Soka la bongo ni ubabaishaji mtupu

Soka la bongo ni ubabaishaji mtupu

neindiwe

Member
Joined
May 21, 2012
Posts
33
Reaction score
22
Ligi kuu ya voda com inakwenda ukingoni. Pamoja na ligi hiyo kwenda ukingoni tumeshuhudia ubabaishaji wa hali ya juu hasa kipindi hiki cha mechi za mwisho. Timu zilionyesha wazi kupanga matokeo.

Mfano mech ya simba na Azam. Simba na Ashante. Azam na Coastal. Pia waamuzi walionekana kuvurunda sana. Mfano leo pale mbeya watu wote wameona kilichotokea kwa mwamzi kutoa maamuzi yasiyo na stahiki.Azam imekuwa bingwa lakini soka lake halilidhishi kabisa.

Kuna timu zilikuwa bingwa Tanzania mfano Pan Africa chini ya washambuliaji mahiri kama Peter Tino. Ali katolila. Abdala Burhan. Zilitisha sana hakuna aliyelalamilka.

Pamba ilikuwa bingwa hakuna aliyelalamika. Majimaji. Tukuyu. Naomba TFF mjipange vzr ili madudu haya yasirudie tena mwakani.
 
Jjipaangen ligi Upo na mwaka ni
 
Michepuko Ina raha zake mpwa mlipokea mill mia mkkahisi zitanena wapi
 
Hivi pamba ilishakuwa Bingwa ?..., I doubt it najua kina Tukuyu pia walishakuwa mabingwa, cheki vizuri makabrasha yako mkuu
 
Pamba iliwahi kuwa bingwa....Yaani Yanga na Simba wanadhani wao tu ndio wana haki miliki ya ubingwa.....Wameanza maneno ya fitna juu ya Ubingwa wa Azam.
Huo ubingwa wa fitna zimezoea Yanga na Simba,hamuwezi kujifananisha na Azam kwa ubora,wana uwanja,wana hostel,wana sehemu ya Gym,wanakula chakula kizuri na uwanja mzuri wa mazoezi...Nyie wengine mna shamba Boko kazi kupalilia bila maana,wengine mpo maporomokoni.Mpira ni sayansi sio majigambo na Siasa za Manji na Rage
 
Pamba iliwahi kuwa
bingwa....Yaani Yanga na Simba wanadhani wao tu ndio wana haki miliki ya
ubingwa.....Wameanza maneno ya fitna juu ya Ubingwa wa Azam.
Huo ubingwa wa fitna zimezoea Yanga na Simba,hamuwezi kujifananisha
na Azam kwa ubora,wana uwanja,wana hostel,wana sehemu ya Gym,wanakula
chakula kizuri na uwanja mzuri wa mazoezi...Nyie wengine mna shamba Boko
kazi kupalilia bila maana,wengine mpo maporomokoni.Mpira ni sayansi sio
majigambo na Siasa za Manji na Rage

kama hayo yote unayoona ndo ubora wa Azam kushinda Simba na Yanga,mbona nao wajiingiza kwenye hizi fitna za kununua mechi?
 
Muleta thread hizo ni dua ZA kuku. yanga nasimba wanaongoza kununua mechi na hasa kuwahonga wachezaji wa time pinzani. Hutaki soka la bongo, hAmia Somalia.
 
Mmezoea vya kunyonga,vya kuchinja hamuwezi! Na msimu ujao mambumbumbu fc lazima mshuke daraja.
 
Pamba haijawahi kuwa bingwa wa Ligi Kuu. Walikuwa mabingwa wa kombe gani lile lililokuwa linalounganisha timu za bara na visiwani?
Pamba walikuwa wanapoteza ubingwa wa ligi mwishoni mwishoni.....ila siku hizi naelewa kwanini ilikuwa inatokea hivyo.
 
azam%20bingwa.jpg

Wachezaji wa Azam wakishangilia Jana Uwanja wa Sokoine. Kulia John Bocco amemkumbatia Mwaikimba
 
Ligi kuu ya voda com inakwenda ukingoni. Pamoja na ligi hiyo kwenda ukingoni tumeshuhudia ubabaishaji wa hali ya juu hasa kipindi hiki cha mechi za mwisho. Timu zilionyesha wazi kupanga matokeo. Mfano mech ya simba na Azam. Simba na Ashante. Azam na Coastal. Pia waamuzi walionekana kuvurunda sana. Mfano leo pale mbeya watu wote wameona kilichotokea kwa mwamzi kutoa maamuzi yasiyo na stahiki.Azam imekuwa bingwa lakini soka lake halilidhishi kabisa. Kuna timu zilikuwa bingwa Tanzania mfano Pan Africa chini ya washambuliaji mahiri kama Peter Tino. Ali katolila. Abdala Burhan. Zilitisha sana hakuna aliyelalamilka
.Pamba ilikuwa bingwa hakuna aliyelalamika. Majimaji. Tukuyu. Naomba TFF mjipange vzr ili madudu haya yasirudie tena mwakani.

Ulitaka yanga ndo iwe bingwa..kwa mpira gani sasa?acha wivu wa kike
 
Hivi pamba ilishakuwa Bingwa ?..., I doubt it najua kina Tukuyu pia walishakuwa mabingwa, cheki vizuri makabrasha yako mkuu

kijana umezaliwa mwaka gani? .unamjua george masatu hussein masha john makelele niko bambaga haoni baadhi ya wachezaji wa pamba
 
naikumbuka sana pamba ya kina paul rwechungura,hamza mponda,khalfan ngasa,george magere masatu,hussein masha,david mwakalebela(enzi za kina dominic chilambo-rip na charles hilary) na wengineo iliyombamiza "ansebarou' (sina hakika na spelling) ya shelisheli. Jamani,wapi coastal union ya enzi hizo? Anyway,pengine ndo outcomes za professional soccer. Hivi hata total football ya waholanzi bado ipo kweli?
 
kijana umezaliwa mwaka gani? .unamjua george masatu hussein masha john makelele niko bambaga haoni baadhi ya wachezaji wa pamba

Mkuu mimi nilikuwa mshabiki wa Pamba hata kabla ya kina George Mabele Masatu..., Enzi za kina Joram Mwakatika, na Baadae Raphael Paul, as well as Khalfan Ngassa Babu..., Pamba ilikuwa timu nzuri sana ila kama nakumbuka vizuri haikuwahi kuchukua Kombe la ligi, ilichofikia karibu sana ni kuchukua kombe la Muungano (sikumbuki kipindi hicho lilikuwa linaitwa nini) kwa kufungwa na Malindi kwa penalty na kusema kwamba Kipa George Muhina alihongwa sababu aliruka upande mwingine penalty ikaingia upande mwingine..., ebu nikumbushe ilichukua kombe la ligi kuu Tanzania mwaka gani na kikosi kilikuwa na kina nani
 
Ulitaka nani awe Bingwa?Aliyetolewa na warabu wazee wenye stress za vita?Jipange mkuu usubiri mwakani

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Tukuyu stars ya mwaka 1985 ilikuwa kama Barca!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
tatizo mshakariri simba na yanga ndo sababu na mwakani tynabeba tena mpaka muache ujinga wa kukalili..
 
Jamani wacheni wivu Leo Azam imekuwa bingwa tuwape hongera zao tu sio kulalamika hata Yanga na Simba miaka kibao ubingwa wao wa kulipa waaamuzi pia kwanza Simba na Yanga ndio timu zimeziuwa timu Kama Pan African,Pamba na zengine nyingi nzuri kwa kuwaonea wivu na kuanza kuhonga mapesa Leo kashinda mwenzenu kumpa pongezi imekuwa tabu? Tujifunze kutoa pongezi bila lawama.
 
Back
Top Bottom