila kwa EPL viwango vyao vilijitosheleza
 
Nilitaka kukuamisha kuwa unaweza kuwa na wachezaji wazuri sana lkn ukakosa kikosi bora,kikosi bora kinatengenezwa na mwl na hicho Ferguson alifaulu sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukisoma komenti yangu ya kwanza ndio nilichokisema!
Katika timu kwanza ni mbinu za kocha, kisha wachezaji wazuri nampinga lippi kusema wachezaji wazuri sio muhimu.
Ni kweli mbinu za kocha zinachukua karibia 60%
Kisha wachezaji ndio wanafata.
 
Tafauti ya Lippi na makocha wengine ni kua hategemei individual skills za wachezaji kwenye mchezo wake, kila attack inakwenda kwa mujibu wa mfumo wake sio kutegemea mchezaji Fulani apewe mpira maeneo Fulani afanye mambo. Na ndio mana katika mfumo wake anahitaji Zaidi mchezaji hata wakiwango cha chini lakini awe anatii na kufata maelekezo yake vizuri kuliko individual talent ambaye hatii vizuri.kwa lugha nyepesi anaweza hata mueka bench messi mbele ya Muntari kwenye timu yake kwa kua tu muntari anafata vizuri maelekezo yake. kwa sababu anaamini maelekezo yake ndio ushindi wa timu na si kipaji cha mchezaji.

Sikupingi, unachoongelea mie ndio nisemacho!!

Individual skills ipo pale kwa maana kadhaa, moja ni kutopoteza mpira kizembe, pili kufanya kazi ya kocha kuwa nyepesi, ana simplify shughuli ya kocha! Iwe goalkeeping,kuzuia kuchezesha timu ama kufunga.

Leta kikosi chochote cha lippi tulitizame uzuri wa wachezaji wake kama alikuwa na kiwango cha kina macheda.
 
wachezaji wa Man UTD wa miongo yote ya mafanikio ya Ferguson hawakua wachezaji wabaya ila hawakuwa wachezaji wa viwango vikubwa kwa viwango vya ulaya. ila kwa EPL viwango vyao vilijitosheleza

Sina hakika na ukisemacho inategemea na wewe unavyowachagua wachezaji wa kiwango cha dunia.
Kwangu giggs, schooles, cr7, rud va, van de sar, schmiechel, patrice evra, rooney, cantona, beckham walikuwa ni wachezaji wa viwango vya dunia.
 
Tafauti ya Lippi na makocha wengine ni kua hategemei individual skills za wachezaji kwenye mchezo wake, kila attack inakwenda kwa mujibu wa mfumo wake sio kutegemea mchezaji Fulani apewe mpira maeneo Fulani afanye mambo. Na ndio mana katika mfumo wake anahitaji Zaidi mchezaji hata wakiwango cha chini lakini awe anatii na kufata maelekezo yake vizuri kuliko individual talent ambaye hatii vizuri.kwa lugha nyepesi anaweza hata mueka bench messi mbele ya Muntari kwenye timu yake kwa kua tu muntari anafata vizuri maelekezo yake. kwa sababu anaamini maelekezo yake ndio ushindi wa timu na si kipaji cha mchezaji.
Huyo uliyemzungumzia hapo ni Sir Alex Ferguson maana ndy ilikuwa tabia yake hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom