BUNGE ni Taasisi yenye heshima kubwa ndani na nje ya Nchi. Heshima ya Bunge inatokana na umuhimu wa kazi yake kwa maslahi ya nchi na wananchi.
Kazi za Bunge kupitia kamati zake mbalimbali zina manufaa makubwa kwa Taifa. Mathalani, Kamati ya Hesabu za Serikali ya Bunge ina kazi muhimu ya kuhakikisha kuwa hesabu za serikali zinakuwa bayana na sahihi.
Kwa kufanya kazi zake kwa uadilifu na uzalendo, Kamati za Bunge zina nafasi muhimu ya kuisukuma na kuiwajibisha serikali kwa manufaa ya Umma. Kwa kiasi fulani, hatusiti kusema kuwa Kamati hizo zinajitahidi kutimiza wajibu wao.
Hata hivyo, tunalazimika kuikosoa hadharani Kamati ya Hesabu za Serikali ya Bunge kwa namna ilivyoandaa na kuwasilisha ripoti yake ya Fedha za Akaunti ya Escrow.
Taifa lilishitushwa na taarifa ya Kamati hiyo kuwa fedha nyingi za nchi zimechotwa kinyume na taratibu. Kamati imetaja majina ya watu na hata mazingira ya wizi ikiwa ni pamoja na maboksi, viroba na masandarusi yaliyotumika kubebea fedha hizo!
Mjadala ukawa mzito ambapo ndani ya Bunge na nje yake, moto wa hasira uliwaka kwelikweli. Ni ujasiri wa hali ya juu uliohitajika kutuliza hasira hizo kwa
maneno tofauti na yale ya Kamati.
Ilikuwa kana kwamba kila mtu alitakiwa kuamini bila kuhoji. Aliyehoji au kutoa maoni tofauti akaonekana kama mchawi na labda ni sehemu ya watu waliopata mgao.
Ndani ya Bunge, ujasiri wa mawaziri kama Hawa Ghasia, Celina Kombani na Angellah Karuki pamoja na Wabunge kama Asumta Mshama na Job Lusinde na waziri mahiri Simbachawene wa kukataa uongo ulionekana kama kero tu ambayo Taifa halikutakiwa kuisikia. Mawaziri hawa wanwake na Wabunge hawa wanabaki kama wapiganaji waliojitoa muhanga kuhakikisha kuwa ukweli unachukua nafasi masikioni na machoni mwa wananchi.
Pale mwanzo, ujasiri huo ulionekana kwa wachache ambao ilionekana kama vile wangeshindwa na wengi walioamini kila kilichoandikwa na kusemwa na Kamati hiyo ya Bunge!
Ni kweli, PAC ilivuna imani ya wananchi wengi. Lakini, kadiri muda ulivyokwenda hasa baada ya ripoti kukabidhiwa kwa Rais,na serikali kufanya uamuzi wa kuichunguza upya kadhia nzima ya Escrow,kiwango cha imani ya watu juu ya Ripoti ya Kamati kimeonekana kupungua.
Hatua ya Rais kuteua CAG mpya yaweza kuhesabika kama msingi wa kujenga mazingira ya kupata ukweli juu ya hesabu zilizoleta utatanishi. Kila mtu sasa akatulia kusubiri CAG mpya angesema nini.
Yumkini wengi waliamini kuwa majibu ya CAG yangewaweka pagumu wale waliotuhumiwa. Lakini Ripoti ya CAG,baada ya uhakiki, imewalowesha wale
ambao awali waliamini Ripoti ya PAC!
Kusawajika huko kunatokana na masahihisho ya hesabu zilizowasilishwa na Kamati. Mgongano wa kimahesabu kati ya dola milioni 306.6 zilizodaiwa na PAC kuwemo katika Akaunti ya Escrow na dola milioni 182.7 ambazo CAG anasema ndizo zilizokuwemo kwenye Akaunti hiyo umewashangaza wengi!
Taifa linamwamini CAG kwa asilimia 100 kwamba ndiye chombo cha kuweza kutoa taarifa sahihi. Na hata PAC inategemea taarifa za CAG. Swali linaweza kuulizwa, ni nani aliyesababisha mgongano wa mahesabu kwa kughushi na kukikuza kiasi cha fedha kinyume na taarifa ya CAG?
Na aliyefanya hivyo alikusudia nini? Na alifanya kwa maslahi ya nani? Je, huu sio mchezo mchafu wa kuchezea hesabu za serikali kwa malengo yaliyojificha yakiwemo ya kimasilahi, kisiasa na kibiashara?
Kwa kuwasilisha hesabu ambazo CAG anasema si sahihi, maana yake PAC imelidanganya Bunge na Taifa kwa ujumla! Kwa kuwa uongo huu umeleta usumbufu na umegharimu heshima za watu, pamoja na kulishulishushia heshima Tiafa mbele ya jumuiya ya kimataifa kuwa la wala rushwa na wafuja pesa, sisi tunapendekeza kuwa Bunge likutane kwa dharura ili PAC iliombe radhi Taifa kwa uongo huo.
Zaidi ya hivyo, kwa kuwa imepoteza imani ya watu juu ya umakini na uadilifu wake, PAC haina sababu ya kubaki na uongozi uliopo hivi sasa. Bunge linahitaji kujisafisha kwa kuivunja PAC na kuiunda upya.
Ni muhimu kuivunja PAC na kuipatia uongozi mpya kwani, kwa sura ya sasa haitaaminika tena masikioni na machoni mwa wananchi. Sio tu viongozi wake wa sasa hawapaswi kuwepo madarakani bali wana kila sababu ya kukabiliwa na jinai ya kuwapotosha Wananchi na kuhatarisha usalama wa Taifa.

Mjadala ukawa mzito ambapo ndani ya Bunge na nje yake, moto wa hasira uliwaka kwelikweli. Ni ujasiri wa hali ya juu uliohitajika kutuliza hasira hizo kwa maneno tofauti na yale ya Kamati.

Ndani ya Bunge, ujasiri wa mawaziri kama Hawa Ghasia, Celina Kombani na Angellah Karuki pamoja na Wabunge kama Asumta Mshama na Job Lusinde wa kukataa uongo ulionekana kama kero tu ambayo Taifa halikutakiwa kuisikia.
Mawaziri hawa wanwake na Wabunge hawa wanabaki kama wapiganaji waliojitoa muhanga kuhakikisha kuwa ukweli unachukua nafasi masikioni na machoni mwa wananchi.

Ni kweli, PAC ilivuna imani ya wananchi wengi. Lakini, kadiri muda ulivyokwenda hasa baada ya ripoti kukabidhiwa kwa Rais, na serikali kufanya uamuzi wa kuichunguza upya kadhia nzima ya Escrow, kiwango cha imani ya watu juu ya Ripoti ya Kamati kimeonekana kupungua.

Yumkini wengi waliamini kuwa majibu ya CAG yangewaweka pagumu wale waliotuhumiwa. Lakini Ripoti ya CAG, baada ya uhakiki, imewalowesha wale ambao awali waliamini Ripoti ya PAC! Kusawajika huko kunatokana na masahihisho ya hesabu zilizowasilishwa na Kamati.
Mgongano wa kimahesabu kati ya dola bilioni 306.6 zilizodaiwa na PAC kuwemo katika Akaunti ya Escrow na dola bilioni 182.7 ambazo CAG anasema ndizo zilizokuwemo kwenye Akaunti hiyo umewashangaza wengi!

Kwa kuwasilisha hesabu ambazo CAG anasema si sahihi, maana yake PAC imelidanganya Bunge na Taifa kwa ujumla!
Kwa kuwa uongo huu umeleta usumbufu na umegharimu heshima za watu, pamoja na kulishulishushia heshima Tiafa mbele ya jumuiya ya kimataifa kuwa la wala rushwa na wafuja pesa, sisi tunapendekeza kuwa Bunge likutane kwa dharura ili PAC iliombe radhi Taifa kwa uongo huo.