Slaa: Mgombea sahihi katika wakati mbovu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa: Mgombea sahihi katika wakati mbovu.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zawadi Ngoda, Sep 14, 2010.

 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Kama kura za uraisi zingekuwa zinapigwa kupitia mtandaoni na kujumuisha wapenda mtandao tu, na hasa kama JF ndio ingekuwa ni kituo pekee cha upigaji kura, basi Slaa angeshinda kwa kishindo. Hilo lingewezekana kama tu tungefikiria kuwa idadi ya wapiga kura wote Tanzania hawazidi elfu 10.

  Lakini hiyo ni ndoto tu kwani hali halisi ni nyingine kabisa katika viwanja vya mpira kule Ulyankuru, Sekenke na maeneo mengine yafananayo na hayo Tanzania. Kiujumla tamko sahihi ni kwamba, Kikwete ni mzito sana kwa Slaa. Slaa angegombea wakati wa Mkapa ungekuwa wakati Muafaka, lakini safari hii kajiua kisiasa au pengine kakiua chama kizima kisiasa. Lau kama angesubiri mpaka 2015 angeweza kuambulia chochote, lakini kushindwa kwake mwaka huu kutamshushia hadhi yake hata 2015 kama ilivyokuwa kwa Mrema 1995 na kulamba dume 2000.

  Kuna sababu tatu kuu zitazomuangusha Slaa; Kikwete kamaliza matatizo ya kimsingi ya Mtanzania ikiwa pamoja na usalama wa Raia na mali zake. Pili matatizo ya ujambazi yaliyokuwa yanawakera watanzania tokea Boko mpaka wasafiri wa mabasi mikoani ameyaondoa kabisa. Tatu kaondoa tofauti za wananchi kivyama au kaviunganisha vyama kwa kuelewa kuwa mpinzani wako si adui yako bali ni rafiki yako unayoweza kukaanaye na mkala sahani moja. Kuchaguliwa kwa akina Kabwe kushiriki katika kamati ya madini ni moja ya miujiza aliyoifanya Kikwete. Hata akisafiri haishi kuwachukua wapinzani katika misafara yake huko Ughaibuni. Sijakueleza maswala ya Muafaka alivyoyapeleka mpaka kafika kituoni BILA HATA VIONGOZI WA WAPINZANI KUTIWA NDANI. Kifupi hakuna mpinzani aliyetiwa ndani mwaka huu. Uhuru wa kusema ndio sikwambii, hata akina zawadi Ngoda eti leo wanaandika bila woga wowote ule.

  Hayo na mengine mengi, yamefanya hata uchaguzi wa mwaka huu kutokuwa na mfuto sana, kwa kila mtanzania anajua kuwa katika nafasi ya uraisi Slaa ni msindikizaji tu. WanaCHADEMA wote wanafahamu kuwa hapo wamepoteza kiti cha Ubunge, na hii itawagharimu sana CHADEMA SIKU ZIJAZO.

  Panga pangua, Slaa hawezi kushinda kwa vile zaidi ya kujiita Dr hana sifa kama zile za Kikwete. Kikwete kashika nafasi nyingi serikalini na jeshini, je Slaa ana nini la kutuambia. Kutosoma alama za nyakati ndiko kulikompotosha Slaa au CHADEMA kwa ujumla. Washauri wake hawakumchagulia wakati muafaka kwake kugombea uraisi. Pengine wamemtosa kistile. Mkaidi hafaidi mpaka siku ya IDD, lakini je siku ya Idd kwa Slaa imefika? Hilo ni swali ambalo kila mwana CHADEMA ajiuliza.
   
 2. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  :lalala: there we go thread number 234,567,982,000 of lame attempts to sell a defective product...
  Mi nasuiri hapa Quinine na Mwafrika nirudi kucheka... ila mkuu kusema uongo kama huu haufai maana si kwenye mtandao hata huko barabarani (si mjini hata vijijini) watu wanaongea kuhusu mgombea wenu na wameshampachika majina kama vile Dr Ahadi, Vasco Da Gama etc.
  Propaganda hizi zote wala hazitu-affect in positive or negative way.. leaves us bored.. ila endelea tu kumnadi ni haki yako but thread hii itakufa mapema tu kama yale mengine ya propaganda...

  Jamani Mwafrika, Quinine tunaomba zile picha zinazoambatana na maelezo kama haya :smile-big:
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Sep 14, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Zawadi Ngoda,
  Pengine wewe hujui Siasa zaidi ya kusomma hiki kijiwe cha JF. Unaandika mengi kwa fikra zako kuliko kuwa na utafiti wa kutosha halafu pia huna takwimu zinazoweza kuhakikisha maneno yako. Zaidi ya yote haya inaonyesha hofuy yako kuingia kwa Dr.Slaa ktk Uchaguzi huu kwa sababu hali iliyopo leo kisiasa haijawahi kutokea hata ule wakati wa Mrema haikufikia wananchi kuwa na mwanga mkubwa kiasi hiki.

  Labda nikuulize wewe unayejua zaidi, Je, Chadema wangekuwa ktk hali gani kama Dr. Slaa asingegombea?
   
 4. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  Huu ni ushabiki! Kikwete huwezi linganisha na Mkapa hata siku moja! Achana na vitu vidogo kama mambo ya vibaka na siasa senu za uzandiki! Taja vitu hata kimoja tu alichofanya Kikwete miaka 5 iliyopita. Mkapa kajenga uwanja, barabara, ali control mfumuko wa bei na uchumi ulikuwa stable, japo aliiba sana na kuuza nchi Nashangaa leo anatuambia tukatae utumwa wa Wamagharibi

  Huyu msanii wako tuichoambulia ni smile, katembea mpaka Hollywood, katembeza bakuli kazi hataki kufanya, mfumuko wa bei kila kitu kiko juu! Kiwango cha ufaulu kimeshuka na hiyo migofu yenu ya shule za kata. Hivi ulishaona wapi umemkamata mwizi unamwambia rudisha tu halafu uondoke! Mwizi? tena wa mabilion! Sheria iko wapi? Mafisadi yanajinafasi mitaani! Kwa ufupi kama lipo hata moja la kusifia ningefanya hivyo!
   
 5. s

  suley Member

  #5
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Let's put aside the enemity for awhile and walk our walk as tanzanian, as society of common good.,as civilised and responsible citizens...,kikwete kafanya hili halina ubishi.,sio propaganda..,hakuna changa la macho katika vitu ambavyo vipo tunakanyaga na tunaviona kwa macho yetu..,bahati mbaya tumesimamia makosa machache na kusahau wema mwingi tuliotendewa.,kwa haya yaliyobaki tushirikiane nae tuyakamilisha badala ya kuyabeza ilihali tunajuwa kuwa ni ya msingi na yanaleta na yataleta tija katika taifa hili...!
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Yapi mbona hujayataja tuya digest?
   
 7. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2010
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haha Slaa fixi tu, nilimsikia jana ati akichaguliwa ataleta high speed train, Mwanza-Dar in 3 hours... Msanii tu
   
 8. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Mwaka huu hakukuwa cha Mbowe, Slaa wala Silaha ambaye angeisetiri CHADEMA. Pengine kidogo huyo Kabwe kwa ukijana wake (sio sera) angevutia vijana ambao ni wengi miongoni mwa wapiga kura. Hata hivyo angepata labda 20% ya kura zote.

  Mwaka huu ni hatari, nyie jiliwazeni tu katika huu mtandao!!
   
 9. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Vibaka? Ha ha hhha. Waulize Jamaica, jeshi walipambana na kibak zaidi ya siku kumi, zaidi ya watu 200 waliuawa. Sikwambii huko Latin Amerika.

  Watanzania mtakusoma na kupindukia bila kujua matatizo ya msingi yanayowasumbua. Kweli nyie badooooooo!
   
 10. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Kwani unafikiri uongo?? Tayari ishakuwa coordinated, nyie mnaishi kwenye ujima!!
   
 11. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2010
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haha basi kama tayari si tuwape credit serikali zilizopita ikiwemo hii ya JK, Slaa atamalizia tu au?
   
 12. m

  mfundishi Member

  #12
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 27, 2008
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wazo lako linakosa mtiririko, lau kwa para moja ungeweza kutudokeza kuwa kwa nini Dr Slaa ni mgombea sahihi (heading inavyo someka) baadala ya kukimbilia kufikiri kuwa atapoteza.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Sep 14, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sasa hapa ndipo unapoonyesha rangi zako na kuuficha ukweli wote ulofikiria umeandika..Hakuna mtu anayejilaza isipokuwa kila anayeandika hapa anakuja na mawazo ambayo anaweza kuya back up na data au utafiti alofanya, sii mahala pa kuandika pumba ukafikiria Ushabiki zaidi. Au hayo majini ya Sheikh Yahya ndio umeona mtandao tosha maanake watu kama nyie hamkosi kuamini majini ndio yanalinda usalama wa wananchi.

  Kisha kwako wewe Upinzani ni makosa...yaani unachotaka wewe JK asimame peke yake pasipo kupingwa kama mnavyogawana madaraka ndani ya chama, lakini Watanzania hawajalala kama unavyofikiria. Kisha sifa unazompamba hata Zitto haziingi akilini yaani watu wamchague Zitto kwa sababu ni kijana?.. ama kweli wanaCCM bado mko dunia ya Ujima, endeleeni kutumia mawe..
   
 14. K

  Keil JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkandara,

  Naona huelewi unajadiliana na nani, usiumize kichwa chako wala kupoteza nguvu kujadiliana na huyu rafiki. Soon atakupeleka kwenye hoja ambazo kila siku huwa unapingana nazo. Huyu rafiki mwelekeo wake ni kule kwa akina Rev. Masanilo na Mwafrika.
   
 15. S

  Sylver Senior Member

  #15
  Sep 14, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Propaganda zako ziko very low ndugu.
  Unashindwa kututea unachongea ,una bwabwaja tu ,can you come with evidence/data to back up what you're saying.
  Inaonekana unapapara kuandika unachotaka kuandika inakufanya ghafla usema utumbo
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Inaonyesha uko tayari kwa lolote kutoka kwa jK, hizi sifa si bure hahaha aha ahah !!!!
   
 17. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,501
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  ninautupilia mbali ujinga na upuuzi wako tena ninarudia ninautupilia mbali upupu wako maana hauna msingi
   
 18. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160

  Join Date Tue Aug 2010, thanked by Zawadi Ngoda!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! vyote vijakazi vya mabwana zao
   
 19. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  mi nilifikiri ukiandika kwa kiswahili kidogo unaweza kujenga hoja.....maana thread zako za kingereza huwa nikisoma nasikia kichefuchefu kwa zile "direct translation" sasa nimeelewa tatizo sio lugha ni akili tu hapa!:becky:
   
 20. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Sina shaka kuwa aliyeanzisha thread hii ni kada aliyekunywa maji ya bendera ya kijani na njano
   
Loading...