Slaa alipua kombora jingine

Basi na huyu babu aje na jipya, kila kukicha ni nyimbo hiyo hiyo? Hana jipya nini?
 
ccm mnakazi kweli kurudisha imani kwa wananchi, dr tupe na za kuinua uchumi ni makampuni gani yarikwapua hizo pesa, maana muuza sura alijitamba tumetenga trilion 1 kwa ajiri ya mtikisiko wa uchumi na makampuni yalioadhirika yalikuwa mengi ya pamba na watu wakaanzisha makampuni feki hapo hapo kupitisha hizo fedha, dr slaaa wa ukweli tupe majina
 
Dr. Slaa, kaa chin jipange upya. Njoo kivingine

Akae chini kabla mechi haijaisha? Nani anaweza kucheza badala yake! Ni yeye pekee yake mwenye uwezo wa kumkabili JK na kundi la wahuni wenzake. Slaa akinyamaza kimya Tz itauzwa kwa bei ya jumla kwa majambazi wanaoitwa wawekezaji. Tumtue moyo aendelee kumpiga la mgambo kwa niamba ya Wtz wote.
 
JK naye ni mwizi sasa anaanzaje kuwashugulikia wezi wenzie..yaani 2015 nina vitu vingi sana vya kuangalia kabla ya kupiga kura....naangalia kuanzia sura,jina .,dini ,GPA mpaka rais ana watoto wangapi....bila hivo sipigi kura mimi
 
Mibongo bana!

Yani badala ya kuhakiisha watuhumiwa wa ufisadi wanafikishwa makahakani kujibu tuhuma za uhujumu uchumi, badala ake eti mnapigiana kampeni kuwa ni nani atahakikisha analinda maslahi ya wastaafu mafisadi na kuwaacha wapunzike, huo ndo utaratibu wenu wabongo! Si mllimamwini JK? kuwa atawasghulikia mafisadi.


Acheni ujinga ndugu zangu wa ndoto za alinacha, EPA IMWINGIZE JK na CCM madarakani halafu mseme ataifuatilia, hii mambo ya banana republic noma!
 
Ni Wakati wetu watanzania kuweka maslahi yetu binafsi pembeni na kuunga mkono kwa ujasiri juhudi hizi za kudai haki zetu...tunalipa kodi kila siku kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu,ila inasikitisha sana kuwa baadhi yetu wanatufanya tu wajinga kiasi cha kuona hatutaweza kusimama dhidi ya wizi wa namna hii.
 
Hivi tulitafuta uhuru kumuondoa mkoloni mweupe na kumkabidhi mkoloni mweusi ambaye hana huruma kwa watu wake na nchi yake? Ni yale yale alioandika Jaramogi Oginga Odinga Not yet Uhuru.Ila hakuna marefu yasio na ncha.Kujilimbikiza mali za dhuruma sio ujanja ni ujinga.Slaa ametoa wake up call,lakini sikio la kufa halisikii dawa.
 
Huyu nae kesha choooka maana ukiona mtu anatupa makombora kila kuchapo bila ya kombora kulipuka na kuleta tija basi jua mtu huyo hajasomea vizuri namna ya kulipoa kombora!

Namshauri huyu padre apumzike tu kwa sasa na kazi hizi awaachie vijana kama zito, mbowe,mnyika nk...

umekosa la kuandika.
 
Back
Top Bottom