Smile Karibuuu! Tulikumiss ile Mbaya.

Michael Scofield

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
1,225
471
Smile jamvini karibu, Japo waona aibu.
Mimi si mtabibu, Ila mama Umemtibu.

Member wote tuliomba, Mama apate kupona.
Sina haja ya kupamba, Kila mtu aliona.

AshaDii alikwambia, Mungu ataporidhia.
Daktari kumfikia, Maradhi yatamwishia.

Russian Roulette pia, Nae nilimsikia.
Kwa watu akisifia, Mama wamemtibia.

Kuna mengi umekosa, Pindi ulipoondoka.
Kongosho katolewa posa, Bishanga ameropoka

Kuna mkwe Mtambuzi, Jana ameleta uzi.

Msaidizi wa kazi, Alivyompa mauzi.

Asprin nae kalia, Pale aliposikia.
Kongosho hana jinsia, Kumbe anamwibia

Cantalisia binti Mtambuzi, Juzi alipata buzi.
Katuacha vinywa wazi, Baba yake kaliuzi.

Ivuga mtakatifu, Ametuwekea bifu.
Mwali kwake mtiifu, Tusitake kumsifu.

Preta ameridhia, Wewe hapa kurejea.
Japo alikawia, Kumtuliza Rejea. (Rejao)

Hata mimi sikutaka, Husninyo kunifata.
Marytina kishahapa, Kwako sitotoka kapa.

Kama kuna member nimetumia jina lake vibaya! natanguliza Samahani.
Lakini sina nia mbaya ni utenzi tu!
 
Jamani nilisahau doh, pole na kuuguza dada.

Huyo wa mistari anakupambaje baada ya valentine?
Karibu dada, hali ya mama inaendeleaje mkuu.
 
Smile jamvini karibu, Japo waona aibu.
Mimi si mtabibu, Ila mama Umemtibu.

Member wote tuliomba, Mama apate kupona.
Sina haja ya kupamba, Kila mtu aliona.

AshaDii alikwambia, Mungu ataporidhia.
Daktari kumfikia, Maradhi yatamwishia.

Russian Roulette pia, Nae nilimsikia.
Kwa watu akisifia, Mama wamemtibia.

Kuna mengi umekosa, Pindi ulipoondoka.
Kongosho katolewa posa, Bishanga ameropoka

Kuna mkwe Mtambuzi, Jana ameleta uzi.

Msaidizi wa kazi, Alivyompa mauzi.

Asprin nae kalia, Pale aliposikia.
Kongosho hana jinsia, Kumbe anamwibia

Cantalisia binti Mtambuzi, Juzi alipata buzi.
Katuacha vinywa wazi, Baba yake kaliuzi.

Ivuga mtakatifu, Ametuwekea bifu.
Mwali kwake mtiifu, Tusitake kumsifu.

Preta ameridhia, Wewe hapa kurejea.
Japo alikawia, Kumtuliza Rejea. (Rejao)

Hata mimi sikutaka, Husninyo kunifata.
Marytina kishahapa, Kwako sitotoka kapa.

Kama kuna member nimetumia jina lake vibaya! natanguliza Samahani.
Lakini sina nia mbaya ni utenzi tu!

Kweli, watu wakitaka kula tunda wananyenyekea kama wewe,
hongera sana, je mtoto mwenyewe amekuelewa.
 
Michael Scofield, mkuu unatisha!
Hatimaye my darling barafu wangu wa moyo Smile ametabasamu.
Thanx kwa kazi nzuri
 
Back
Top Bottom