SMZ: Kwanini wajumbe wapande daladala? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SMZ: Kwanini wajumbe wapande daladala?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, May 10, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Usafiri wa daladala Zanzibar


  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema hakuna sababu kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, kutumia usafiri wa daladala wakati Serikali ilishawapa fedha za kununua magari siku nyingi.

  Hayo yameelezwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, kufuatia Mwakilishi wa Jimbo la Tumbe (CUF), Ali Mhammed Bakari kufunguliwa mashtaka Polisi kwa tuhuma za kumpiga mchuuzi wa samaki baada ya nguo zake kuchafuliwa na vumba la samaki ndani ya daladala.

  Waziri Hamza alisema Serikali imekuwa ikiwagharamia wajumbe usafiri kwa kuwapa posho ya mafuta kila siku ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao katika mazingira ya utulivu.

  “Hakuna sababu kwa Wajumbe wa Baraza kutumia usafiri wa daladala kwa vile wote wanalipwa posho za mafuta,” alisema waziri Hamza.

  Alisema Serikali iliamua kuwapa fedha tasilimu Wajumbe wa Baraza hilo ili wanunue magari lakini inashangaza kuwepo baadhi yao wakionekana kutumia usafiri wa daladala wakiwa katika majukumu yao.

  Waziri Hamza alisema Serikali inafahamu kama Mwakilishi wa Jimbo la Tumbe amefunguliwa mashtaka katika kituo cha Polisi Wete Pemba na Serikali inaviachia vyombo vya sheria ili kuona haki inatendeka katika suala hilo.

  Waziri Hamza ambaye ni Waziri dhamana wa masuala ya Baraza la Wawakilishi alisema kwa kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inasimamia misingi ya utawala bora ndo maana imeshindwa kuingilia kati suala hilo ili kuvipa nafasi vyombo vya sheria kuamua kwa kuzingatia ukweli wake.

  Hata hivyo alisema wajumbe wote wa Baraza hilo wanayo kinga ya kutokamatwa na Polisi wanapotekeleza majukumu yao lakini wanapokuwa nje ya Baraza kinga hiyo hutoweka na kuwa sawa na raia wengine.

  Aidha, alisema Serikali haijafuta posho za mafuta kwa Wajumbe wake kwa vile kazi wanazofanya ni nyeti na wanahitaji usafiri wa uhakika wanapokuwa katika majukumu ya kuwatumikia wananchi katika majimbo yao.


  CHANZO:
  NIPASHE JUMAPILI
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ingawaje hatua alizochukua mwakilishi huyu dhidi ya mchhuzi wa samaki hazistahili kuungwa mkono, mimi nafikiri kupanda daladala kunategemea sana mazingira ya wakati huo kwani posho ya mafuta pekee siyo inayoendesha gari. Inawezekana alipata breakdown akajikwamua kwa kupanda daladala ili afike aendako na baadaye afanye mpango wa matengenezo ya gari. Wakati mwingine inawezekana alikuwa anakwenda gereji.

  La msingi hapo ni kwamba anapopanda daladala ajue kuna adha atakutana nazo na awe tayari kuzikabili bila jazba wala kuleta rabsha zitakazompa usumbufu, kuaibika na hata kuzua maswali kama haya yanayojitokeza sasa ya yeye kupanda daladala ilhali yeye ni mtu mkubwa sana.
   
 3. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haya ndiyo tunayakataa ya kuweka matabaka ya wengine kuonekana wana hadhi ya kutopanda daladala na wengine daladala ndio stahili yao katika nchi inayohubiri juu ya haki na fursa sawa kwa wote! Kwani Mjumbe wa Baraza la wawakilishi ama Mbunge akipanda daladala kuna tatizo gani mbona wananchi wengine wanapanda?
   
 4. T

  Tom JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni wazo zuri kupunguza gharama na msongamano wa magari ili kupunguza pollusion, huyo mwakilishi nampongeza kupanda daladala. Afu hizo posho za mafuta zingeondolewa, kwani baikeli ingefaa sana kwa matumizi ya wawakilishi
   
Loading...