Soka la Bongo na kashfa za kulawiti

Soka la Bongo na kashfa za kulawiti

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,348
Wadau wa Soka la Bongo, kuna kashfa ya makocha na watu wa ufundi katika timu zetu kulawiti, na wakati mwingine kuomba rushwa ya ngono kinyume na maumbile kwa wachezaji wa kiume ili wawape namba kikosini.

Mambo haya si mageni masikioni kwangu, kama mnakumbuka klabu ya Simba iliwahi kukutwa na kashfa hii miaka ya 2000 kule Morogoro. Kashfa ikimhusisha wachezaji kadhaa na na aliyekuwa 'memba' wa benchi la ufundi wakati huo.

Binafsi nimeyasikia tena malalamiko kutoka kwa wachezaji ambao wameshawahi kupita katika timu hizi za Tanzania Premier League - Ligi Kuu. Bila kutoa 'ndogo' kwa kocha au kiongozi hupati namba kikosini na itaendelea kuwa hivyo.

Kuendelea kuyafumbia macho haya mambo hakusaidii soka letu, kama ni kweli maana yake wanadidimiza Soka na wakati huo huo wanaharibu vijana wetu kiafya na kimaadili. Nasikia kijana wa kiume ukishaanza ule mchezo huwezi kuacha, achilia mbali hatari ya kupata magojwa ya zinaa na VVU.

Kwa sababu fulani za kimaadili au kujuana na wahusika waandishi wetu wa habari hawajawahi kujadili kwa kina kuhusu tuhuma hizi, japo wanazifahamu kwa undani kabisa. Hapa ni mtandaoni na tunao uhuru wa kujadili kadiri tuwezavyo, kuwaanika wahusika na kupendekeza suluhisho.

Tujadili kwa uwazi.

10171109_971447929536952_3931625938031081304_n.jpg
 
Nahukuru kwa hii mada. ila ulivyoandika haitoi clue yoyote. ni sawa na waandishi wa magazeti wanavyoandika. Kama ulivyosema hapa ni mtandao na hatujuwani. kwa nini usizungumze na kuweka bayana angalau uliowahi kuwasikia.

Balantanda ana hint kuhusu nilichokisema katika aya ya pili kuhusu kocha na wachezaji wa Simba Sports Club. Nilikuwa bado mdogo wakati hili tukio likitokea, na kama unavyojua vyombo vyetu vya habari vilifunika kama halijawahi kutokea na hao watu hadi leo wana hatamu katika vilabu vya soka na hata timu za taifa za ngazi mbalimbali. Tizama alichokisema hapa katika hii post: https://www.jamiiforums.com/sports/327497-yanga-kushney-kwaheri-tom.html#post4681098
 
Last edited by a moderator:
Morinyo ni kocha wa chalsea, ila Iringa imetoa watu
 
Kipa wa zamani wa Simba wa Simba, Andrew Ntala alishawahi kuhusishwa na kashfa hizi. Haya ni mahojiano yake akikanusha taarifa hizo. KAtika kukanusha huko mwenyewe anakiri kuwa alishasikia teetsi za huyo kocha kuwa mdau wa mapenzi ya jinsia moja.

WIKI iliyopita, kipa wa zamani wa Kagera Sugar na Simba, Andrew Ntalla alielezea mikasa aliyokutana nayo kwenye Klabu ya Simba, nyakati ngumu na ahadi hewa kutoka kwa viongozi waklabu hiyo likiwemo suala la kukosa mahali pa kuishi wakati aliahidiwa kupewa nyumba ya kuishi.
Endelea…

NILIPOTOKA kwenye ile gesti ya Manzese ambayo walikuwa wamenipangia kisha kuhamia katika nyumba moja ya mzee Kinesi ambayo ipo Magomeni Kagera ambayo wanaishi wachezaji wa Simba B, kama nilivyosema kuwa mambo yalikuwa yaleyale.

Furaha yote iliondoka kutokana na mazingira mabovu kama vile wadudu wengi kwenye vitanda, kwa ufupi ni kuwa haikuwa nyumba nzuri ya kuishi mchezaji wa klabu kubwa kama ya Simba ambayo ina historia kubwa zaidi katika soka la Tanzania.

Maana ile kambi ni kama vile kambi ya mende, kunguni na mbu, ni kama hakuna mtu anayeishi humo ndani, labda kama wawe wametengeneza sasa hivi, lakini uliza hata wachezaji wa Simba wanajua hilo.

Sisemi yote hayo kwa kuwa sipo Simba, asikwambie mtu kaka, kuna baadhi ya wachezaji hapo Simba wana mateso makubwa, utakuta katika mikataba yao imeandikwa kuwa watalipwa shilingi laki nane (800,000) kumbe za kwao hapo ni laki nne (400,000).

Fedha nyingine ni za watu ambao wanawafanya waendelee kuwa klabuni hapo.

Ndiyo maana unaweza kuona mchezaji kiwango chake ni cha chini na hana sifa ya kucheza ligi kuu lakini hafukuzwi, kumbe yupo hapo kwa maslahi ya watu fulani.

Tuachane na hayo, mateso yalinizidi nikawa sina tena amani kwa sababu ya mazingira hayo mabovu niliyokuwa naishi, amani nilikuwa naipata pindi tulipokuwa tunakwenda kupiga kambi Bamba Beach.

Lakini baada ya kurudi kutoka huko, mawazo yaliongezeka kwa sababu nilikuwa naingia tena katika mateso makubwa.

Kila nilipokuwa nikiwambia viongozi wangu waliitikia tu kuwa watanitafutia nyumba lakini baada ya hapo hakuna aliyenijali, kila mtu aliendelea na 50 zake.

Kusema kweli hali hiyo ilikuwa ikiniumiza zaidi kila nilipokuwa nikifikiria hali nzuri ya maisha niliyokuwa nayo kabla ya kujiunga na Simba.

Msongo huo wa mawazo (stress) niliokuwa nao ulisababisha hata kiwango changu cha kudaka kushuka sana kwa kuwa muda mwingi nilikuwa nafikiria hatima ya mateso yote yale.

Kuna wakati ilifikia kipindi nilitumia muda wangu mwingi kufikiria maisha yangu nikiwa langoni na siyo kuwaza nini kinaendelea kwenye mechi husika.

Mashabiki wakawa wananitukana na kunilaumu kila mara, siwalaumu kwa kuwa siyo makosa yao na hawakujua lolote lililokuwa likiendelea.

Nilipoona mambo yanazidi kuwa mabaya nilikata tamaa na kuacha kujituma tena mazoezini na hata katika mechi.

Nilifanya hivyo kwa sababu niliona kuwa sithaminiki tena katika klabu hiyo, wachezaji wa kigeni walipokuwa wanafika tu siku chache wanapitiwa nyumba, mimi nikiendelea kusota katika jumba hilo bovu.

Hata hivyo mambo yalivyozidi kuwa mabaya ilinibidi niondoke katika nyumba hiyo na kwenda kuishi na dada yangu huko Salasala.

Nilifanya hivyo baada ya kumsimulia kila kitu juu ya shida hizo nilizokuwa nazipata Simba, alinishauri na kuniambia kuwa kama itawezekana ni bora niachane na soka kwanza nifanye mambo yangu na baadaye ndipo nirudi kuendelea kucheza.

Nilifanya hivyo na sasa namshukuru Mungu nina kwangu naishi na mke wangu, pia nafanyabiashara zangu za kuuza nguo nazitoa Dar es Salaam na kwenda kuziuza Mbeya.

Lakini wakati huo natoa Mbeya nafaka na kuja kuuza Dar es Salaam, maisha yanaenda vizuri, mtoto wangu Frank ambaye yupo darasa la kwanza anaendelea vizuri.

Kuhusu ushoga
Tuhuma hizo siyo za kweli na sijawahi kabisa kufanya jambo kama hilo maishani mwangu, huyo kocha ambaye walikuwa wananihusisha naye hata mawasiliano yake sina.

Siyo kwa sasa tu hata wakati nilipokuwa Simba sikuwa nayo, tulikuwa tunakutana mazoezi tu baada ya hapo kila mtu aliendelea na mambo yake.

Hata mimi nilikuwa nasikia tu watu wakimtuhumu kocha huyo kuwa anajihusisha na mapenzi ya jinsi moja lakini siyo kwangu mimi, kama alikuwa anafanya mchezo huo labda na wachezaji wengine.

Nakuhakikishia kwa mara nyingine tena kuwa mchezo huo sifanyi na wala sijawahi kufanya na waliokuwa wasema hayo sijui niliwakosea nini mpaka wakafikia hatua hiyo ya kunichafulia jina langu kwa kiasi kikubwa namna hiyo, Mungu yupo na atalipa.

Namshukuru Mungu kwa yote. Hakika uwepo wangu Simba umenifundisha mengi kuhusu maisha (Anainama na kufuta machozi).

Chanzo: GlobalPublishers
 
071 ndio maana tunafungwa kila siku..watoto sio ridhiki
 
kwa kifupi jibu ndilo hilo Simba hakuua na Ushga
Ushoga katika Kambi zozote hutokea wa ridhaa ya mtu mwenyewe akipenda
Magereza
Mabwenini
Hostel nk

Kuhusu ushoga
Tuhuma hizo siyo za kweli na sijawahi kabisa kufanya jambo kama hilo maishani mwangu, huyo kocha ambaye walikuwa wananihusisha naye hata mawasiliano yake sina.
Siyo kwa sasa tu hata wakati nilipokuwa Simba sikuwa nayo, tulikuwa tunakutana mazoezi tu baada ya hapo kila mtu aliendelea na mambo yake.
Hata mimi nilikuwa nasikia tu watu wakimtuhumu kocha huyo kuwa anajihusisha na mapenzi ya jinsi moja lakini siyo kwangu mimi, kama alikuwa anafanya mchezo huo labda na wachezaji wengine.
Nakuhakikishia kwa mara nyingine tena kuwa mchezo huo sifanyi na wala sijawahi kufanya na waliokuwa wasema hayo sijui niliwakosea nini mpaka wakafikia hatua hiyo ya kunichafulia jina langu kwa kiasi kikubwa namna hiyo, Mungu yupo na atalipa.
Namshukuru Mungu kwa yote. Hakika uwepo wangu Simba umenifundisha mengi kuhusu maisha (Anainama na kufuta machozi).
 
Ninazo habari za kutosha kuhusu hili, kwa sababu za kimaadili, sintaweka hapa majina, wengine washatangulia mbele za haki, baadhi wapo hai!

  1. Hata sasa hivi, yupo mchezaji mmoja wa SIMBA (ni fundi sana, wanamsifu kuwa ni mmoja wa wachezaji asieshuka kiwango kwa kipindi kirefu cha uchezaji), aliwahi kuchezea SIMBA, akaondoka, na msimu huu karudi tena, ana uhusiano wa moja kwa moja na mambo haya!
  2. Sio ktk soka tu, hata katika Bongo fleva, wasaniii mishumaa, mapresenter mishumaa!

Mungu atuapushie mbali!
 
Kama ushahidi upo kwanini usiwekwe hadharani, hii tabia ya kujidai ninao ushahidi ila siwezi weka ni danganya toto. Mfano Walcot na Ashley Cole walihusishwa na kashfa ya ushoga na vyombo vyao vya habari viliripoti, sasa kama bongo watu kama hao wapo kwanini wasiwekwe hadharani?

Asilimia kubwa humu tunatumia feki id so nini hofu? Come direct and say someone is a gay ili kufunga mjadala.
 
Nakumbuka enzi hizoo Sigara walikuwa na kocha mmoja anaitwa Magram alikuwa mbaya ktk masuala ya 0713 kiasi kwa wachezaji hawapangwi mfululizo mpaka atoe kitengo hicho,alale angoje kiama huko aliko akhera.
 
Nakumbuka enzi hizoo Sigara walikuwa na kocha mmoja anaitwa Magram alikuwa mbaya ktk masuala ya 0713 kiasi kwa wachezaji hawapangwi mfululizo mpaka atoe kitengo hicho,alale angoje kiama huko aliko akhera.

Mansour magram miaka ya tisini mwishoni akiwa kocha wa timu ya simba,alifumwa live akimlawiti mchezaji wake aliyekuwa akiitwa tomas karume
 
Inasemekana pia kuwa, kocha wa Yanga Saintfiet alifukuzwa kwa kuhusishwa na tuhuma za USHOGA, ambapo inasemekana mara kwa mara alikuwa akijifungia chumbani na CHUJI ndipo viongozi wa Yanga walipombana CHUJI kuwa anajifungia chumbani na kocha wanaongea vitu gani vya siri? Hapo ndipo CHUJI alipofunguka na kuwaambia viongozi kuwa "hakuna kocha hapa, ni mtoto wa watu huyu". Hapo ndipo viongozi wa Yanga wakaamua kumuondoa haraka. Wapenzi na Wanachama wa Yanga wa Morogoro na hata Dsm wengi wanafahamu suala hili.
 
kwa kifupi jibu ndilo hilo Simba hakuua na Ushga
Ushoga katika Kambi zozote hutokea wa ridhaa ya mtu mwenyewe akipenda
Magereza
Mabwenini
Hostel nk

Umeongea la maana, vipi kama kocha anapenda mwenyewe na anataka aruke na wachezaji. Huoni suala husika lina athari kwa mwenendo wa timu kiufundi na kimaadili?
 
Mansour magram miaka ya tisini mwishoni akiwa kocha wa timu ya simba,alifumwa live akimlawiti mchezaji wake aliyekuwa akiitwa tomas karume

Thomas KArume anatajwa mara nyingi kwenye sakata hili. Kuna wadau wanahoji kama nina ushahidi, kwanini mtu mmoja atajwe zaidi ya mara moja kwa jambo tata kama hili.

Karume huyu ndiye aliyetajwa tena kashfa ya Chachandu kule Morogoro?
 
Kuna moja ilitokea Copa coca cola kanda ya ziwa, Mbona wachezaji wanaliwa sana hasa ktk grass root level.. hadi kinyaa
 
Nilikuwa napiga misele bongo, nikakutana na timu moja airport. Nikafikiri ni timu ya shule ya sekondari jinsi watu walivyokondeana. Nikauliza hii timu gani, nikaambiwa hao Simba hao.

Nikahuzunika sana, kwa maana nilikiwa mpenzi mkubwa wa Simba zamani.

Nilivyosoma hivyo habari ya Andrew Ntala anabyoelezea walivyoishi it all makes sense mow.

Na inaelezea sababu nyingi kwa nini mpira wetu haukui.
 
Back
Top Bottom