Slaa adharirishwa Kigoma Kaskazini jioni hii. Akimbia mkutano

Status
Not open for further replies.
Nyie akina Taswira inaonesha mlikaa na akina Raia Watanzania ila mkashindwa kukubaliana nani apost. Hii inadhihirishwa na mlichokiandika kutokuwa na source lakini post zote zinafanana.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu,
Taarifa za uhakika kutoka kwa katibu wa JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI CHADEMA ndugu RAMA RUAHA, ni kwamba Katibu mkuu wa CHADEMA Padri SLAA leo alikuwa afanye mikutano miwili katika vijiji viwili baada ya kukimbia NGOME KUU YA ZZK ''MWANDIGA'' na kukimbilia kuweka mikutano ifanyike kijiji cha NYARUBANDA na mwingine KIDAHWE.

Taarifa kamili ni kama ifuatavyo

(i). MKUTANO WA NYARUBANDA. - Itabidi PADRI SLAA aishukuru mvua iliyowatawanyisha wananchi wenye HASIRA walioanza kumshambulia SLAA kwa mabango, maneno makali na mawe, huku vijana wake wa REDBRIGED wakionyesha kuishiwa nguvu na kuomba msaada wa POLISI.

SLAA anayejidai kichwa ngumu leo ameishukuru mvua hiyo iliyositiri AIBU YAKE YA KARNE YA KUPOPOLEWA NA MAYAI VIZA NA MAWE.

(ii). MKUTANO WA KIDAHWE - Katika Hali ile ile ya WAHA WA KIGOMA kumchukia DOKTA SLAA kwa kuwafanya wendawazimu na kuwataka washerehekee MAZISHI YA KIJANA WAO, huku SLAA ILIMBIDI AINGIE MITINI.

NDIO, SLAA AMESHINDWA KUTOKEA MKUTANONI KIDAHWE BAADA YA KUAMBIWA KUWA WANANCHI WA ENEO HILO WANA HASIRA NA CHUKI KUBWA DHIDI YAKE, VIONGOZI WA CHADEMA KIDAHWE WALIKATAA HATA KUMUWEKEA MEZA YA KUSIMAMA KUHUTUBIA, GARI LA M4C LILILOONGOZANA NA VIBARAKA WAKE LILIAMBULIA MATUSI MAKUBWA NA MAWE MFULULIZO KISHA KUPEWA TAHADHARI KUWA MLETENI SLAA AONE CHA MTEMA KUNI.

KWA KIFUPI KABISA SLAA AMEUMBUKA KWA KUSHINDWA KUHUTUBIA JIMBONI KWA ZITTO KABWE,

WENYEWE WANASEMA ''slaa hawezi kutuulia mwanetu halafu anakuja kutuimbia NGOMA za kikweo tucheze, sisi sio wapuuzi''

namuomba MOLEMO, BEN SAA NANE, TUMAINI MAKENE, WAITARA NA WENGINEO WOTE WAJE HAPA KUBISHA AMA KUTHIBITISHA TOFAUTI''

Msafara wa Gwiji wa siasa Tanzania na Katibu mkuu CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa ndo unakatiza hapa Kigoma mjini, ishara ya vidole viwili inatanda kila mahali na maneno ya ''Dkt. Slaa huyo huyo...Chademaaaa....Chademaaaa''.

Msafara unaelekea Jimbo la Kigoma Kaskazini Mkutano wa Kwanza utakuwa Nyarubanga, kisha utaelekea mkutano wa pili.

Updates.....

Ndo twawasili Nyarubanga hapa. Akina mama wamejipanga barabarani pembeni kdg ya uwanja wanaimba kumpokea Katibu Mkuu Dkt. Slaa. Msafara umeshaingia uwanjani.

Red Brigade wako imara kweli kweli leo hapa. Wananchi wanasogea sogea. Naona ngoma hapa inachezwa na akina mama.

Updates No 2:

Dkt. Slaa anaingia kucheza ngoma na wenyeji hapa. Ngoma hii inachezwa na kikundi cha ngoma cha akina mama wa CHADEMA kuhamasisha wananchi kujiunga na CHADEMA hasa akina mama na vijana.

Naambiwa inaitwa Denga. Wananchi wanashangilia kumuona Dokta anaungana na akina mama kucheza Denga!

Updates No 3.....

Mkutano umeshafunguliwa na Mkiti Issa Kibaba. Waitara amemkaribisha Mratibu wa Kanda ambaye amezungumzia namna Kanda inavyojipanga kuhudumia wanachama na wananchi kwa ujumla.

Sasa anapanda Mkiti wa Kanda Shaaban Mambo, anazungumza kidogo kwa sbb ya dalili ya mvua kubwa. Sasa amepanda Dkt. Slaa.

Mvua imekuwa kubwa hapa. Wav wamevumilia kumsikiliza Dkt, ambaye ameamua kubadili kubadili mbinu ya mkutano badala ya kuendelea kuhutubia, anatoa nafasi ya maswali kwa wananchi ili wasiende mbali

Updates No 4.....

Watu 4 hadi sasa wameshauliza maswali na Dkt. Slaa anaendelea kujibu maswali yote 5, 3 yanayuhusu maamuzi ya Kamati Kuu kuwavua madaraka Zitto, Kitila na Mwigamba

Mengine 2 yanayuhusu Chadema na misingi yake. Dkt, anaendelea kufafanua, masuala yote yaliyoulizwa.

Mvua inazidi kuwa kubwa hapa. Dkt. Slaa anawauliza wananchi aendelee au afunge mkutano, wananchi wanasema aendelee. Anaendelea hapa.

Mvua kubwa iliyotanguliwa na ukungu mkubwa sana ktk eneo la mkutano imezidi kuongezeka.

Sehemu ya umati wa wananchi wametafuta miamvuli na kubaki karibu na jukwaa. Wengine wako jukwaa kuu, wengine wamekimbilia upenuni mwa nyumba kuendelea kusikiliza.

Mvua ktk eneo hili la mkutano ni kubwa sana, ingawa mbali kdg tu kutoka hapa hakuna ukungu wala mvua.

Updates No 5....

Kutokana na mvua kuzidi kuwa kubwa Wananchi wamemruhusu Dkt. Slaa ashuke jukwaani baada ya kuhutubia kama dkk 45.

Msafara unalazimika kuondoka kwenda mkutano wa pili.

Kuna utani unazungumzwa na baadhi ya wananchi kwamba ''wameshindwa njia zote sasa wameamua kujaribu hii...''.

Lakini Dkt. Slaa kabla hajaondoka jukwaani, aliwaambia wananchi kuwa mvua ni baraka, hivyo wasilaumu!

Picha chini ni kabla mvua haijaanza kunyesha:
attachment.php

Source: Afisa Habari Mkuu CHADEMA Tumaini Makene

CC: Taswira

Mods huu ni ukweli kutoka Kigoma. Thread ya Raia Watanzania haina ukweli naombeni muwatendee haki members
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha haa a a a....aisee... misukule imeanza kutiririka kama imechomolewa vichwa..
 
Kuna watu kama huyu ni sawa na futuhi ama zekomedi kwaajili ya kuburudisha GT wa jf,

Dr Alex kazi aliyopewa na akina Zitto na ccm ya kuratibu vurugu imemsgunda
 
Kajifunze kiswahili fasaha kwanza ndo uje,au ukafundishwe mwandiko-kudharirishwa ndo nini? Au msamiati mpya?
 
Back
Top Bottom