Socialphobia, anxiety, depression, panic attack inaniua taratibu! Msaada

Kuhusu ushauri wa kuanza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mademu mimi sikushauri kabisa!

Nenda kwa kiongozi wako wa Kiimani kama vile Shekhe au Mchungaji/Padre kafunguke kwa msaada wa Mungu atakusaidia!
 
Imeandikwa:
“Mtu Aziniye na mwanamke hana akili kabisa,
Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake,
Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima,
Wala fedheha yake haitafutika!

Mithali 6:32-33
 
Hivi bongo hamna therapist wanaoshughulika na haya mambo ya anxiety na depression naona ni fursa ya kupata pesa sana madaktari fanyeni speciliazion kataika eneo hilo mfungue clinic mtapata pesa. Ni tatizo linalokuwa kwa kasi sana kwa sasa.
 
ID unayotumia inatanabaisha jinsi ulivyokata tamaa! Kufanikiwa au kufeli kunategemeana na wewe mwenyewe! Woga wako ndio umasikini wako. Pia huwezi kufanikiwa kwa kujifungia ndani, so nakushauri jichanganye na jamii inayokuzunguka itakuwa rahisi kwako kupata marafiki, kazi, mchumba/mke n.k.
Ila pole sana.
 
ID unayotumia inatanabaisha jinsi ulivyokata tamaa! Kufanikiwa au kufeli kunategemeana na wewe mwenyewe! Woga wako ndio umasikini wako. Pia huwezi kufanikiwa kwa kujifungia ndani, so nakushauri jichanganye na jamii inayokuzunguka itakuwa rahisi kwako kupata marafiki, kazi, mchumba/mke n.k.
Ila pole sana.

asante
 
Hivi bongo hamna therapist wanaoshughulika na haya mambo ya anxiety na depression naona ni fursa ya kupata pesa sana madaktari fanyeni speciliazion kataika eneo hilo mfungue clinic mtapata pesa. Ni tatizo linalokuwa kwa kasi sana kwa sasa.

Bora watoe huduma bure kuliko kutoza maana wengi watashindwa kumudu gharama zao
 
concordile 101, Hapo kuna mzazi wangu anahusika kwa asilimia 90%. Ningeweza kubadili kila kitu kuhusu mm maana mapungufu yangu nayajua ila sasa mkosi ulioje katika umri ambao sikutakiwa kuwa nyumbani nikajitegemee huko na maisha yangu ndo nimepata majanga yanayoniweka nyumbani 24/7 wala sina msaada wowote zaidi ya wazazi ambao nilitamani kuwa mbali nao ili nigrow katika kuamua na kujitegemea mwenyewe
 
"Basi Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake" Kwanini sisi tukaumbwa kwa mfano wa Mungu? kwani Mungu yukoje anafananaje? Mungu alimuumbaje Adamu?

Mkuu nimeona nianze na hayo maandiko na maswali maana yatakuongoza na ndo nayatumia katika maisha yangu ya kilasiku na nayatumia kuwafunza watu hasa walokata tamaa na kuwaumbia wanao na ndugu zao vibaya.

Ni hivi mkuu Mungu alisema mtu na awe na kweli mtu akawa na akawa na pumzi so Mungu aliumba kwa kinywa nasi tunauwezo wa kuumba kwa vinywa vyetu yani ukisema HUWEZI kweli hutoweza ila ukisema UNAWEZA kweli utaweza na ndo maana huwa hatushauri mtu kuita mtoto majina mabaya maana unaenda kumuumba kulingana na yale mabaya.
Hayo ni kulingana na imani

Kwa upande wapili Tatizo si tatizo tena ukishalijua, uzuri umelijua tatizo toka kiini mpaka hatua lilipo na inaelekea unauwezo mzuri wa kufuatilia na kubaini ni wakati sasa wa kubadili mtizamo, maana kinachokusumbua sasa ni mtizamo wako hasi kuwa huwezi kusidika na kuwa vile wengine walivyo kitu ambacho si kweli mkuu.

Pia Dr. Wansegamila naona amekupa kitabu msaada sana katika kubadili mtizamo wako, so soma na weka mtizamo wako free usijiwekee mpaka ambao umeuweka kwasasa, usisome kitabu uku ukiwa na majibu yako kichwani na maamuzi yako tayari, naamini ukifanya hivyo utapata matokeo chanya na mazuri.

Nikupe pole na nikuombee mafanikio mema
 
Uchira 1, Ahsante sana mku wangu kwa ushauri na nasaha, kuhusu kitabu cha Dr Wansegamila nimekisoma ila hakijaniletea impact yoyote kwenye maisha yangu nafkiri ni sababu ya mimi kuwa mzito kwenye kufanya maamuzi kwa vitendo, sina mtu/rafiki wa kuniforce/kunishika mkono kwenye kufanya maamuzi ya kwa vitendo
 
Mkuu nakushauri umuone psychiatrist, atakupa anti depressants,ukizitumia kama alivyokuelekeza hilo tatizo linaisha chap.
 
ahsante sana mku wangu kwa ushauri na nasaha, kuhusu kitabu cha Dr Wansegamila nimekisoma ila hakijaniletea impact yoyote kwenye maisha yangu nafkiri ni sababu ya mimi kuwa mzito kwenye kufanya maamuzi kwa vitendo, sina mtu/rafiki wa kuniforce/kunishika mkono kwenye kufanya maamuzi ya kwa vitendo
mkuu mtu hafundishwi akili, fika maahali uamue kubadilika kwakuwa unajua tatizo na unajua A to Z, ucngoje mtu akuforce amua kuwa mtu mpya japo kwakujilazimisha
 

Similar Discussions

20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom