mtazamo wako upo sawa, Mleta mada amesema
CAMERA YA KIBIASHARA Sio tu kamera. sasa tukizungumzia kamera ya kibiashara ni kamera inayoweza kushindana katika soko la biashara ya photographing. na hapo tunaongelea Professional cameras.
Hiyo LG G4
View attachment 487102
hata kama inayo manual control ya shutter, lakini haina mechanical shutter hizo tu ni software settings, yaani kila kitu hapo ni software hakuna cha mechanical Apperture setting, Hakuna manual focus kwa sababu lens ni Fixed.
Ukichukua camera kama CANON 1100 , unapopiga picha unasikia kabisa mtetemeko wa shutter inavyofanya yake huko ndani. pia unapanga mwenyewe Arpeture size (Kiasi cha mwanga unaoruhusiwa).
Kuwa na PIXELs nyingi sio ubora wa kamera hata kidogo, hiyo simu yenye 16MP inaweza kupitwa hata na kiCamera cha Sony DSC 930 (
hiyo ni kwa mfano).
Angalia uwezo wa Flash ya camera za kawaida, yaani kwenye giza ukipigwa flash hadi macho yanaona giza mara 2 zaidi, na ukilazimisha flash mwenye mwanga picha inakuwa Over exposed,kitu ambacho kwenye simu ni nadra sana.