SKONGA na USWAZI vinakujenga je? On EATV

Mmasi

Senior Member
Oct 26, 2011
164
15
Kwa kweli mi sioni umuhimu wa hivi vipindi labda wakuu mnifumbue.....!
 
Binafsi sioni kama kuna tatizo. Hivi ni vipindi vya kuburudisha, na kuna watu wanavifurahia sana. Unajua kwenye swala la burudani kila mtu ana hisia zake, kitu ambacho wewe unaona hakina mvuto kwako kuna mwingine kinamburudisha sana. Kwa mfano kuna mwingine hapendi sigara au pombe lakini kuna mwingine ana bajeti maalum kwa ajili ya vitu hivi.Na ni vigumu kumbadilisha kwa sababu burudani yake ndiyo anaipata huko.

Mkuu kwani wewe hujaona mtu badala ya kuangalia taarifa ya habari anaweka maigizo au muziki? Au hujajiuliza ni kwanini mtu analipia DSTV kwa gharama kubwa, unadhani anailipia kwa sababu ya kuangalia channels za vikatuni, wengi wao (kama sio wote) ni kwa sababu ya mpira tena football. Kwa mtu ambaye si mpenzi wa football lazima atamwona huyu jamaa kama mtu asiyejua matumizi ya hela. Hii yote ni kwa sababu ya interest. Kiukweli tunatofautiana sana katika hisia na mambo yanayohusu burudani.

Lakini pia ukumbuke ile ni TV ya kibiashara, wanajaribu kubuni vipindi ambavyo vinawavuta watazamaji wengi ili wapate wadau wengi wataojitaganzia kwao. Siamini kama wanajua kwamba vipindi ulivyotaja havina mvuto kwa jamii, wangeishaviondoa. Waandaaji wa vipindi vya redio na tv wako makini sana linapokuja swala la kubuni vipindi.

Mimi naamini dhima ya vyombo hivi, pamoja na kutuhabarisha lakini pia vinatuburudisha, so vipindi vingine usitegemee kujifunza kitu, vianakuwa vya burudani tu. Mbona hujahoji vipindi vya katuni au musiki, kwani vyenyewe vinatufundisha nini?
 
huwa siangalii hivo vipindi,labda bahati mbaya..lakn nadhani vinaonyesha hali halisi ya maisha ya huko uswazi ili watu wasije dhani kuishi mjini ni fulll shangwe magorofa na huduma nzuri kila mahali.
 
bora uswaz kinaonyesha maisha halisi ya uswahilini lakin sconga hasa pale wanafunzi wanapokata viuno kinanikera sana, wabaki hukohuko dar huku mikoani wasije kutuharibia watoto
 
kipindi cha skonga kizuri japo si mfuatiliaji. Kinaonyesha ni jinsi gani wanafunzi wasivyo makini na elimu ya darasani lakini makini kwenye soka, muziki na mitindo, sio kwa kushiriki bali kuwa na taarifa za kutosha kuhusu mambo hayo. Hii inaleta picha kuwa mitaala inaweza badilishwa kuendana na mahaba ya wanafunzi juu ya mambo wayapendayo
 
Binafsi sioni kama kuna tatizo. Hivi ni vipindi vya kuburudisha, na kuna watu wanavifurahia sana. Unajua kwenye swala la burudani kila mtu ana hisia zake, kitu ambacho wewe unaona hakina mvuto kwako kuna mwingine kinamburudisha sana. Kwa mfano kuna mwingine hapendi sigara au pombe lakini kuna mwingine ana bajeti maalum kwa ajili ya vitu hivi.Na ni vigumu kumbadilisha kwa sababu burudani yake ndiyo anaipata huko.

Mkuu kwani wewe hujaona mtu badala ya kuangalia taarifa ya habari anaweka maigizo au muziki? Au hujajiuliza ni kwanini mtu analipia DSTV kwa gharama kubwa, unadhani anailipia kwa sababu ya kuangalia channels za vikatuni, wengi wao (kama sio wote) ni kwa sababu ya mpira tena football. Kwa mtu ambaye si mpenzi wa football lazima atamwona huyu jamaa kama mtu asiyejua matumizi ya hela. Hii yote ni kwa sababu ya interest. Kiukweli tunatofautiana sana katika hisia na mambo yanayohusu burudani.

Lakini pia ukumbuke ile ni TV ya kibiashara, wanajaribu kubuni vipindi ambavyo vinawavuta watazamaji wengi ili wapate wadau wengi wataojitaganzia kwao. Siamini kama wanajua kwamba vipindi ulivyotaja havina mvuto kwa jamii, wangeishaviondoa. Waandaaji wa vipindi vya redio na tv wako makini sana linapokuja swala la kubuni vipindi.

Mimi naamini dhima ya vyombo hivi, pamoja na kutuhabarisha lakini pia vinatuburudisha, so vipindi vingine usitegemee kujifunza kitu, vianakuwa vya burudani tu. Mbona hujahoji vipindi vya katuni au musiki, kwani vyenyewe vinatufundisha nini?

Kwa mfano kipindi hiki kinachokaribia mwanzo wa mwaka shule nyingi zinarusha matangazo kupitia skonga na wao wanaingiza hela kwa jambo ambalo unaona halina maana
 
huwa siangalii hivo vipindi,labda bahati mbaya..lakn nadhani vinaonyesha hali halisi ya maisha ya huko uswazi ili watu wasije dhani kuishi mjini ni fulll shangwe magorofa na huduma nzuri kila mahali.

Kweli kabisa mkuu kama hiki cha uswazi watu tunaona matukio na vitu tofauti ambavyo tulijua havipo kumbe vipo
 
bora uswaz kinaonyesha maisha halisi ya uswahilini lakin sconga hasa pale wanafunzi wanapokata viuno kinanikera sana, wabaki hukohuko dar huku mikoani wasije kutuharibia watoto

Hapo si wanakuonyesha ukweli wa mambo kwa wanafunzi walio mashuleni wanachofanya?
 
Uwepo wa kitu fulani kina umuhim kwa baadhi ya watu na kama kwako hakina umuhimu kutakuwa na kingine chenye umuhim
 
Back
Top Bottom