SMZ yawaomba radhi mabalozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SMZ yawaomba radhi mabalozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Aug 6, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeomba radhi kufuatia baadhi ya mabalozi wa nchi za kiarabu waliopo Zanzibar kuzuiliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Amani Abeid Karume mjini Zanzibar.

  Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais Mohammed Aboud amesema serikali itawahakikishia mabolozi waliopo Zanzibar na kutoka nchi nyingine kitendo kama hicho hakitatokea tena.

  Amesema wafanyakazi waliofanya vitendo hivyo watashughulikia ili kuona heshma na nidhamu inaendelea kuwepo kwa viongozi hao wa kimataifa walioletwa na nchi zao kudumisha ushirikiano.

  Awali mwakilishi wa jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan Juma alitishia kuzuwia kifungu cha fedha cha wizara ya miundo mbinu na mawasiliano wakati wakupitisha bajeti ya wizara hiyo akitaka serikali kutoa kauli juu ya kitendo cha kufungiwa geti maafisa hao wa kibalozi katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.

  Hata hivyo Juma ameitaka serikali kuheshimu sheria katika uteuzi wa viongozi wa mamlaka za taasisi za serikali badala ya kutumia utashi binafsi
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Aug 6, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  ..Waznz wamevunja katiba kwa kitendo cha SMZ kuwaomba radhi mabalozi.

  ..suala hilo lilipaswa kushughulikiwa na serikali ya MUUNGANO.

  ..ZNZ hawana waziri wa mambo ya nje, kwa hivyo mawasiliano yote na mabalozi ni lazima yapitie kwa MEMBE.
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Ni Mabalozi wadogo wanaowakilisha nchi zao wakiwa Zanzibar kwahiyo Zanzibar ina haki ya kuomba radhi

  Wana Naibu Waziri Wa Nje
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Aug 6, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  nngu007,

  ..mimi sijawahi ona mabalozi wakiwasilisha hati za utambulisho kwa Raisi wa serikali ya mapinduzi ZNZ.

  ..pia hakuna nchi inayowakilishwa ktk nchi nyingine na balozi mdogo. kilichoko ZNZ ni ofisi ndogo tu za balozi zinazowakilisha nchi hizo TANZANIA.

  ..kwasababu masuala ya mambo ya nje ni mambo ya MUUNGANO, anayetakiwa kuomba radhi kwa vitendo vya aibu vya SMZ kwa mabalozi wa nchi za nje ni waziri wa mambo ya nje ktk serikali ya muungano
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Ni Manaibu Balozi wanakwenda kumtembelea Rais wa Zanzibar Ofisini kwake na kuongea nae... na Saa nyingine

  Mabalozi wanakwenda kumtembelea Mfano hapa Balozi wa Japan

  [​IMG]
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mophamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Japan Nchini Tanzania,Mhe Masaki Okada,alipofika ikulu Mjini Zanzibar kusalimiana na Rais,
  [​IMG]
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mophamed Shein,akizungumza na Balozi wa Japan Nchini Tanzania,Mhe Masaki Okada,alipofika ikulu Mjini Zanzibar kusalimiana na Rais.
  Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar   
 6. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hao Mabalozi kwenda kumtembelea Dr. Shein haina maana kwamba kuna nchi inaitwa Zanzibar, wanatembelea sehemu ya Tanzania kama vile wangeenda Mwanza na kuongea na Mkuu wa Mkoa. Sasa likitokea jambo lolote huko linalohitaji kuombwa radhi hao mabalozi, Mkuu wa Mkoa hawezi kuchukua hilo jukumu. Ni kweli hapa Tanzania kuna mambo tunayafanya kienyeji sana kama protocol inayotumika Raisi wetu anapotembelea Zanzibar lakini hayo ni mambo ya jikoni tu kama "kitchen party" na hatuwezi kuyaendeleza kwenye medani za kimataifa. Tuache uswahili jamani, kuna mambo yanatuletea fedheha na dharau mbele ya macho ya watu waliostaarabika.
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Aug 6, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  nguu007,

  ..ur 100% correct.

  ..Mabalozi wanaweza kumtembelea Raisi wa ZNZ pamoja na viongozi wengne wa ZNZ.

  ..Pamoja na hayo, mabalozi hao hawawezi kuwasilishi HATI ZA UTAMBULISHO kwa Raisi wa serikali ya mapinduzi ZNZ.

  ..suala lingine ambalo nadhani haliwezi kutokea, ni Raisi wa ZNZ kupokea UJUMBE MAALUM toka kwa Raisi wa nchi nyingine.
   
 8. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,948
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  hainihusu!
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  By JokaKuu

  Hawa Wote wanawapeleka Hati zao kwa Rais wa Zanzibar

  [h=2]India's Consul General visits MCT's office in Zanzibar[/h]WEDNESDAY, 01 AUGUST 2012 12:14
  [​IMG][​IMG][​IMG]

  [​IMG]

  The Consul General of the Indian Consulate in Zanzibar, Pawan Kumaar, has expressed readiness to work closely with
  the Media Council of Tanzania and asked the Council to publicise India's training opportunities.
  Kumaar said that India has training opportunities for developing countries in various disciplines including journalism and urged Tanzanian journalists to utilize them.
  Consul General Kumaar was speaking at MCT offices in Zanzibar on August 2, 2012 when he paid a courtesy call.
  He said the training is provided in two phases and lasts 38 weeks adding that they will be useful in raising the capacity of journalists in various areas.
  "The training is fully sponsored by the Indian Government and is specialized for developing countries", he said pointing out that it was pertinent the journalists are aware of such opportunities and fully utilize them.

  MSAADA WA CHINA KWA ZANZIBAR

  Na Hamad Hija-Maelezo Zanzibar

  Waziri wa Habari utamaduni utalii na michezo Zanzibar Said Ali Mbaruok ameiomba Serikali ya China kuwapatia mafunzo waandishi wa habari na watangazaji wa Zanzibar ili yasaidiye kurahisisha majukumu yao ya kazi za kila siku katika sehemu zao.

  Waziri Mbaruok ameyasema hayo leo huko ofisini kwake Kikwajuni mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na Balozi mdogo wa china aliyepo Zanzibar Bibi Sheen Limun ambapo wamebadilishana mawazo juu ya mambo mbali mbali.

 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Hawa Wote wanawapeleka Hati zao kwa Rais wa Zanzibar

  India's Consul General visits MCT's office in Zanzibar

  WEDNESDAY, 01 AUGUST 2012 12:14
  [​IMG][​IMG][​IMG]

  [​IMG]

  The Consul General of the Indian Consulate in Zanzibar, Pawan Kumaar, has expressed readiness to work closely with
  the Media Council of Tanzania and asked the Council to publicise India's training opportunities.
  Kumaar said that India has training opportunities for developing countries in various disciplines including journalism and urged Tanzanian journalists to utilize them.
  Consul General Kumaar was speaking at MCT offices in Zanzibar on August 2, 2012 when he paid a courtesy call.
  He said the training is provided in two phases and lasts 38 weeks adding that they will be useful in raising the capacity of journalists in various areas.
  "The training is fully sponsored by the Indian Government and is specialized for developing countries", he said pointing out that it was pertinent the journalists are aware of such opportunities and fully utilize them.

  MSAADA WA CHINA KWA ZANZIBAR

  Na Hamad Hija-Maelezo Zanzibar

  Waziri wa Habari utamaduni utalii na michezo Zanzibar Said Ali Mbaruok ameiomba Serikali ya China kuwapatia mafunzo waandishi wa habari na watangazaji wa Zanzibar ili yasaidiye kurahisisha majukumu yao ya kazi za kila siku katika sehemu zao.

  Waziri Mbaruok ameyasema hayo leo huko ofisini kwake Kikwajuni mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na Balozi mdogo wa china aliyepo Zanzibar Bibi Sheen Limun ambapo wamebadilishana mawazo juu ya mambo mbali mbali.
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  msibishane. Hivi karibuni zanzibar itakuwa nchi kamili
   
Loading...