Slaa amgomea JK


ukosawa, tatizo letu hatyupendi kufikiri. Hakuna sehemu masikini tz. Uvivu ktk kufikiri na kutenda juu ya raslimali zetu bahari,maziwa, mito,ardhi yenye rutuba namenginer mengi vinatosha kutoaumasikini.jambo jingine muhimu ni uadilifu kwa tulio wapa mamlaka.
 

Hatamu hakuna tena, mjadala unarudi kwa wananchi, ieleweke hii ni katiba mpya. Hakuna mwenye haki ya kuhodhi mjadala, hata wabunge wa CCM wamekiona cha moto. Na bado, inawezekana ukarudi bungeni kwa marekebisho. Mwisho tunataka maoni ya wenye nchi (Umma) yaheshimiwe. Kwa upande mwingine tujitahidi kusoma historia iliyojificha, itatusaidia.
 
Heshima Mkuu!
Ninakubaliana na wewe na wengine wengi juu ya kile "Tunachokita", lakini kwa bahati mbaya, kilichopo ni kile "Tulichopewa". Naomba upitie thread ya Mwanakijiji ambapo inaonesha kuwa Watanzania tumepitishwa katika uchochoro usio na pa kutokea. Bado naamini kuwa tunaweza kubadilisha hili, sio kwa kushiriki japo kwa wingi katika kutoa maoni kwani maoni yetu yanaweza kuwekwa upande na kutumikia matakwa ya CCM, bali kuupinga mchakato huu hivi sasa katika Mahakama ya Katiba kabla haijafikia hiyo hatua ya katiba kupitishwa.
 

Ni sisi sote kuhamasisha watanzania umuhimu wa zoezi hili. Kila mahala tutakapokuko kuamsha mazungumzo kuhusu umuhimu wa kujiandaa kutoa maoni katika hii tume. Kwa sasa tusubiri kidogo ili tuone mwenendo wa tume kabla ya kwenda mahakamani. Kwa sababu tunajadili katiba ya muungano na si ya tanganyika, wamejiweka wenyewe katika mtego.
 

Pia utawala wa kimajimbo unasaidia kupata Rais mzuri wa nchi kama wanavyofanya wamarekani,ambapo wanaowania Urais wamekuwa masenetor ktk majimbo yao hivyo sheria ikitengenezwa hivy tutakuwa na reference nzuri ktk kuleta maendeleo ktk majimbo yao.

Pia serikali za majimbo zinasaidia kuepuka iwapo kiongozi aliopo madarakani si mtendaji mzuri au msimamizi mzuri wa shughuli za serikali au fedha hivyo udhaifu huo unakuwa hauenei nchi nzima.

Pia kuna masuala ya kushughulia masuala ya matatizo ya kijamii,serikali za majimbo inatatua harka zaidi kuliko ilivyo kama uendeshaji unaoendelea hivi sasa
 

Hizi akili huwa tunazipata wapi ngd zanguni..Mbona tunakuwa wagumu wa kufikir.
Leo hii viwanda vinatengeneza ndege ila haziachi kuzitengeneza kwa kuwa kuna nyingine zinaanguka na kuuwa watu..Suala la kutengeneza na kuanguka ni vitu viwili tofauti ila vinavyoshabiana kiamtukio na linalobaki kuwa ni changamoto kwa kila kimoja.
Tukibaki kusema tukifanya hivi mbona kule yanatokea hivi huo utakuwa ni ufinyu wa AKILI tena si kidogo.....

Ndg Kobelo nadhani unaufaham udhaifu wa mfumo tuliona sisi na ubora wa mfumo wa majimbo......

Leo hii Kenya katiba yao ni wa mfumo wa majimbo,tutazidi kutanguliwa na Wakenya kwa kila jambo kwa kuwa na vichwa vingi vibovu serikalini vinavyofikiri kidogo kama samaki kama anavyopinga KOBELLO
 
I said the same thing but in a different way.

Huwezi kusema unataka kupata katiba mpya ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania bila kuuzungumzia muungano.

Hiyo siyo katiba ya wananchi.

Hapo mtanisamehe.
 
Mi hata sioni hiyo faida ya kuungana, kama kweli tuna jeshi kwanini kaeneo kama Zanzibar katuzingue? Si tujitenge nao tu halafu kila upande uchukue 50 zake? Maana hakuna kwenye Muungano anayefaidika, kila upande unalalamika tu... Hii ni sawa na wanandoa ambao hawaelewani wala hawana mahusiano ya kindoa lakini bado wameng'ang'ana kukaa nyumba moja. Si ajabu ipo siku mmoja atamchoma hata kisu mwenziwe! Sababu zinazotolewa kuhalalisha Muungano ni za kihuni, eti tuna-undugu wa damu, eti tumechanganyikana, n.k. Hivi huo undugu wa damu upo kati ya Tanganyika na Zanzibar tu? Hivi hakuna Wamasai wa Tz na Kenya? Hakuna Wajaluo Mara na Kenya? Hakuna Wamakonde Mtwara na Msumbiji? Hivi Tz imepakana na nchi ngapi, huko watu wetu hawajaoa na kuolewa? Sasa wote hao si ndugu zetu wa damu? Mbona hatuongelei kuungana na nchi zote zilizotuzunguka kama kweli tunaamini ktk Muungano? Sasa nakubaliana na yule Meya wa Dsm aliyesema baadhi yetu tunafikiri kwa kutumia makalio!
Bado tuna wasomi na wengine wakijiita Wataalamu wa Katiba! Shit! Sasa kama wapo hao na huku tangu Muungano uasisiwe kumekuwa na kero chungu nzima, huku fedha za walipa kodi zikiteketea kwa UFISADI wa kuzitatua kero hizo, na wengine wakijidai kuwa kuna mambo mengi yameongezwa ambayo hayakuwa ya Muungano, mbona Wanasheria wetu wasidai hazi hizo kupitia Mahakama za Kikatiba au hata za Kimataifa kuliko kuendelea kulaumu tu humu? Hivi ni nani aliyeziona hizo nakala za HATI NA MKATABA WA MUUNGANO? Watz wangapi walishaziona? Sasa iweje kutupotezea muda na rasilimali kujadili NADHARIA ambayo nina uhakika hata hao Wazanzibari wenyewe wanaisikia tu midomoni mwa watu? Si Mwanasheria wao Mkuu ndiye aliyesema hakuwahi kuziona hizo HATI? Sasa Mpemba wa kawaida anayevua samaki mwambao wa bahari ndiye anayelalamika utafikiri alikuwepo au alikuwa Mgeni rasmi wakati wa utiaji saini wa Mikataba hiyo feki?
THIS IS AMAZING. Hebu Mungu Atujalie ili ktk nafasi hii finyu tusipoteze muda kujadili upuuzi kama huu wakati Mtz wa kawaida hana uhakika wa hata mlo wa siku halafu Mwanasiasa aliyeshiba kwa fedha za EPA akimtaka ajadili Muungano!! Hivi ni kipi kilianza, KUKU (kwa maana ya Mtanzania) ama YAI (kwa maana ya Muungano wa watu wawili waliovalia suti huku wakipulizwa na upepo wa Magogoni?)
 
Kuvunjika kwa muungano kutasababishwa na kutukuuzungumzia katika hili zoezi. Ubishi mwingine wa kishabiki hausaidii. Kwanza ikumbukwe muungano haukuwa na referendum bali ulikuwa wa viongozi wa juu. Huu ni wakati muafaka kuurekebisha.

Kumbukeni
Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania, John Malecela na Katibu Mkuu wa CCM, Harace Kolimba wakajiondoa bila ya wao kutaka ili kuinusuru nchi.
Katika pendekezo la kugeuza mfumo wa Muungano wa Serikali mbili na kuundwa kwa mfumo wa Shirikisho la Serikali Tatu, CCM kwa wakati huo ilikataa mfumo huo kwa hoja dhaifu sana.
Hata hivyo, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha azimio la kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Jamhuri ya Muungano baada ya kundi la wabunge 55 kutoka majimbo ya Tanzania Bara kuwasilisha hoja binafsi Bungeni na kukubaliwa.
Kimsingi Bunge lilipitisha kwa kauli moja, Agosti 1993 Azimio la kutaka Serikali ya Tanzania kupelekwa muswada wa sheria kubadili Katiba ya Jamhuri ya Muungano ili kuwa na Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano.
 
Katiba yoyote duniani huwa na misingi mikuu. Katika nchi ya
kidemokrasia msingi mkuu wa Katiba ni ule unaoweka mamlaka
yote mikononi mwa wananchi. Misingi mingine ni:-
(a) Katiba ni lazima iwezeshe wananchi kuridhiana kitaifa
(b) Ushiriki wa wananchi ni lazima uwe wa kutosheleza ili
kuwezesha umiliki wa wananchi wa Katiba husika
(c) Katiba huwa ni ya kipekee kutokana na historia ya nchi husika
(d) Katiba yeyote hairuhusu ubaguzi wa aina yeyote miongoni
mwa raia wake
(e) Katiba lazima itoe maono ya mbele ya taifa husika
(f) Katiba ni sheria mama katika nchi ambapo hakuna sheria
inayotungwa itaruhusiwa kukinzana nayo.

Soma zaidi hapa:
http://www.policyforum-tz.org/files/MwongozowaKatibakwaRaia.pdf
 
Tume inaanza kazi lini, maana tuna mengi sana ya kuchangia. Jf ina nafasi gani katika hili.
 
"Muungano ni kama koti joto likizidi unalivua" Ni kawaida kwa binadamu wenye akili timamu kila linapotokea tatizo la kutokuelewana katika jamii au baina ya watu wawili njia pekee ya kuleta maelewano baina yao ni kukaa chini na kulizungumza tatizo lao kwa maana ya kutaka kulipatia ufumbuzi na shuluhisho la kudumu ili katika siku za baadae lisitokee tena. Kwetu sisi tuna tatizo Wazanzibari wanasema kwa uwazi kabisa kuwa kuna kasoro katika muungano wetu japo Watanganyika tuliowengi hatusemi kwa nguvu kama wenzetu wa Zanzibar lakini kasoro zipo na tunaziona.Kwa kulitambua hilo ndio maana hata serikali ya JMT imeunda idara maalum chini ya ofisi ya makamu wa rais ili kushughulikia kero za muungano. Sasa kama tunatambua kuwa zipo kero kwani zisijadiliwe na wananchi ambao ndio wenye muungano?
 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano haiwezi kushughulikia matatizo ya muungano kwa niaba ya watanganyika. Sasa ni wakati wa kushughulikia matatizo ya muungano, bila kufumba macho. Sina maana ya kuvunja muungano. Ni kama mtu ukiwa katika ndoa, halafu kukatokea hitilafu, basi pande zote mbili zinawajibika kutafuta suluhu. Kungekuwa na serikali tatu mengi yasingetokea.
 
Mwisho wa malalamiko ni kuwa na Serikali tatu,

Wananchi waamasishwe kuwepo kwa serikali ya tatu

a. Serikali ndogo ya Muungano yenye makao makuu Dar es Salaam

b. Serikali ya Tanganyika yenye makao makuu yake Dodoma

c. Serikali ya watu wa zanzibar yenye makao makuu unguja (kama sasa)
 

Tena hii itatoa mwanya wa nchi nyingine kuingia katika muungano. Huu wa sasa ni kizungumkuti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…