alma gemela
JF-Expert Member
- Feb 22, 2013
- 842
- 280
Usimpeleke special school, atalemaa kaisaaa na kuwa na uwezomdogo hivo hivo. Itamfanya ajikubali which is not right.
Huyo mpe mavitamin yale ya aloevera, lishe bora, mtafutuie shule nzuri ambayo darasani wako wachache na personal tutor awe anamkazia mafunzo akirudi home. Akikaa na normal kids na kuwa challanged anaweza kurecover mpaka ukashangaaaa!
Mungu akutie nguvu usichoke kumkazania.
Fuata ushauri wa wadau hapo juu bila kusahau na wewe mwenyewe ujitahidi kumsimamia mtoto usitegemee waalimu peke yake. Pia umfundishapo mtoto kamwe usimwambie wewe ni slow learner bali mtreat kama wakawaida tu ili asije akajiona kweli yeye ana tatizo hilo na pengine kubweteka.
Nakumbuka niliwahi kumpeleka last born wangu shule flani nikaambiwa mtoto wangu ni slow learner kiukweli sikukubaliana nao. Nilichogundua ile shule ilikua na tatizo ktk kumfundisha mtoto anaeanza kujifunza. Niliamua kumhamisha mtoto na kumpeleka shule tofauti kule alikua mtoto mzuri na alifanya vizuri mno na mpaka sasa anafanya vizuri sana kama watoto wengine.
Tatizo pia hana kumbukumbu
Inawezekana hamumpi mazoezi ya kutosha. Weka utaratibu kila siku jioni awe na muda wa one hour kureview somo la jana yake. Pia angalia vipindi vya tv anavyotizama. Viwe educative na creative. Fanya kujifunza kuwe funny. Mfano ongea nae kuhusu topic, umuhimu na relevance yake.
Tatizo pia hana kumbukumbu
Mmmh inawezekana na wewe umejenga hisia kuwa mwanao ana tatizo na hapo ndipo penye shida. Kumbuka unapewa kwa kadiri unavyoamini , jiulize je kwenu kuna wa hivyo yaani kuna watu wasio na kumbukumbu au maslow learner. Binafsi huwa huwa sikubali anya negative thought juu ya mtoto au juu yangu mwenyewe.Tatizo pia hana kumbukumbu