"Basi Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake" Kwanini sisi tukaumbwa kwa mfano wa Mungu? kwani Mungu yukoje anafananaje? Mungu alimuumbaje Adamu?
Mkuu nimeona nianze na hayo maandiko na maswali maana yatakuongoza na ndo nayatumia katika maisha yangu ya kilasiku na nayatumia kuwafunza watu hasa walokata tamaa na kuwaumbia wanao na ndugu zao vibaya.
Ni hivi mkuu Mungu alisema mtu na awe na kweli mtu akawa na akawa na pumzi so Mungu aliumba kwa kinywa nasi tunauwezo wa kuumba kwa vinywa vyetu yani ukisema HUWEZI kweli hutoweza ila ukisema UNAWEZA kweli utaweza na ndo maana huwa hatushauri mtu kuita mtoto majina mabaya maana unaenda kumuumba kulingana na yale mabaya.
Hayo ni kulingana na imani
Kwa upande wapili Tatizo si tatizo tena ukishalijua, uzuri umelijua tatizo toka kiini mpaka hatua lilipo na inaelekea unauwezo mzuri wa kufuatilia na kubaini ni wakati sasa wa kubadili mtizamo, maana kinachokusumbua sasa ni mtizamo wako hasi kuwa huwezi kusidika na kuwa vile wengine walivyo kitu ambacho si kweli mkuu.
Pia
Dr. Wansegamila naona amekupa kitabu msaada sana katika kubadili mtizamo wako, so soma na weka mtizamo wako free usijiwekee mpaka ambao umeuweka kwasasa, usisome kitabu uku ukiwa na majibu yako kichwani na maamuzi yako tayari, naamini ukifanya hivyo utapata matokeo chanya na mazuri.
Nikupe pole na nikuombee mafanikio mema