Lizzy, please mwambie Mbu asiweke 'likes' kwenye hilo kundi hapo juu!Mbu mpaka LIKE ni tatizo?
Haya ngoja wahusika watupe mbinu na maujanja.
...tangu mchipuko wa mitandao ya jamii kuibuka sambamba na teknolojia ya huduma ya internet kupatikana kwenye simu za mikononi, binafsi nishahadithiwa, kusoma na kujionea mipasuko ya ki mahusiano, mapenzi, urafiki na hata ndoa kutokana matumizi yasiyo sahihi ya mitandao hii.
...na hii haikuanzia kwa Facebook pekee, Friends Reunited, myspace, WAYN, Hi5, Twitter na hata Google + mitandao yote hii kwa namna moja au nyingine imegeuka hatarishi kwa usalama wa mahusiano, mapenzi urafiki na ndoa!
Je, kwa upande wako Unajiepusha vipi au, ...nini msimamo wako unapokumbana na comments za ajabu ajabu kwenye profile page ya mwenza wako, iwe ni kwenye wall, picha (incl tags), 'Questionable' friends au hata likes na private mails anazotoa na yeye anazopokea? how far can you tolerate each other,...au 'unakufa' na tai yako shingoni?
Lizzy, please mwambie Mbu asiweke 'likes' kwenye hilo kundi hapo juu!
Mbu mpaka LIKE ni tatizo?
Haya ngoja wahusika watupe mbinu na maujanja.
Hahahahaha, at least inaonesha it is not that complicated anymore, wameanza kukubaliana kwa status......hahahahaa, RR.....majuzi nilikuwa nasikiliza kesi ya facebook baina ya mtu na mkewe, kisa kwanini jamaa
kampa 'like' mkewe alipobadilisha status toka married to complicated!
....Mbu weye sikuwezi kwa threads zako zilizotulia. We acha tu hii technology inasababisha mavarangati makubwa sana ndani ya mahusiano. Pia kuna ile wenyewe wanadai kwa "wasomi" linkedIn huko nako kumesababisha mahusiano kuvunjika.
Hahahahaha, at least inaonesha it is not that complicated anymore, wameanza kukubaliana kwa status.
Mke kasema it is complicated, na mume kakubaliana nae. sasa kosa la mume nini jamani? Kwa hiyo mke alitaka wampinge?
Lizzy, please mwambie Mbu asiweke 'likes' kwenye hilo kundi hapo juu!
....eeehhh? e bwana weee? jana nimesoma mmoja katimuliwa kazi kisa kaweka CV yake kwenye Linkedn....kumbe hata huko kunavunja ndoa?
...tatizo ni nini? ...ni utandawazi, uwazi na ukweli unatuponza au? yale yaliyokuwa yamejificha vifuani, siku hizi ukiudhiwa tu unapandisha kwenye Twitter, au Facebook!
.....hahahahaa, RR.....majuzi nilikuwa nasikiliza kesi ya facebook baina ya mtu na mkewe, kisa kwanini jamaa
kampa 'like' mkewe alipobadilisha status toka married to complicated!
RR mwenyewe namshangaa maana hizo wengine hua wanagonga alimradi tu na wao waonekane "walikewepo. . . wameona".
...lol....ushafika, nilidhani ushalala...enhe...fungua darasa!
wewe hupekui kuchungulia kale kabinti kanakotoa likes hata "MR" akiandika mbofu mbofu?
...We acha tu Mkuu Mbu haya mahusiano ya siku hizi yana majaribu makubwa sana. Jamaa aliingia kwenye page ya mamsap kule linkeIn na kukuta jamaa kajaa tele halafu katika page yake kaanika kila kitu mpaka namba yake ya simu. Mwenye mali zake akanyanyua simu na kuanza kuvurumisha matusi ya nguoni huku njemba doezi ikidai kwamba ipo ipo tu hakuna chochote kinachoendelea. Mwenye mali zake akatoa dakika 10 tu kila ili njemba doezi ijifute katika page ya mamsapu au cha moto atakiona. Jamaa kuchungulia baada ya kumaliza kuvurumisha matusi yake akakuta kweli jamaa kajiondoa. Nilipohadithiwa hii nilitafakari sana jinsi ya mahusiano ya siku hizi yalivyo na majaribu mengi ukilinganisha na enzi zile za Wazazi wetu. Inasemekana Njemba doezi iliwahi kuwa karibu sana na mamsap miaka ya nyuma kabla hajaolewa.
Hahahahaha wewe ulikuwa hujui Malaika shauri yako lol!...Mie sipendi kila anachoandika nanihii umpe LIKES...basi unaona LIKES zinaingia mitini kimya kimya hahahah lol!
hahahahahahaha!.....hapo kesi haijaisha hiyo, ngoma kwa mkewe nyumbani!
balaaaa....sasa imagine angechungulia huko kwenye profile ya mkewe halafu
ajikute hana tena access, mkewe kesha m block zamani! weeeee....!