Smartphone sasa balaa

Smartphone sasa balaa

Eyoma

Senior Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
166
Reaction score
40
Zinapunguza wateja mahotelini kwenye mabaa kwa kuwa mtu afikapo anakaa tuu anaanza kuchati mara Whatsapp,kisha Facebook, alafu instagram, anamalizia na Jamiiforums ndo unasikia niletee mchemsho, akimaliza kula anaanza tena kuchati weee,

Inaudhi sana hata kwenye usafiri mtu hakuna hata kubadilishana habari au maongezi jitu linakaa linaanza na kuchati tuu, tena zaleta ajali pia kuweni makini.
 
Muone huyo hapo kwenye basi anavochati wee hebu msalimie huyo jirani yako kwanza ukipata matatizo safarini ndo unaanza ooh habari yako.ni shidaaaaa
 
Du yaani hamna mwenye nafuu, si wewe wala mimi, wote yunachart tu! cc: Thw priest!
 
Rose muhando ameimba wimbo unaitwa facebook unazungumza haya yote
 
Utakuta mtu anacheeka peke yake hadi anatoa machozi hee.wehu huanza taratiiibu
 
Kuna ukweli, hizi smartphone zimepunguza sana one-on-one interaction. Ukienda sehem unaweza kukaa pekeyo hamna wa kuongea nae coz everyone's busy with their phones. Wakati mwingine umekaa na mwenza wako, ukitegemea muongee constructive issues yeye ni busy na sim.
 
ni shida new world order mkiabiwa sasa hivi kila goti litpigwa kwa shetan mnabisha...! taratibu hapa wajinga ndiyo waliwao ata ufanisi wa kazi maofisini umepungua hakuna concetration ya kazi. kazi zina a lot of errors.
 
Smartfon ilinisaidia sana kutafuna mabebeez watamu, enzi hizo hazijawa yebo yebo...

Saivi habari ya mjini ni liverossa tu...
 
hahahaha utakuta mtu anakula mpo nae, ye anamkaribisha mtu wa mbali kwa watsap et "karibu tule beby" , beby mwenyewe yupo dar nyie mliokuanae tanga, tena meza moja mnabaki kutoleana mimacho tu....
 
Mwee wengine hatupendagi mastory na MTU kwe gari salaam baas nipo bize na sim yangu safari yenye unaona fupi !!
 
Zinapunguza sana hata utendaji kazi na concentration ya kufikiria mambo mengine ya maendeleo, mfano mtu all the time unachat huku headphones zikiwa masikioni, utakuwa na mad wa kufikiria issues zingine? Wazungu wametuweza sana jamani. Ni nadra sana kumkuta mzungu anachat kwa cm au anasikiliza mziki masikioni.... We've to change, hasa wadada!
 
Inaudhi sana hata kwenye usafiri mtu hakuna hata kubadilishana habari au maongezi jitu linakaa linaanza na kuchati tuu, tena zaleta ajali pia kuweni makini.

aisee! Yaani umesema nilichokua nafikiria muda huu,nipo kwenye basi nimekaa na watu hapa kila mtu na lismati foni lake. Kwa kweli haijakaa vyema.
 
Ckuiz kila mtu Full time kuchart mpaka maofisini,tena zinamaliza Vocha ni kwamba hatugundui unaeza kujikuta kwa mwezi unatumia hela nyingi kuweka vifurushi. All at all zitumike constructively kama kuperuzi habari muhimu, kutafuta fursa mbalimbali kama ajira kuliko kutumia kwa mambo yasiyo ya msingi muda wote!
 
Smartphones kama ugonjwa vile kwa waafrika. Naamini tutakuja kuzizoea baadae kidogo.
 
na hata kutongozana siku hizi ni kwa smartphone, wacha ziendelee tu, ukitaka story jioni kijiwe cha kahawa na pweza.
 
Hili nalo litapita....

Zinapunguza wateja mahotelini kwenye mabaa kwa kuwa mtu afikapo anakaa tuu anaanza kuchati mara Whatsapp,kisha Facebook, alafu instagram, anamalizia na Jamiiforums ndo unasikia niletee mchemsho, akimaliza kula anaanza tena kuchati weee,

Inaudhi sana hata kwenye usafiri mtu hakuna hata kubadilishana habari au maongezi jitu linakaa linaanza na kuchati tuu, tena zaleta ajali pia kuweni makini.
 
Hili nalo litapita....

Kama DENGUE lakini EBOLA ndio inatesa!!! Huko China tayari kuna hospitali zimefunguliwa zinazotibu wagonjwa wenye addiction ya smartphones na internet!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom