Mimi na wengi tu akiwemo Raisi Kikwete,Edward Lowasa.Mizengo Pinda,Anna Makinda,Wilbroad Slaa,Anna makinda,Augustino lyatonga MREMA,freeman MBOWE na wengi tu tullisoma bure na kupata huduma bure kuanzia shuleni,kulala bure mabwenini,kula bure boarding kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu wengine wazazi walikuwa na uwezo mkubwa wa kusomesha watoto hata ulaya lakini walisoma bure na kutibiwa bure chini ya ujamaa.Wewe ndio nakushangaa kama umesoma hivyo vitabu ulivyosema hapo juu na hujui mwisho wa ideology iliyomo humo huwa ni kwa benefit ya masses na siyo minority.Ukisema ujamaa hautoi huduma bure naiachia hadhira ya jamii fforum iammue nani mbumbumbu wa kutupwa kati ya wewe na mimi .Ujamaa wengine tumeuishi hatukusoma kwenye vitabu na kukariri tupasi mitihani kama wewe sisi tunajua reality ya ujamaa kwa kuuishi siyo kuuona kwenye mashelf ya maktaba za vitabu.Na bahati nzuri tumeishi mifumo yote miwili ule wa ujamaa na huu wa kibepari sasa tunaweza kusema kwa kujidai kabisa tunadhani upi ni bora zaidi.Kwangu mimi nikilinganisha mifumo hii miwili ambayo yote nimeishi nimeiona nasema hivi UJAMAA HOYEE na UBEPARI ZII na naomba tuchague turudi kwenye ujamaa.