Social media na ndoa yangu


mkuu ninamengi ya kukujuza na. ninaamini yatakuwa msaada kwa ndoa yako...sema sipo na laptop...but hebu pitia kitabu flani hivi kinaitwa 5 LOVE LANGUAGES CHA DR. GARY CHAPMAN nna uhakika kitakuwa msaada mkubwa kwako...na hiyo ndoa utaifuraiya sana
 
kwa hiyo kaenda kuanika siri zako kwenye mitandao kuwa jamaa ni kibamia?!
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako ambao nikili uko vizuri sana. Nimemweleza yote na nimeenda nae pole pole sana lakini ni kama anafanya mambo kunikomoa. Nasema hivi kwa sababu kitu unachomwambia hukipendi yeye anakifanya muda huo huo ili kukuonesha kua anakifanya. Mimi nimehisi kua anaweza kua na spiritual hasband lakini hata jeuri na kiburi kinachangia sana. Suala la kuvunja ndoa nimelikifiria sana for 5 months now. Ukweli kutoka moyoni ni kua sioni future ila naona naweza kufa mapema. Sipendi kucheat ni maisha ambayo nimeyakataa toka moyoni na hua nipo clear sana.
 
Mkuu unavyo ongea inamanisha umevumilia mengi sana tumbua ilo jipu mkuu

Kuna mambo mengi but hayo ni sehemu tu ya mambo amabayo yananikera bora hata angekua anajieleza kutoa sababu za maana ila majibu yake ni simple kama "nimeamua", "mambo binafsi". Mimi naamini kitendo cha kumuoa tu ni upendo mkubwa, sisi wananume wakati wa kuchagua mtu wa kuoa tunachangamoto kubwa sana. Sasa ile kumchagua tu yeye ni upendo mkubwa.

Suala la kuweka picha yake facebook au whatsapp binafsi sioni kama ni muhimu kwangu. Mimi naamini siishi kuonesha watu nini nakifanya au kutangaza maisha ya mke wangu. Simple, naamini ili mradi ninatunza familia na nina amani ya moyo wangu tosha kabisa. Kama nitaweka mapicha hata 200 ila siko responsible kwa familia itasaidia nini? cha msingi nafikiri ni kutimiza majukumu ipasavyo na sio kuishi maisha ya kujishow kwa watu. Kuna jamaa nawafahamu kabisa ukiangalia profile zao zimejaa picha za wake zao,lakini wanavimada kila mtaa.

Ishu ya kuacha mke na kutomuacha mimi naamini liko katika amani ya moyo. Kama huna amani na maisha kwako unaona ni shida, nife na kitanzi shingoni wakati naweza kukitoa. Nimeshuhudia mzee mmoja kwa macho yangu anauwawa na mkewe live na sasa hayupo duniani. Mzee alikubali kufa na kitanzi shingoni wakati maisha tunaishi mara moja tu, hakuna part two ya maisha. Asante kwa ushauri mzuri
 
 
kuna umuhimu wa kuwashirikisha watu was karibu yenu kama vile wazazi wa pande zote mbili km unaona ushauri na maonyo yako hayatilii maanani

Katika ndoa nafikiri kuna mambo unakua huru kuwashirikisha wazazi na mambo mengine ni magumu sana inakua kama unawakosea heshima. Wazazi wangu naona sio vizuri kuwashirikisha maana ataona kama anaonewa na atasema hapendwi na wakwe. Kuna mambo niliongea na wazazi wake sikufualitia mrejesho wake maana nilikua kama nawapa information tu kua wasije wakashtuka lolote litakapotokea. Ukweli nimejaribu kutatua na nimetulia kwa muda kutafakari nacho kiona sijafika mabli sana katika maisha ili niwe huru na amani nafikiri tutengue ndoa kwanza then tupate muda wa kila mtu kutafakari upya juu ya mahusiano ya ndoa. Otherwise, maisha ni full frustrations.
 
Umeshaamua kumuacha, fuata taratibu zinazofaa.
Ndio kitu amabacho ninapangilia kwa sasa hasa kuangalia vipengele vya kisheria lakini pia kulinda heshima ya kila mtu. Ninajaribu kumshauri tuachane kwa amani japo hataki lakini ninamuandaa kisaikologia ili lisiwe jambo la kushtukiza tu. so nakwenda nalo pole pole huku nikijiandaa hasa kisaikologia na natumaini ndani ya huu mwaka mambo yatakamilika yote.
 
Lakini issue ni hiyo tu bro au na wewe hukumpenda kivileee heb eleza ukwel
 
Reactions: nao
Unazungumza na mkeo shida zenu? Ukimkera akikuambia upo tayari kuyaongea??
Make watu wengine hamuambiliki mtu anaona ajifariji mtandaoni na ujumbe utaukuta mtandaoni
 
Unazungumza na mkeo shida zenu? Ukimkera akikuambia upo tayari kuyaongea??
Make watu wengine hamuambiliki mtu anaona ajifariji mtandaoni na ujumbe utaukuta mtandaoni

Nafikiri hakuna situation ambayo inafanya mtu mzima na akili yake aweke family matters kwenye public walls. Kuna mambo we disagree kabisa lakini mazungumzo ni priority number one. Maana mtu anapoamua kubehave immaturely hapo ndo shida inaanza. Kwanza haijengi zaidi ya kubomoa. Maana hata kama kulikua na masikilizano kidogo inaua kabisa hata hio kidogo. Pili, hata kama kulikua na mapenzi nayo yanakufa. Situation inakua mbaya kuliko mwanzo, ndio maana wahenga wanasema ziba ufa kabla hujajenga ukuta. Nafiri nidhamu kwanza mengine baadae. Hata kama unakereka ni vizuri ukatumia heshima kuwasilisha ujumbe wako. Hakuna mume anaejitambua atakusikiliza kama humuaproach kwa heshima.
 
Hii mitandao imeharibu mambo mengi sana ukichanganya na ulibukeni wa sisi waafrika ndio kabisaa!
 
Ukishakamilisha taratibu za kumuacha hakikisha unaenda kuwaomba radhi mliowachangisha michango ya harusi kwa utapeli mliowafanyia. Ndo mana nilishaacha kuchangia michango ya harusi unakuta limtu kila siku mimassage ya mchango ukilichangia baada ya mwaka linaanza kusema eti huyu sio chaguo langu kweliiiiii!!!!! shame on you
 
Wengine njia hiyo inajenga ha ha ha ha ha
 
Hahahahaha aisee umeongea kitu cha msingi sana
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…