Slaa alitetea JWTZ mabomu ya Gongo la Mboto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa alitetea JWTZ mabomu ya Gongo la Mboto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Feb 26, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Dk Slaa amesema kulipuka kwa mabomu hayo kumetokana na Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete kupuuza ombi la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuwapa fedha kwa ajili ya kuteketeza mabomu yaliyokwisha muda wake.

  Amesema kazi ya jeshi ni kulinda uhai wa watu wake nchini, lakini kupitia jeshi taifa limeweza kupoteza watu zaidi ya 40 kutokana na serikali kugoma kutoa fedha hizo ambazo ziliombwa na JWTZ.

  "Tunataka Kikwete atueleze kwa kina kama ni kweli, maana tunaambiwa kabla ya mabomu kulipuka mwaka 2009 JWTZ (Mbagala) waliomba fedha kwa ajili ya kuteketeza mabomu, lakini kutokana na serikali kutothamini maisha ya watu wake ilikataa kuwa hakuna fedha.

  "Tunaambiwa tena kuwa kabla ya mabomu haya ya mwisho(Gongo la Mboto) kulipuka wanajeshi waliomba fedha serikalini kwa ajili ya kuteketeza mabomu hayo, lakini pia serikali hiyohiyo haikutoa kwa madai kuwa hakuna fedha," alieleza Dk. Slaa.

  Kwa sababu hiyo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi anawajibika moja kwa moja ajiuzulu.

  Source: Mwananchi.
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  tunajuaje kama haya mabomu ni ya mwisho kulipuka.....si walisema yale ya Mbagala yalikuwa ya mwisho na haitatokea tena?.....sasa tutakua na imani gani na serikali?.....wao watufahamishe ni wapi next yatalipuka ili watu waweze kujipanga......maana hata hiyo dalili ya serikali kutoa pesa haipo........sijui hatma ya nchi inaelekea wapi
   
Loading...