Napata taabu kuelewa naomba msaada wenu, kuuliza si ujinga wakuu.
Hivi Slaa (Dr.) anaamini juu ya sera na itikadi gani? Maana alipokuwa CDM aliwasasha moto mkubwa kwa CCM, tena moto mkubwa haswaaaa. Aligombea Urais 2010 kupitia CDM hii ikimanisha haikuikubali CCM, Sera zake na itikadi yake, pia au hakumkubali JK.
Kwa vile 2015 alijiondoka chamani ilionesha pia hakumkubali EL, ni ni kweli alimtaja sana kama fisadi mkubwa na mtu asiyefaa.
Sasa yuko CCM alipo JK na EL kwa pamoja, pia kwenye sera na itikaidi ileile, contradiction!!!! am getting confused yaani CCM Enzi zile za 2005, 2010 hadi 2015 October alikuwa anapigania nini? na sasa anapigania nini?
Alihama CDM kwa vile EL aliingia CDM, yaani muda wote anapambana akiwa upinzani alipambana juu ya mtu? sio sera na itikadi? ila Slaa huyo huyo hahami CCM kwa EL kurejea CCM, nini kinamshikiria huko ambacho kilikosekana wakati EL anahamia CDM ili kumshikilia?
Namweshimu kwanza kama Padri pia mtu ambaye alichagiza mabadiliko ya sera kwa sura ya dhati, je heshima hii ni bubble balloon? Is he fake in out? why or why not? huyu jamaa anaamini nini kuhusu soasa za TZ?
Je huyu jamaa Slaa anawakilisha wanasiasa wengi TZ ama ni special case? Tunawaambia nini vijana wadogo wambao walishawishika na sera zake ambazo sasa nashindwa kuelewa ni aina ipi? ama ni chuki na watu ama mtu wala sio sera? au ni mapenzi na mtu wala sio sera na itikadi?
Nawasilisha, I just want to have insights of what this man is in terms of political understanding and his stand.
Alijisaliti mwenyewe kwa upumbavu wake.
K ile ina elements za utamu usio wa kawa! Ila hapa hajajisaliti hata tone. The mwanzo justified that mwisho .... ramani ilikolezwa na mdau mwingine kujiunga na CHADEMA. Sio ishu ya mafahali mbili boma moja. Wala! Ilibidi ramani ibadilishwe kwa kuhamisha kete. Wadanganywa mpo?
(From a certified cuckoo's head)
Kuhusu ufisadi na mafisadi msimamo wangu bado ule ule sishirikiani nao, Slaa alituambia Lowassa ni fisadi nikamwamini leo mwenzetu anakunywa naye mvinyo, mimi niko nje ya tent nawatizama. Lol.
Kwa sasa anajilipizia kisasi tu kwa uhuni aliofanyiwa.
Mbachao imepita na msala umepita.
Wewe Dr slaa yuko scandinavia kule anakula bata balaa si unaona amekua kijana kule anasimamia nchi kama tisa hivi yani fulu kusafiri na kujionea ma vivutio dizanini kama yuko vacation amestaafu kwa ufahari kuliko angebaki ufipa pale ofisi kama ka stoo na fastration kibao. ACHA mzee wawatu afaidi uzee wake
Katibu mkuu wa Chama kikuu Cha Upinzani ni cheo kikubwa sana si kwa Tanzania tu bali nchi nyingi Duniani. Tena Dr Slaa alienda hadi kuua kuwa Mgombea Uraisi na kupata % si haba.
Sasa unapo kuja kuwa chini ya Waziri na usha wahi kuwa kiongozi wa kitaifa hii ni Demotion ila watu tunaweza ona kapanda ila hii ni kushuka thamani.
Ni sawa ja Marehemu Samweli Sita alivyo toka kuwa Spika wa Bunge na kwenda kuwa Waziri wa Africa Mashariki. Usipika ni Cheo kikubwa kabisa kabisa sasa tena kuja kuwa Waziri ni kujishusha kwa kiwango cha kutisha.
Mifano iko Mingi sana ila shida inabakia ni NJAAA hakuna uzalendo wala Mjomba wake na uzalendo ni NJAAA hata ningejuwa mimi ningeshuka tu kwa sababu ya NJAAA tu.
Ila Isingekuwa NJAA Dr Mihogo hakupaswa kuwa Balozi na kuja kuwajibika kwa Waziri
Kwa sasa anajilipizia kisasi tu kwa uhuni aliofanyiwa.
Mbachao imepita na msala umepita.
Dr. Slaa kashakula matapishi kwa kukubali appointment ya serikali ya CCM aliyoishutumu sana.
Ningemuona ngangali kama angekataa ubalozi.
Sasa kukataa kula matapishi kwa mtu mmoja halafu kula matapishi kwa mfumo mzima ni ujinga.
Na Slaa si mjinga.
Ina maana kuna zaidi ya matapishi hapa, kuna suala la maslahi.
I suspect it was never there to begin with.So the principle has moved to voice for opportunity not for the voiceless?