Wastani wa hoja za wacahngiaji unakubaliana bila ya kujijua na hoja ya mtoa mada. Walio wengi wanakubali kwamba 'Simba na Yanga' huwa zinahonga. Lakini timu hizo hazichezi ligi ya peke yao. Kama kuhonga, zitahonga timu nyingine kwenye ligi hiyohiyo, ikiwamo Azam yenyewe. Kwa hivyo kama ni hatia, mtoa na kupokea rushwa wote wana hatia. Sasa kama mchezo huo upo kweli. hata kama wahongaji ni timu hizo mbili, maana yake ni kwamba mwaka huu umefanyika pia. Hivyo kweli ligi hiyo ni ya ubabaishaji, hata kama bingwa angekuwa Ashanti. Aidha, hakuna mchangiaji yeyote aliyebisha madai ya mtoa mada kwamba refa aliboronga kwa faida ya Azam kwenye mechi na Mbeya City, iwe kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Kwa asiye na upande kwenye hili, anashawishika kuamini kwamba mtoa mada yuko sahihi. Hasa ikitiliwa maanani mechi kadhaa zinazoihusu Azam ziliwahi kuchezeshwa namna hiyo misimu iliyotangulia. Mechi na Yanga iliyosababisha Cannavaro kufungiwa na Yanga kumpiga mwamuzi ilikuwa katika mazingira kama hao. Mwamuzi Ramadhan Ibada (Kibo) aliwahi kufungiwa kwa kuipendelea Azam kwenye mechi za Kimbe la Mapinduzi, iwe kwa makusudi au kwa bahati mbaya.Ndio maana kuna baadhi ya wachangiaji wamekuwa wakmtaka mwanzisha mada kuachana na wivu wakike. Bila ya kujijua, wachangiaji hao wanakusudia kwamba Azam iachwe ishinde kama ambavyo wanadhani Yanga na Simba zinashinda. Wastani wa hoja zote hizo ni kwamba kuna mushkeli mkubwa juu ya uungwana (fairness) wa matokeo ya mechi za Ligi ya Vodaco. Kwa maoni ya mtoa mada, huo ni ubabaishaji, na sitowashangaa wanaokubaliana naye. Ninaowangaa ni wanaotofautia naye huku wakijisema wenyewe kwenye hoja zao kwamba wanajua ukweli huo!