Weka kando Juventus, Atalanta, Jinamizi liualo kimya kimya Ligi ya Serie A na UEFA

Nabii kibonge

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
277
308
Wiki iliyopita katika hapa na pale ulizuka mjadala katika chombo fulani cha habari za michezo kuhusiana na ubora wa timu hizi kati ya Rasen Ball Leipzig na Atalanta B.C ipi imekuwa na mwenendo mzuri tokaligi zirejeshwe baada ya corona.

Katika mjadala huo ukazuka mjadala mwingine tena baada ya mchambuzi wa soka katika kituo hicho(pia mchezaji na kocha wa zamani ) Thomas Rongen (usijali kama hujamfahamu, tuendelee) aliposema Atalanta wamekuwa wakijitahidi kidogo sana serie A hivyo haifai kufananisha na RB Leipzig

THOMAS RONGEN ALIMAANISHA NINI?
Huyu bwana alimaanisha nini?na hapo ndipo mjadala ulipozuka kwani Atalanta wamecheza michezo 8 na wameshinda 7 na draw 1 (juzi na juventus) na hadi sasa wanashika nafasi ya pili huku RB Leipzig katika michezo yao 9 walishinda michezo 4 tu na draw 4 na Lose 1.Je alipima ubora wa timu hizi kwa lipi? Alimaanisha nini? Maneno ya Thomas Rongen yakaenda mbali na kufikirisha zaidi je ni kipi kipimo cha kocha bora?

Mjadala huu ulinikumbusha baadhi ya matukio,ukanifanya niyarejee,
1.Ubingwa wa Leicester city chini ya kocha Claudio Ranieri
2.Mtazamo wa watu kuhusu ligi ya Italia wakisema ni ligi ya wakulima (Famers league) na kwamba haina timu zenye ushindani

Na hapa ndio nilipogundua watu aina ya Thomas Rongen ni wengi sana na tupo nao, watu ambao wanaongea vitu kwakubwatuka tu wakijifanya kuwa na uzoefu kuhusu mambo fulani, watu ambao hawana ukamili wa data kuhusu jambo fulani lakini watakupa majibu kwa kujiamini kabisa bila wasiwasi.

Ukitazama msimamo wa serie A Atalanta anashika nafasi ya pili huku akiwa amefunga magoli 93 (26 zaidi ya juventus) huku wakiwa na goal difference ya 50.

Atalanta wamecheza mchezo wao wa 15 jana bila kupoteza wakishusha kipigo cha 6-1 kwa klabu ya Brescia, kila mtu anao ukweli kuhusu draw ya 2-2 na Juventus isitoshe ni hao hao waliompiga goli 5 Ac Milan pia wakampiga goli tano AsRoma.

Labda utasema kwa kuwa ligi haina ushindani, Lakini hao hao katika UEFA champions League wamemtandika hovyo huovyo valencia goli 7-3 huku akipoteza michezo yote miwili home and away. Hapo utajiuliza sasa kama huyu Valencia alimkosesha Barcelona copa del rey kachabangwa goli saba je ubora upi unoongelewa???

IPI NI SIRI YA ATALANTA

Ukiifuatilia Atalanta utamfahamu mtu anaitwa Gean Piero Gasperini. Achana na Antonio Conte au Maurizio Sarri watu ambao tuanaamini ni makocha nguli na vinara wa soka la kiitaliano almaarufu kama CATANACIO.

Rejea fainali ya Internazionale Milan na Bayern Munich 2010. Usiku wa machungu kwa the bavarians ulioletwa na muargentina Diego Milito aliyefunga goli zote mbili. Je unamkumbuka Diego Milito??

Diego Milito ambae ni zao la kocha Gasperini alikuwa ametoka klabu ya Genoa, Klabu ambayo Mario Gasperini alipanda nayo daraja na kuifanya ishike nafasi ya tano katika Serie A ille ya kutisha yenye vilabu kama Ac Milan Juventus Napoli Roma Udinese Na Internazionale vyote vikiwa vinatisha wakati huo.

Baada ya hapoMario Gasperini alizunguka klabu mbali mbali kabla ya kuja kuibuka tena na klabu ya Atalanta ambayo ilikuwa inataka kujinasua na kushuka daraja msimu uliopita

Lakini kupitia kocha huyu klabu hiyo haifikirii tena kushuka daraja haifikirii kufedheheshwa kwa kufungwa goli nyingi na Giants wa Ligi hiyo , bali inafkiria kuchukua ubingwa Serie A, inafikiria kufika mbali hata fainali UEFA.

Yote hayo yameletwa na Gasperini ambaye kikosi chake kinaundwa na wachezaji wa kawaida mno kama kina Duvan Zapata, Papu Gomes, Kina Frank Hotebar, Casagne na Mario Pasalic ambao hatukuwahi kuwajua kabla.Pia Atalanta inashika nafasi ya pili katika msimamo huku katika budget ya bills za malipo na gharama za wachezaji inashika nafasi ya 13..Inafikirisha kidogo

Hapa ndipo nilipokumbuka kuhusu ubingwa wa Leicester, chini ya wachezaji kama Mahrez, Vardy, Albrighton, na Kante ambao dunia haikuwafahamu kabla lakini waliwezaje kichukua ubingwa?

Mpira ni game of tactics na katija hili naungana na kauli ya Danny Levy anasema " money cannot buy your silverware" na hilo ndio Gasperini analithibitisha kwa wachambuzi vilaza kama Thomas Rongen.

Katika jambo la msingi kuzingatia katika ubora wa manager lazima tuangalie hata na budget yake kiujumla lazima tuangalie implementation ya tactics zake na lazima tuangalie matokeo yake uwanjani. Nani asiyejua investment ya Red Bull kwenye Club ya Leipzig??? Nani asiyejua leipzig inavochukiwa n wajerumani kutokana na system zake za umiliki nani? Je hiyo investment inafanana na Atalanta. Je investment ya Leipzig inaendana na matokeo yake uwanjani??

Yupi ni kocha bora kati ya Gasperini na Ninglesman??? Rejea mafanikio ya kocha Arrigio Sacchi chini ya kina Baressi na Maldini na Costarcuta Na Vanbasten ambao most of the team walikua ni academy players na wengine waliosajiliwa kwa bei chee. Rejea na hapo utajua kuwa mpira ni Game of tactics

TACTICS ZA ATALANTA CHINI YA GASPERINI

Kama uliwahi kusikia kuhusu tiki taka basi italia kuna kitu kinaitwa Catenacio, hii ni aina ya uchezaji wa mpira inayohusisha timu kudefend effectively na pia kupanda na kushuka kwa pamoja huku ikihusisha mabeki wa kati watatu(centrale) na kiungo wa kati akicheza kama deep holding midfilder ambaye kuna mda anaplay role kama beki wa kati (mediano). Pia kuna nafasi kama destro . Regista, Terquista (nitaelezea siku nyingine)

Gasperini akiwa muumini mkubwa wa catanacio akiwa na formation 3-4-1-2 au 3-4-2-1 huku timu yake ikiundwa na wachezaji wanaojituma ambao wengi umri wao bado ni mdogo (age avarage ya timu ni 24 ) hii yote ni kuwafanya waweze kuhimili kupanda na kushuka mda wa kupandisha mashambulizi na kurudi kudefend kwa haraka.

Uwezo mkubwa wa Gasperini katika mfumo huu na unafikirisha kuhusu ubora kwa kocha huyu kwani Juventus chini ya kocha Maurizio Sarri wametengeneza chance chache za kufunga magoli na wanazidiwa hata na Leicester au Wolves. Rudi kwa Antonio Conte pamoja na usajili mkubwa alioufanya lakini bado timu yake inagombania kushika nafasi ya 3.

Je Gasperini si kocha bora?Perfomance ya Atalanta ni ya Kawaida?
Thomas Rongens Ulimaanisha nini???

Mwisho ni kwamba tutegemee makubwa toka kwa Atalanta msimu huu kwani sitoshangaa Wakifika nusu Fainali ya UEFA na zaidi ya hapo. Muhimu ni muda Tu
 
Atalanta kilichowagharimu ni mwanzo mbaya. Waliuanza msimu vibaya sana kwenye serie A na champions league pia. Laiti kama wangeanza vizuri serie A kwa moto huu basi bila shaka wangekuwa wanaongoza ligi mpaka sasa.

Kingine wamekuwa na best attacking football lakini kwenye upande wa defending wako ovyo sana. Hivyo mpira wako umekuwa funga nikufunge. Wakiimalisha safu yao ya ulinzi watatisha zaidi ya hapa walipofikia
 
Nawafahamu Atalanta vizuri tu...tangu 2017 nikiwatia kwenye mikeka huwa sina hofu yeyote...bt RB in timu inafanya vizuri sana kwa wakati Fulani lakini kunakipindi hupitiwa na mawimbi....kifupi zote ziko njema tu ukitaka kuzichambua sana ili upate ipi in bora kuliko nyingine unaweza kukuta umedanganya tu...all in all Uzi mzuri...thanx
 
Atalanta wamekuja vizuri msimu huu(kongole kwao)....chamsingi ni consistency..je huu ni mwanzo wa wao kuwa miamba barani Ulaya ama ndiyo yaleyale ya ''One season wonder'' ..
Tatizo unakuta hata wachezaji wao na kocha vilevile wana ndoto za kwenda kwenye timu kubwa zaidi...
 
Apo umeongea mkuu ni kweli wanaconcede sana na hio ndio changamoto kubwa katika mbinu za kocha wao
 
Atalanta wamekuja vizuri msimu huu(kongole kwao)....chamsingi ni consistency..je huu ni mwanzo wa wao kuwa miamba barani Ulaya ama ndiyo yaleyale ya ''One season wonder'' ..
Tatizo unakuta hata wachezaji wao na kocha vilevile wana ndoto za kwenda kwenye timu kubwa zaidi...
Ilo ni kweli kuna shida kubwa sana timu ndogo zinazoperfom vizuri sana huwa wanapoteana sana msimu unaofuta pale wachezaji wao wanapoondoka kwenda timu kubwa
 
Nawafahamu Atalanta vizuri tu...tangu 2017 nikiwatia kwenye mikeka huwa sina hofu yeyote...bt RB in timu inafanya vizuri sana kwa wakati Fulani lakini kunakipindi hupitiwa na mawimbi....kifupi zote ziko njema tu ukitaka kuzichambua sana ili upate ipi in bora kuliko nyingine unaweza kukuta umedanganya tu...all in all Uzi mzuri...thanx
Pamoja sana mkuu pia kongole kwa kuifuatilia ligi hii maana watu wengi wanamentality kwamba ligi ni moja tu nayo ni england
 
Ilo ni kweli kuna shida kubwa sana timu ndogo zinazoperfom vizuri sana huwa wanapoteana sana msimu unaofuta pale wachezaji wao wanapoondoka kwenda timu kubwa
ndio matokeo ya uchumi wa kibepari..mfanyakazi(mchezaji) ataona anastahili kufaidika kadri ya alivyozalisha..Kama muajiri atakuwa na uwezo wa kumbakiza ni masuala ya maelewano...
.. mambo ya kuchezea kwa mapenzi yaliishia kwa Totti na Maldini
 
Wiki iliyopita katika hapa na pale ulizuka mjadala katika chombo fulani cha habari za michezo kuhusiana na ubora wa timu hizi kati ya Rasen Ball Leipzig na Atalanta B.C ipi imekuwa na mwenendo mzuri tokaligi zirejeshwe baada ya corona.

Katika mjadala huo ukazuka mjadala mwingine tena baada ya mchambuzi wa soka katika kituo hicho(pia mchezaji na kocha wa zamani ) Thomas Rongen (usijali kama hujamfahamu, tuendelee) aliposema Atalanta wamekuwa wakijitahidi kidogo sana serie A hivyo haifai kufananisha na RB Leipzig

THOMAS RONGEN ALIMAANISHA NINI?
Huyu bwana alimaanisha nini?na hapo ndipo mjadala ulipozuka kwani Atalanta wamecheza michezo 8 na wameshinda 7 na draw 1 (juzi na juventus) na hadi sasa wanashika nafasi ya pili huku RB Leipzig katika michezo yao 9 walishinda michezo 4 tu na draw 4 na Lose 1.Je alipima ubora wa timu hizi kwa lipi? Alimaanisha nini? Maneno ya Thomas Rongen yakaenda mbali na kufikirisha zaidi je ni kipi kipimo cha kocha bora?

Mjadala huu ulinikumbusha baadhi ya matukio,ukanifanya niyarejee,
1.Ubingwa wa Leicester city chini ya kocha Claudio Ranieri
2.Mtazamo wa watu kuhusu ligi ya Italia wakisema ni ligi ya wakulima (Famers league) na kwamba haina timu zenye ushindani

Na hapa ndio nilipogundua watu aina ya Thomas Rongen ni wengi sana na tupo nao, watu ambao wanaongea vitu kwakubwatuka tu wakijifanya kuwa na uzoefu kuhusu mambo fulani, watu ambao hawana ukamili wa data kuhusu jambo fulani lakini watakupa majibu kwa kujiamini kabisa bila wasiwasi.

Ukitazama msimamo wa serie A Atalanta anashika nafasi ya pili huku akiwa amefunga magoli 93 (26 zaidi ya juventus) huku wakiwa na goal difference ya 50.

Atalanta wamecheza mchezo wao wa 15 jana bila kupoteza wakishusha kipigo cha 6-1 kwa klabu ya Brescia, kila mtu anao ukweli kuhusu draw ya 2-2 na Juventus isitoshe ni hao hao waliompiga goli 5 Ac Milan pia wakampiga goli tano AsRoma.

Labda utasema kwa kuwa ligi haina ushindani, Lakini hao hao katika UEFA champions League wamemtandika hovyo huovyo valencia goli 7-3 huku akipoteza michezo yote miwili home and away. Hapo utajiuliza sasa kama huyu Valencia alimkosesha Barcelona copa del rey kachabangwa goli saba je ubora upi unoongelewa???

IPI NI SIRI YA ATALANTA

Ukiifuatilia Atalanta utamfahamu mtu anaitwa Gean Piero Gasperini. Achana na Antonio Conte au Maurizio Sarri watu ambao tuanaamini ni makocha nguli na vinara wa soka la kiitaliano almaarufu kama CATANACIO.

Rejea fainali ya Internazionale Milan na Bayern Munich 2010. Usiku wa machungu kwa the bavarians ulioletwa na muargentina Diego Milito aliyefunga goli zote mbili. Je unamkumbuka Diego Milito??

Diego Milito ambae ni zao la kocha Gasperini alikuwa ametoka klabu ya Genoa, Klabu ambayo Mario Gasperini alipanda nayo daraja na kuifanya ishike nafasi ya tano katika Serie A ille ya kutisha yenye vilabu kama Ac Milan Juventus Napoli Roma Udinese Na Internazionale vyote vikiwa vinatisha wakati huo.

Baada ya hapoMario Gasperini alizunguka klabu mbali mbali kabla ya kuja kuibuka tena na klabu ya Atalanta ambayo ilikuwa inataka kujinasua na kushuka daraja msimu uliopita

Lakini kupitia kocha huyu klabu hiyo haifikirii tena kushuka daraja haifikirii kufedheheshwa kwa kufungwa goli nyingi na Giants wa Ligi hiyo , bali inafkiria kuchukua ubingwa Serie A, inafikiria kufika mbali hata fainali UEFA.

Yote hayo yameletwa na Gasperini ambaye kikosi chake kinaundwa na wachezaji wa kawaida mno kama kina Duvan Zapata, Papu Gomes, Kina Frank Hotebar, Casagne na Mario Pasalic ambao hatukuwahi kuwajua kabla.Pia Atalanta inashika nafasi ya pili katika msimamo huku katika budget ya bills za malipo na gharama za wachezaji inashika nafasi ya 13..Inafikirisha kidogo

Hapa ndipo nilipokumbuka kuhusu ubingwa wa Leicester, chini ya wachezaji kama Mahrez, Vardy, Albrighton, na Kante ambao dunia haikuwafahamu kabla lakini waliwezaje kichukua ubingwa?

Mpira ni game of tactics na katija hili naungana na kauli ya Danny Levy anasema " money cannot buy your silverware" na hilo ndio Gasperini analithibitisha kwa wachambuzi vilaza kama Thomas Rongen.

Katika jambo la msingi kuzingatia katika ubora wa manager lazima tuangalie hata na budget yake kiujumla lazima tuangalie implementation ya tactics zake na lazima tuangalie matokeo yake uwanjani. Nani asiyejua investment ya Red Bull kwenye Club ya Leipzig??? Nani asiyejua leipzig inavochukiwa n wajerumani kutokana na system zake za umiliki nani? Je hiyo investment inafanana na Atalanta. Je investment ya Leipzig inaendana na matokeo yake uwanjani??

Yupi ni kocha bora kati ya Gasperini na Ninglesman??? Rejea mafanikio ya kocha Arrigio Sacchi chini ya kina Baressi na Maldini na Costarcuta Na Vanbasten ambao most of the team walikua ni academy players na wengine waliosajiliwa kwa bei chee. Rejea na hapo utajua kuwa mpira ni Game of tactics

TACTICS ZA ATALANTA CHINI YA GASPERINI

Kama uliwahi kusikia kuhusu tiki taka basi italia kuna kitu kinaitwa Catenacio, hii ni aina ya uchezaji wa mpira inayohusisha timu kudefend effectively na pia kupanda na kushuka kwa pamoja huku ikihusisha mabeki wa kati watatu(centrale) na kiungo wa kati akicheza kama deep holding midfilder ambaye kuna mda anaplay role kama beki wa kati (mediano). Pia kuna nafasi kama destro . Regista, Terquista (nitaelezea siku nyingine)

Gasperini akiwa muumini mkubwa wa catanacio akiwa na formation 3-4-1-2 au 3-4-2-1 huku timu yake ikiundwa na wachezaji wanaojituma ambao wengi umri wao bado ni mdogo (age avarage ya timu ni 24 ) hii yote ni kuwafanya waweze kuhimili kupanda na kushuka mda wa kupandisha mashambulizi na kurudi kudefend kwa haraka.

Uwezo mkubwa wa Gasperini katika mfumo huu na unafikirisha kuhusu ubora kwa kocha huyu kwani Juventus chini ya kocha Maurizio Sarri wametengeneza chance chache za kufunga magoli na wanazidiwa hata na Leicester au Wolves. Rudi kwa Antonio Conte pamoja na usajili mkubwa alioufanya lakini bado timu yake inagombania kushika nafasi ya 3.

Je Gasperini si kocha bora?Perfomance ya Atalanta ni ya Kawaida?
Thomas Rongens Ulimaanisha nini???

Mwisho ni kwamba tutegemee makubwa toka kwa Atalanta msimu huu kwani sitoshangaa Wakifika nusu Fainali ya UEFA na zaidi ya hapo. Muhimu ni muda Tu
Umeshusha nondo za maana Mkuu. Kunywa barimi mbili ntalipa.
 
Kuna watu wakilala wakiamka wanawaza ligi ua uk ila kwenye uefa.ndio wanabahatika kuona timu nyingine Italy bado ligi yao ni bora hata hao milan waliolala wanakuja juu mwakani utawaona
 
Moja ya Sifa kubwa y Atalanta ni kuwa wamekua wakifanya vizuri kwa misimu kadhaa licha ya wachezaji wao bora wengi kununuliwa na timu kubwa. Conti, Kessié , Bryan Cristante, Mattia Caldara, Alessandro Bastoni, Gagliardini, Gianluca Mancini.
 
Na hawa jamaa hilo suala lakutupia magoli mengi halijaanza msimu huu, ni misimu kadhaa sasa toke aje huyu kocha scoring rate yao ni kubwa sana
 
Back
Top Bottom