SMZ yavunja nyumba za mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SMZ yavunja nyumba za mawaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mallaba, Dec 29, 2010.

 1. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  SIKU chache baada ya kupiga marufuku ujenzi eneo la Mombasa kwa Mchina nje kidogo ya Mji wa Zanzibar, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetoa amri ya kuvunjwa nyumba zote zilizojengwa eneo hilo.

  Agizo la kuvunja nyumba hizo ambazo nyingi ni za vigogo wa serikali na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), lilitolewa juzi jioni na Makamu wa pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd , alipotembelea eneo hilo.

  Baadhi ya vigogo wa serikali na viongozi wanaodaiwa kujenga eneo hilo ni Waziri wa Wizara Maalum, Suleiman Othman Nyanga na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz.
  Hivi karibuni serikali ilifutia vibali viwanja vyote vya ujenzi eneo hilo kwa kile ilichoeleza kuwa, ni eneo la wazi ambalo halipaswi kumilikiwa na mtu.

  “Haiwezekani kubakia na mambo ya upuuzi, upuuzi huu, hapa serikali ilishasema pasifanyiwe jambo lolote, inakuwaje pale kuna nyumba inajengwa na nyie mpo hapa hapa? Eeeh vipi eee…. inakuwaje?” alihoji Balozi Idd kwa hasira alipozungumza na watendaji wa serikali wanaohusika na ardhi na viwanja na viongozi wa halmashauri.
  Kutokana na hali hiyo, Balozi Iddi aliwataka viongozi hao kuhakikisha majengo yanayoendelea kujengwa kubomolewa yote ndani ya wiki mbili na kontena lililowekwa eneo hilo, liondoke mara moja.

  Hivi karibuni serikali ilifuta vibali vya wamiliki 20 wa viwanja eneo hilo ikieleza kuwa, haliruhusiwi tena kujengwa kitu chochote.

  Licha ya kufutiwa vibali hivyo, serikali iliwataka wamiliki hao kurudisha nyaraka walizopewa ndani ya kipindi cha wiki moja kutoka siku waliyopewa amri hiyo, suala ambalo baadhi yao walishatekeleza.

  Wakati wasimamizi wa ardhi wakishindwa kumweleza Balozi Iddi jinsi eneo hilo linavyoendelea kujengwa, habari zinasema wamiliki wake ambao wengi ni mawaziri na vigogo serikalini, wamekuwa wakijenga nyumba zao usiku baada ya agizo hilo.

  Wasimamizi wa ardhi walimweleza Balozi Idd kuwa, hawana taarifa za ujenzi huo kuendelea kwani, wamiliki wote wanakwenda wakijua eneo hilo limepigwa marufuku.
  Balozi Idd alisema serikali haiwezi kunyamazia utendaji huo alioita mbovu unaofanywa na watu wachache kwa maslahi binafsi.

  Alisema ziara yake eneo hilo imekuja baada na sababu zingine baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kuendelea kwa ujenzi, ilhali limepigwa marufuku.

  “Inashangaza kuona tayari amri ya serikali ipo, lakini viongozi wamekuwa wakiachia watu kujifanyia mambo watakavyo huku waliopewa dhamana ya kusimamia hilo wakiwa watazamaji,” alisema.

  Mkurugenzi wa Ardhi na Usajili, Salum Simba, alisema idara yake ilishatoa amri ya kufuta viwanja hivyo, lakini hawafahamu jinsi baadhi ya watu walivyoamua kukiuka amri hiyo.

  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Magharibi, Hamid Tahir Lupindo, ambaye ni miongoni mwa watendaji waliokuwepo kwenye ziara hiyo, alionekana kushtushwa baada ya Balozi Idd kumuonyeshea kidole kwa kuwa yeye ndio msimamizi mkuu wa halmshauri hiyo.

  Tahir aliahidi kwamba watafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na serikali na watahakikisha amri ya kuondoa majengo inamalizika kwa muda ulipangwa.

  Mwannchi.
   
 2. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kama vile Merehemu Umaru yaradua (RIP) wa Nigeria
   
 3. C

  CHE GUEVARA2 Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zanzibar mpya ,serikali mpya na sheria mpya haha wale viongozi na vigogo wote wa serikali ya zamani waliokuwa wanaiba mali ya uma na kuchukua ardhi za Wa zanzibari wanyonge wajitayarishe kurudisha mali za uma au watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria:A S-alert1:
  **********CHANGE WE NEED*************
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Tunahitaji viongozi wa aina hiyo.
   
 5. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kweli lakini tunao kweli?
   
 6. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  yes we do
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Utawala wa mkoa wa mjini /magharibi una mashaka makubwa na hasa linapokuja suala la ardhi..
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hivi bado hamujaelewa kama CUF inaongoza serikali huko Zanzibar ??? Wekeni mawazo yenu na fikira zenu sawa kisha pambanueni pimeni na mchakachue ,mtauona ukweli !!
   
Loading...