...Halafu Lizzy umenikumbusha kitu, kuna watu kila siku wanaweka updates zao tangu wanaamka, wanachokula, wanapokwenda,
na mapicha yao ya kila siku, .....akipotea siku moja, siku ya pili anahadithia alipopotelea jana....!
...hivi tafsiri ya siri ya mambo ya ndani ni nini vile?
Mbu mi nawapa mbinu ya kukwepa "mbona X kaLIKE picha uliyopiga beach mwenyewe ila hajaLIKE ile tulopiga wote?Mbona anaomba ujibu msg yake au muende 'inbox' kama wanavyoitaga wenyewe" na nyingine kama hizo.
Ni sawa tu na yale masharti usiguse simu yangu, usipokelee mbali, usifute msg.
Mambo ya ndani yamekua sio ya ndani tena aisee. Unakuta mtu kaandika kabisa "tonight i'm getting some". . . sasa jiulize wewe kama ndio X wake, mfanyakazi mwenzake au rafiki tu inakuhusu? Watu wanaruhusu hii mitandao iwafanye vichaa.
...hahahaha, huyo anayeandika atananihii usiku huenda anamrusha roho 'mgombea mwenza!'...
ila ndio kama unavyosema, kwa faida ya nani?
twitter hata matumizi yake magumu.
facebook unakuwa na friends 5000 na zingine pendings yaani unafans sawa na msanii mwenye jina tz
Yani, ni kaaazi kweli kweli.
Kuna mmoja nimeona kaandika leo hata kurudia kusoma sitaki, sasa sijui watu wanaomheshimu/anaowaheshimu watamchukuliaje baada ya kuandika alochoandika. It's kinda sad. . . watu wanakua malimbukeni bila hata kujua.
..hah? kiongozi hivi kuna umuhimu kumjua sijui kumfahamu ex wa mke/mume?
sasa wale one night stand utawa block vipi nao? nao wamo hao...
Angalau jf ni where we dare to talk openly, huko kwingine labda wanafuata msemo huu;
Be who you are and say what you feel because those who mind don't matter and those who matter don't mind.
...Huwezi kublock 100% lakini pale ambapo unaweza kublock basi sioni sababu ya kutofanya hivyo. Kumbuka kuna mahusiano mengi tu yameshavunjika kupitia Twitter, FB, Skype, emails na upuuzi mwingine. Sasa ili nawe usije kuongeza statistics za walioathiriwa na technology katika mahusiano basi unapoona jambo halikukaa sawa sidhani kama ni vyema kunyamaza kimya bila kutia neno.
Hhahahahaha. . . . haya bana.
BAK Xs wengine wanaweza wakawepo kwenye friends list na wasilete matatizo, wengine wanaweza wasiwepo na wakaleta matatizo. Alafu kumchunga sana mtu ni kazi ya ziada, sidhani kama hiyo nayo inatakiwa iwe kwenye "mahusiano package". . . watu wanatesana tu bure.
...aiseee,
wazee wetu wa walijikinga na boma tu ndoa zao zikasalimika,
sie leo tumeyakaribisha haya ya utandawazi,....mtu ana flirt kwenye mtandao
mpaka pembeni yako kitandani!
Nakubaliana nawe Lizzy lakini ni vigezo gani vitatumika Xs hawa hawafai kuwepo na wale wanafaa kuwepo? si ajabu hao waliobaki ndio hao wanajipitishapitisha kujaribu kumdowea mwenye mali 🙂🙂... Hii kitu ni ngumu sana kusema kweli 🙂🙂 ukiwa na wivu wa kufa mtu unaweza kupata uchizi 🙂🙂
Mwenye X ndie anaetakiwa kujua BAK. Yani kama mtu anajua X wake ni msumbufu,amewahi kumsumbua, hajatulia n.k asimuadd au amdelete bila mwenzake kumtaka fanye hivyo. Yani tusiwe kama watoto kila kitu mpaka mmoja aagize/alazimishe, tutumie common sense. Kama ambavyo hua tunawapotezea marafiki ambao tunaona hawatufai.
Mwenye X ndie anaetakiwa kujua BAK. Yani kama mtu anajua X wake ni msumbufu,amewahi kumsumbua, hajatulia n.k asimuadd au amdelete bila mwenzake kumtaka fanye hivyo. Yani tusiwe kama watoto kila kitu mpaka mmoja aagize/alazimishe, tutumie common sense. Kama ambavyo hua tunawapotezea marafiki ambao tunaona hawatufai.
..hhaaa?!
...hivi hujui kuna vichwa panzi wengine wanajua kwa idadi kubwa ya admirers na ex-'wapenzi' wanaokumbushana enzi zao online ndio naye anajijengea heshima na adabu (boost self esteem) kwa mume/mke'we hapo nyumbani?
...acheni nyie, hii mitandao hasa facebook inawakomoa wengi majumbani....refer post za Nyani Ngabu pale unapokuta mwenza anakataa kuku-accept friendship request, au akishaku add kuna post anakunyima access, au anaku delete!
Nakubaliana nawe Lizzy lakini tukumbuke kwamba common sense in not so common :rant:
Najua Mbu, ila kama mtu kuboost hiyo self-esteem mpaka X ahusishwe basi ana hasara. Hiyo inatakiwa iwe kazi ya mwenzi, kila mmoja amuongezee mwenzie kujiamini.
Naona dalili za kumuendea mtu BWAGAMOYO nikamtengeneze ntakavyo. . . . lolzz. . . maana mambo ya kuchungana mpaka usiku wa manane (asichat, txt na ongea na simu) sitoweza kwakweli.
....amaaa? sasa ilikuwaje mke nae aende utangazia ulimwengu, ndoa yake i mashakani?
mimi tatizo langu linaanzia hapo bana....
Najua Mbu, ila kama mtu kuboost hiyo self-esteem mpaka X ahusishwe basi ana hasara. Hiyo inatakiwa iwe kazi ya mwenzi, kila mmoja amuongezee mwenzie kujiamini.
Naona dalili za kumuendea mtu BWAGAMOYO nikamtengeneze ntakavyo. . . . lolzz. . . maana mambo ya kuchungana mpaka usiku wa manane (asichat, txt na ongea na simu) sitoweza kwakweli.
Hii kazi ya kukimbizana na vivuli siyo mchezo,
Honestly kazi ngumu kuifanya hata kwa malipo...
Jambo la muhimu ni kukubaliana mambo ya msingi kama alivyosema RR na kumwachia kila mtu ajichunge...Ila pia ni vizuri kuweka mstari ambao mtu akishauvuka ajue matokeo yake hata bila kuulizwa!!
...hahahaha, ndilo lililobakia, ...kulishana limbwata na kutegeana tego tu!
....kwa tafsiri ya maisha ya kileo status hiyo inaitwa OPEN RELATIONSHIP, au cheat responsibly :A S-coffee: