Snura aomba radhi kwa wimbo wa chura, aruhusiwa kufanya matamasha na atatoa video nyingine safi

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,542
7,450
Snura aliongozana na meneja wake, Hemed Kavu maarufu HK kwenye mkutano na waandishi ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam Alhamis hii.

“Mimi ni meneja wa Snura Mushi, tunaomba radhi kwa umma na Tanzania kwa ujumla kwa kosa la kutengeneza na kuzindua na kuweka mtandaoni video ya udhalilishaji wa mwanamke na isiyozingatia maadili ya kitanzania,” alisema HK.

“Aidha tunaomba radhi vyombo vya serikali, vinavyosimamia sekta ya sanaa kwa kutokufuata sheria, kanuni na taratibu katika uendeshaji wa shughuli za sanaa hapa nchini. Mimi kama meneja na msanii wangu tunaahidi hatutarudia tena kufanya tukio hilo la udhalilishaji, na iwapo tutarudia adhabu kali juu yetu zichukuliwe,” aliahidi HK.

Aliongeza, “Pia naahidi kuwa mfano bora kwa jamii inayotuzunguka, wasanii wenzetu katika kutunza na kufuata maadili na tamaduni zetu pamoja na sheria za nchi. Hii ni pamoja na kufuata sheria katika mamlaka na taasisi, tunafamu kwamba baadhi ya wasanii hasa hasa wa kizazi kipya, hawajajisajili Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama ilivyokuwa kwa msanii wangu, Snura. Lakini kwa sasa baada ya kupata maelekezo kutoka BASATA, Snura ameshajisajili. Pia tunawashauri wasanii kabla ya kufanya video ya wimbo, waende Bodi ya Filamu kwa ajili ya kupata vibali. Mwisho kabisa tunaahidi kutekeleza maazimio na maelekezo yote yaliyotolewa katika kikao cha Wizara. Maagizo hayo ni kutoa video kwenye mtandao wa YouTube na hilo tumeshalitekeleza, kujisajiri BASATA , tayari tumeshajisajili, na tatu ni la kuifanya upya video ya Chura ambapo mpaka sasa tumeshaandaa script na ipo Bodi ya Filamu inakaguliwa na kila kitu kinaenda sawa.”

Jana video na wimbo huo vilifungiwa na wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kwa madai kuwa inakiuka maadili ya Kitanzania. Pia alizuiwa kufanya maenesho ya hadhara kwakuwa hajajisajili kwenye baraza la sanaa la taifa, BASATA.

Kwa upande wake Snura alizungumzia kwanini aliamua kufanya video ya namna ile wakati anajua kufanya hivyo ni kosa.

“Labda nizungumze kitu kimoja, unajua kila mmoja ana upeo wake wa kifikiria, mimi wakati naanza hii video, kwa sababu nilijua ni Chura, na Chura anakaa kwenye maji, nikaona video ifanyike kwenye maji. Lakini baada ya kuiangalia video baada ya kuisha na watu nguo zao zilikuwa zimeloa, nikaona hii video haijakaa vizuri, nikachukua maamuzi ya kutoipeleka kwenye television na kuweka kwenye YouTube nikiwa na imani YouTube siyo sehemu ambayo watoto wanaruhusiwa kwenda. Lakini juzi baada ya kuitwa na Wizara nikaambia sheria ya makosa ya kwenye mitandao, hairuhusu kufanya hivyo, hivyo tunaomba radhi kwa kilichotokea,” alisema Snura.

160505081930_snura_mushi_2_640x360_bbc.jpg
Serikali ilipiga marufuku maonyesho yote ya hadhara ya Snura hadi pale atakapokamilisha usajili wa kazi zake za Sanaa katika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

160505082849_snura_mushi_640x360_bbc.jpg

Snura amewaomba radhi wananchi kwa kutoa nyimbo ya ‘chura’ ambayo imesitishwa na wizara ya Habari utamaduni Sanaa na michezo baada ya kuona nyimbo hiyo ina udhalilishaji na haipo kimaadili ya kitanzania.

Snura Mushi ameahidi kutotoa tena video yenye maudhui kama yale na tayari ameruhusiwa kufanya show katika majukwaa mbalimbali baada ya kujisajili baraza la Sanaa la Taifa na kupewa cheti.

Kibali.jpg
 
Kuna clip ya salama kwenye kipindi chake cha mikasi akitamka neno la kufedhehesha hivi TCRA haikumsikia?
 
ALIYETAMKA NI SALAMA AU HUYU MCHAGA WA MSOGA
TCRA wenyewe una zania wana ona ki2 ambacho akina madili bali wana kiacha kwanza adi wananchi wanzee kuu zozana ndipo nawo wanachukua atua angalao waonekane wako kazini lamda wange ifungia siku ambayo ime postiwa
 
Anataka Kuiga busying za Mawe sepeto?? Hive Yule mumewe bade Anaya au ndo m ajanga,??
 
Eti maadili ya Mtanzania.....hivi hao polisi wa maadili wanaishi huku huku uraiani tunakoishi sie wengine?

Halafu hao hao polisi wa maadili usikute ndo wanaopiga nyeto maofisini na hata hiyo chura usikute waliipenda.

Unafiki mtupu.
Mkuu huu wimbo wa Chura haupo kwenye maadili ya watani zangu Wachaga, hii hasa unaiona baada ya kuangalia video nyingi za wasanii zina mauno ya kutosha na yenye kutamanisha. Lakini Chura ya Snura Mushi inadhalilisha maadili ya watanzania hasa watani zangu.
 
Ni Salama nimeiweka hapo kwa vile kama ni kwa masuala ya maadili huyo binti alitamka hayo maneno na hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi yake!
SASA UNADHANI BILA USHIRIKIANO WETU HAWA MAJAMAA WA WIZARA HUSIKA WATAWEZA WENYEWE KUSEMA KWELI KAMA SI WATU KULALAMIKA MITANDANI HII VID INGEACHIWA IZAGAE KILA MAHALI WELL DONE
 
Mkuu huu wimbo wa Chura haupo kwenye maadili ya watani zangu Wachaga, hii hasa unaiona baada ya kuangalia video nyingi za wasanii zina mauno ya kutosha na yenye kutamanisha. Lakini Chura ya Snura Mushi inadhalilisha maadili ya watanzania hasa watani zangu.

Mauno ya Snura yana tofauti gani na mauno ya wasanii wengine (ukiachilia labda umahiri wake tu wa kuyazungusha)?

Hata Ali Kiba kwenye nagharamia anakata mauno....mbona ye hajafungiwa?
 
Snura alikuwa anatafuta kiki ya kutokea maana saivi kila kona ya social networks ni mwendo wa chura maana mtu haezi komment bila kuweka neno chura!!!
 
Back
Top Bottom