Slaa alipua kombora jingine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa alipua kombora jingine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 9, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Mwandishi wetu - Tanzania Daima

  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbord Slaa, amelipua kombora jingine kwa kuziweka hadharani kampuni zilizoshindwa kurejesha fedha za madeni ya malipo ya nje (EPA) kwa kile alichokiita kukingiwa kifua na vigogo wa serikali.

  Hatua ya Dk. Slaa imekuja ikiwa ni siku mbili tu tangu alipomshukia Rais Jakaya Kikwete akimsakama kwa kushindwa kuwashughulikia watuhumiwa wa ufisadi na kutatua matatizo ya kiuchumi ambayo yameiyumbisha nchi.


  Akizungumza na Tanzania Daima jana, Dk. Slaa alisema kuwa pamoja na kauli za ukali zilizotolewa na Rais Kikwete muda mrefu uliopita, akiwataka waliokwapua fedha za EPA kuzirejesha kwa hiyari yao wenyewe na kutishia kuwachukulia hatua za kisheria, hadi sasa ni kampuni nane tu kati ya 21 zilizorejesha fedha hizo.  Alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa Rais Kikwete amekaa kimya bila kuchukua hatua wala kusema chochote dhidi ya kampuni zilizodharau agizo lake na kwamba inaonyesha ni jinsi gani serikali na CCM imeelemewa na ufisadi na imeshindwa kuchukua hatua kwa kuwa ufisadi umejikita katika mfumo mzima unaowagusa pia viongozi waandamizi katika chama na serikali.  Alionya kuwa kwa kuwa serikali imeshindwa kutekeleza wajibu huo, namna pekee ya kusimamia uwajibikaji ni kwa kuunganisha nguvu za wananchi katika kutetea rasilimali za taifa.  Slaa alitaja kampuni zilizorejesha fedha hizo na kiasi katika mabano kuwa ni Bencon International Ltd iliyorejesha sh bilioni 7.96 kati ya bilioni 10.56 ilizokwapua; Njake Hotels and Tours & Njake Enterprises Ltd iliyorejesha fedha zote sh bilioni 2.225; na Ndovu Soap sh bilioni 1.548 ambazo ni kiasi chote ilichokuwa imekichukua.  Nyingine zilizorejesha fedha zote zilizokuwa zimechotwa ni pamoja na Kagoda Agriculture, (bilioni 34.781), VB & Associated (bilioni 9.227), VB Holdings Ltd (bilioni 5.148), Venus Hotels & Apartments Ltd (bilioni 4.050) na Bora Hotels & Apartments Ltd (bilioni 5.779).


  Hata hivyo, alizitaja kampuni 13 ambazo zimegoma kurejesha fedha hizo (majina tunayo) na kwamba hazijalipa jumla ya fedha zote zinazokisiwa kufikia sh bilioni 50.


  Dk. Slaa alidai kuwa CHADEMA ilitarajia kwamba mwaka 2011 ulikuwa wa kukamilisha uchunguzi na uchukuaji wa hatua dhidi ya wahusika katika kashfa mbalimbali ili kurejesha utamaduni wa uwajibikaji. Badala yake serikali imeendelea kuahirisha kuchukua hatua kamili serikalini, bungeni na hata ndani ya chama chenyewe.


  Aliongeza kuwa katika hali ya kusikitisha Rais Kikwete katika hotuba yake kwa taifa ya Disemba 31, 2011 hakuzungumzia hatua ambazo serikali yake imefikia katika kushughulikia mafisadi.


  Juzi akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na hotuba ya Rais Kikwete ya kufunga mwaka, Dk. Slaa alidai kuwa hali ya uchumi inazidi kudorora na serikali haionyeshi mikakati yoyote ya kulinusuru taifa.  Alisema kuwa badala yake, Rais Kikwete amekuwa akitoa majibu yanaisukumia lawama hali mbaya ya uchumi ya kidunia, wakati angeweza kufanya jitihada za kuondokana na hali hiyo, na hasa kuwachukulia hatua watu wote wanaotuhumiwa kuhujumu mali ya taifa.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Huyu anafaa kuwa rais ana uchungu wa nchi...
   
 3. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kiongozi hodari huwa hachoki kupigania haki za wanyonge.Hongera Dr. Kwa kutufungua macho wadanganyika
   
 4. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hatutafunga fail mpaka kieleweke
   
 5. v

  vangilichuma Member

  #5
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hatahivyo wanainchi waelimike maisha yamekuwa siyo kira kitu sasa juu 2015 chagueni chadema chadema hoooyeee
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  kikwete hawawezi wezi waliomuweka madarakani.....hawezi kuwafanya lolote.

  Nazi yake ubwabwa.
   
 7. Mmasi

  Mmasi Senior Member

  #7
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Labda ila ataakipewa nchi ataweza?
   
 8. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  lini tuzidai mkuu? tunahitaji mwongozo tu
   
 9. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Eee Mungu fanya lolote kwa ajil ya taifa la TZ, tuepushe na huu uongozi wa Kikwete! Mapenz yako yatimizwe juu ya serikal yake nzima.
  Mpe nguvu na afya njema Baba ye2 na rais anaestahil kuiongoza nchi na s kuitawala Tz, Dkt SLAA! Shusha adhabu juu ya viongoz wote wala rushwa na wale wasio tenda haki. Eee Mungu ikumbuke Tz, kwan kwako tunakuja kwa ku2bu na kwa kunyenyekea. Kwa Jina lako takatifu naomba,.. wote tuseme!
  Amen.....!
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ​ndo nini sasa kutaja zilizorejesha pesa na kutotaja ambazo hazijarejesha peasa?????arrrrrrggggggggghhhhh
   
 11. U

  UMMATI Member

  #11
  Jan 9, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  piga keleleeeee! sema chadema, chadema, chadema, chadema, chadema, chadema, chadema, chadema, chadema,
   
 12. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kikwete hawezi kukamata m2 ye mwenyewe kichwa ***i ya bagamoyo
   
 13. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Jamani Dr Slaa alianza kuyasema Bungeni hakurupukiiiii>>>>>> Kikwete kaa chonjo Saa ni mbaya hii..Watanzania tumechoka na Mibunge inatafuna mifwedha ya Nchi upo kimya,,Wanyama wameporwa upo kimya, Dhahabu Zinapelekwa nje upo kimya, Na hii mifisadi unaiangalia tuu kwani mifedha yote hii imakaliwa na watu kwa mifuko yao..utayajutia haya siku ya siku..
   
 14. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu nae kesha choooka maana ukiona mtu anatupa makombora kila kuchapo bila ya kombora kulipuka na kuleta tija basi jua mtu huyo hajasomea vizuri namna ya kulipoa kombora!

  Namshauri huyu padre apumzike tu kwa sasa na kazi hizi awaachie vijana kama zito, mbowe,mnyika nk...
   
 15. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Ngongo, Ritz na FF bado hawajacomment......???
   
 16. m

  mdoe mchaina Senior Member

  #16
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo ndie DR slaaaaaa Bana .hakuna kuzungumzia oooh sijui fulani kafukuzwa chama anaongelea vitu vyenye mashiko na umuhimu juu ya mustakabali wa Nchi yetu .hongera mzee
   
 17. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 734
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Dr. Slaa, kaa chin jipange upya. Njoo kivingine
   
 18. mzee wa miba

  mzee wa miba JF-Expert Member

  #18
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 763
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Najuta kukichagua Chama Tawala,kila mtu hata watoto wadogo ongea nao wanachukia uamuzi wa watanzania walio wengi kukipa kura 2010,2015 bado ni mbali sana lakini hata wao hawastuki.Kila kukicha oooh mara wanajivua gamba,oooh mara wanawalazimisha wapiga kura wapige mbizi,mwingine huku Rombo yeye kipindi fulani alitulazimisha tule majani fasta tulimtungua,muulizeni lakini hata sijui kesi yake iko wapi.
   
 19. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kama waliochoka wanatakiwa wawaachie vijana, huyu anayelalamikiwa kwa kushindwa kuwachukulia hatua wezi unampa ujumbe gani?
   
 20. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ziko wapi?
   
Loading...