Mzito Kabwela
Platinum Member
- Nov 28, 2009
- 18,908
- 7,751
Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kuwa Dokta Slaa ameanza kampeni kabla ya Muda.
Ni kinyume cha sheria maana kila anapopita anaeleza atakayowafanyia Watanzania pindi akichaguliwa kuwa Rais. Kwakuwa lengo la Mwanasiasa huyo ni kuomba ridhaa ya kudhaminiwa hakupaswa kuanza kutoa ahadi za yale atakayoyafanya maana kwa kufanya hivyo ni kuanza kampeni.
?
Source: Habari leoMCHAKATO wa Chadema kupata wadhamini kwa ajili ya mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano, umeelezwa kukiuka utaratibu na kuonekana kuanza kampeni kabla ya wakati.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa nchini, wamesema wanashindwa kutofautisha mchakato wa udhamini na kampeni za chama kutokana na jinsi mgombea huyo, Dk. Wilbrod Slaa na viongozi wenzake, wanavyozunguka nchini na kufanya mikutano ya hadhara.
"Tunashindwa kuelewa kinachofanyika hasa ni nini kati ya kutafuta wadhamini na kufanya kampeni, mikutano mingi ya hadhara huku na huko badala ya kutafuta wadhamini matawini," alisema mchambuzi wa masuala ya siasa ambaye hakutaka kutajwa gazetini.
Dk. Slaa amezunguka sehemu mbalimbali nchini akitumia helikopta kutafuta wadhamini huku akifanya mikutano ya hadhara ambayo amekuwa akiihutubia sambamba na Mwenyekiti Freeman Mbowe, Mwanasheria Mabere Marando na viongozi wengine.
Akizungumzia mchakato huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Rajab Kiravu, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haina uwezo wa kuwazuia Chadema kufanya wanavyofanya sasa kwa kuwa hawajachukua fomu ya kugombea urais.
"Hatuwezi kuwabana hawa kwa sababu taarifa tuliyonayo ni kwamba wanatafuta wadhamini na si kampeni, kwa sababu kampeni hazijaanza," alisema Kiravu.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, alisema naye anashangaa kuona Chadema inafanya kana kwamba kampeni zimeanza.
"Nami nashangaa na nimekuwa nikimtafuta Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kuhusu hili lakini sijampata … naona sasa nchi ina kambare wengi, kwa sababu kuna tabia ya kutoheshimu sheria za nchi," alisema Werema.
Aliongeza kuwa hata ustaarabu wa kawaida tu nao haupo kwani Chadema walipaswa kujua kuwa wanachokifanya sicho, kwa sababu udhamini hautafutwi kwa kufanya mikutano ya hadhara na kutoa ahadi na kuomba kura.
Alimshangaa Marando ambaye alisema ni mwanasheria aliyebobea ambaye asingetarajiwa kusema anayoyasema sasa katika mikutano ya Chadema, ikiwamo kuahidi kutoa siri zilizo katika nyaraka za kesi zilizoko mahakamani.
Pia alisema kwa mtu ambaye anakiri alikuwa Idara ya Usalama wa Taifa, asingetarajia kumsikia akitamba kuwa ana mambo mengi ya siri anayoyajua na muda ukifika atayaweka hadharani.
"Ni hayo hayo ninayoyasema kwamba sasa kambare wamekuwa wengi nchini … lakini namsubiri ayaseme tu hayo jukwaani, kwa sababu Sheria ya Usalama wa Taifa iko wazi kabisa," alisema Werema.
Katika hotuba nyingi za Dk. Slaa, amekuwa akibeza utawala wa Rais Jakaya Kikwete akisema umeshindwa kuwasaidia wananchi na pia amekuwa akiomba kura za wafanyakazi akisema Kikwete alizikataa hivyo apewe yeye.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na NEC, kampeni zinatarajiwa kuanza rasmi Agosti 20 mwaka huu.
Ndio maana yakeHuyu werema ni mwanachama wa CCM, au ni mwanasheria wa serikali? Au anaogopa Dr Slaa akipata urais kitumbua kitaota mchanga?
MzittokabwelaTaarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kuwa Dokta Slaa ameanza kampeni kabla ya Muda.
Akizungumzia mchakato huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Rajab Kiravu, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haina uwezo wa kuwazuia Chadema kufanya wanavyofanya sasa kwa kuwa hawajachukua fomu ya kugombea urais.
"Hatuwezi kuwabana hawa kwa sababu taarifa tuliyonayo ni kwamba wanatafuta wadhamini na si kampeni, kwa sababu kampeni hazijaanza," alisema Kiravu.
Mzittokabwela
Taarifa yako ni ya uongo umeitoa wapi, NEC hawakusema hivyo, hata hivyo umejuaje Dr.Slaa atachaguliwa kugombea wakati hata fomu za NEC hajachukua.
Mzittokabwela NEC (Kiravu) imesema hivi.....
Nashanga wewe unatuletea habari tofauti kabisa plainly opposite na NEC walivyosema, usije ikawa unachanganya Halmashauri kuu ya CCM nayo huitwa NEC-CCM.
CCM walipokuwa wanawatambulisha wagombea wao ikwepo pale pale jangwani walidhani wengine hawawezi.....mkuki kwa nguruwe..... ukiona hivyo ni kiwewe kimewaingia.
Mzitto amekosea tu padogo, hajadanganya!Gazeti la Habari LeoMCHAKATO wa Chadema kupata wadhamini kwa ajili ya mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano, umeelezwa kukiuka utaratibu na kuonekana kuanza kampeni kabla ya wakati.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa nchini, wamesema wanashindwa kutofautisha mchakato wa udhamini na kampeni za chama kutokana na jinsi mgombea huyo, Dk. Wilbrod Slaa na viongozi wenzake, wanavyozunguka nchini na kufanya mikutano ya hadhara.
"Tunashindwa kuelewa kinachofanyika hasa ni nini kati ya kutafuta wadhamini na kufanya kampeni, mikutano mingi ya hadhara huku na huko badala ya kutafuta wadhamini matawini," alisema mchambuzi wa masuala ya siasa ambaye hakutaka kutajwa gazetini.
Dk. Slaa amezunguka sehemu mbalimbali nchini akitumia helikopta kutafuta wadhamini huku akifanya mikutano ya hadhara ambayo amekuwa akiihutubia sambamba na Mwenyekiti Freeman Mbowe, Mwanasheria Mabere Marando na viongozi wengine.
Akizungumzia mchakato huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Rajab Kiravu, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haina uwezo wa kuwazuia Chadema kufanya wanavyofanya sasa kwa kuwa hawajachukua fomu ya kugombea urais.
"Hatuwezi kuwabana hawa kwa sababu taarifa tuliyonayo ni kwamba wanatafuta wadhamini na si kampeni, kwa sababu kampeni hazijaanza," alisema Kiravu.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, alisema naye anashangaa kuona Chadema inafanya kana kwamba kampeni zimeanza.
"Nami nashangaa na nimekuwa nikimtafuta Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kuhusu hili lakini sijampata … naona sasa nchi ina kambare wengi, kwa sababu kuna tabia ya kutoheshimu sheria za nchi," alisema Werema.
Aliongeza kuwa hata ustaarabu wa kawaida tu nao haupo kwani Chadema walipaswa kujua kuwa wanachokifanya sicho, kwa sababu udhamini hautafutwi kwa kufanya mikutano ya hadhara na kutoa ahadi na kuomba kura.
Alimshangaa Marando ambaye alisema ni mwanasheria aliyebobea ambaye asingetarajiwa kusema anayoyasema sasa katika mikutano ya Chadema, ikiwamo kuahidi kutoa siri zilizo katika nyaraka za kesi zilizoko mahakamani.
Pia alisema kwa mtu ambaye anakiri alikuwa Idara ya Usalama wa Taifa, asingetarajia kumsikia akitamba kuwa ana mambo mengi ya siri anayoyajua na muda ukifika atayaweka hadharani.
"Ni hayo hayo ninayoyasema kwamba sasa kambare wamekuwa wengi nchini … lakini namsubiri ayaseme tu hayo jukwaani, kwa sababu Sheria ya Usalama wa Taifa iko wazi kabisa," alisema Werema.
Katika hotuba nyingi za Dk. Slaa, amekuwa akibeza utawala wa Rais Jakaya Kikwete akisema umeshindwa kuwasaidia wananchi na pia amekuwa akiomba kura za wafanyakazi akisema Kikwete alizikataa hivyo apewe yeye.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na NEC, kampeni zinatarajiwa kuanza rasmi Agosti 20 mwaka huu.
zito wa chadema, kashakuwa mpinzani wa slaa. duh bora zito atimke tu

Hilo utakuwa umelisema wewe au umetumwa na mwenzako Tambwe Hizzazito wa chadema, kashakuwa mpinzani wa slaa. duh bora zito atimke tu
ni kitambo sasa tangu nimejiunga na hii forum kama memba, sijawahi ona mwanajamvi kilaza kama MS, yaaaani haelewi hata kusoma na kutafsiri mambo mepesi kama haya, kweli JF inapita kwenye wakati mgumu kama great thinkers wenyewe ndio kama huyu MS, kifupi huyu ndio mwanajamvi mwenzetu mwenye matatizo zaidi kifikra.zito wa chadema, kashakuwa mpinzani wa slaa. duh bora zito atimke tu
Ni muumini mzuri wa siasa majitakani kitambo sasa tangu nimejiunga na hii forum kama memba, sijawahi ona mwanajamvi kilaza kama MS, yaaaani haelewi hata kusoma na kutafsiri mambo mepesi kama haya, kweli JF inapita kwenye wakati mgumu kama great thinkers wenyewe ndio kama huyu MS, kifupi huyu ndio mwanajamvi mwenzetu mwenye matatizo zaidi kifikra.