Smartphone iliyopotea

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
15,267
Reaction score
25,557
Wadau nilipolwa smartphone yangu na vibaka siku kadhaa zimepita na mpaka hapa nimekwenda kulipoti police but sijapata muhafaka jinsi ya kuweza kuipata, msaada toka kwenu ni njia gani muhafaka inaweza kufanikisha kuipata au kuizima Kwa kutumia hizo namba IMEI au njia nyingine?

Nawasilisha.
 
Kwani uliweka program gani,maana kuna programme nyingi sana za kutafuta hiyo simu kama uliziweka
 
acha roho mbaya unataka kuifunga halafu iweje!
 
Rudi tena polisi ufuatilie utafanikiwa maana nimeshashuhudia jamaa zangu 2 wamefanikiwa. Polisi na kampuni ya simu uliyokuwa unatumia line hiyo wanawasiliana na mwishowe mwizi atajulikana tu
 
TCRA walitoa sheria kuwa kila kampuni ya simu iwe na equipment identification system ili kulinda simu za wateja.So kama alivyoshauri mdau mmoja,nenda kampuni ya simu na polisi.Wao wanajua.
 
mi ndo maana nimeweka avg antivirus hats nikiibiwa najua naweza kufuta data zangu na kulock kupitia email...yaani ni nzuri hata ukibadili line wanakutumia email kukujulisha line imebadilishwa kwenye simu yako
 
TCRA walitoa sheria kuwa kila kampuni ya simu iwe na equipment identification system ili kulinda simu za wateja.So kama alivyoshauri mdau mmoja,nenda kampuni ya simu na polisi.Wao wanajua.

kuwe na centralized eir ndio suluhisho,iwe inamenejiwa na third party,that means nikiibiwa simu nikiripoti tu kwa service provider basi iwe blacklist na haiwezi kukamata mtandao wowote duniani,challenge iliyopo je operators wapo tayari kuimpliment? Cha kukushahuri ni pm imei namba yako niwape watu wa cyber kituo cha kati waifatilie,ningekuwa dar ningeenda mwenye tcra.
 
mi ndo maana nimeweka avg antivirus hats nikiibiwa najua naweza kufuta data zangu na kulock kupitia email...yaani ni nzuri hata ukibadili line wanakutumia email kukujulisha line imebadilishwa kwenye simu yako

Mkuu hiyo app ni nzuri sana ila inafanya udukuzi kwenye simu yako, inafanya kazi ambazo sizo zilizokufanya uidownload. Kazi zenyewe wala hazijaorodheshwa.
Hiyo app ina;
1. Soma msg zako
2. soma email zako
3. Pia inajua idadi ya app ulizonazo kwenye simu yako.
 

Kweli Mkuu mie niliweka hile ya avast kwenye HTC one yangu na simu niliibiwa mpaka Leo sijaipata na HTC zilivokuwa hadimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…