Siyoi ashusha presha Arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siyoi ashusha presha Arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mujumba, Mar 26, 2012.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WIKI moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki, sasa mgombea wa ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Sioi Sumari anaelekea kushusha
  presha, kwani ameibuka na kujigamba kuwa na jeuri ya kushinda uchaguzi kwa zaidi ya asilimia 85.

  Amewahakikishia pia wananchi wa jimbo hilo kwamba atapambana kwa nguvu zote kutatua kero za maji na ardhi mara moja baada ya kuwa mbunge.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Usa River mgombea huyo aliweka wazi
  imani yake hiyo huku akiwaomba wananchi na viongozi wa dini kuombea amani siku hiyo.

  Alisema ana imani atapata ushindi mkubwa kutokana na maandalizi mazuri na sera zinazotekelezeka za CCM.

  Akifafanua sababu za kuamini kushinda katika uchaguzi huo, Sioi ambaye kitaaluma ni
  mwanasheria alisema, kwanza analijua vyema jimbo hilo pamoja na changamoto zinazolikabili.

  Alisema uamuzi wa kujitokeza na kugombea ndani ya CCM ulitokana na ukweli kwamba yeye
  kama Mtanzania alikuwa na haki ya Kikatiba na Kichama.

  Alisema changamoto zilizoko ndani ya jimbo hilo anao uhakika wa kuzitafutia ufumbuzi
  kupitia kwa marafiki zake waliopo ndani na nje ya nchi.

  Akitilia mkazo suala la tatizo la maji alisema kwamba mkazo mkubwa utakuwa ni uboreshaji
  wa huduma za maji, ajira kwa vijana na kuupatia ufumbuzi mgogoro wa ardhi unaowakabili
  wananchi ndani ya jimbo hilo.

  Alisema mpaka sasa baadhi ya matatizo ndani ya jimbo hilo yalishaanza kufanyiwa kazi
  kupitia Serikali Kuu, Mkoa na wilaya.

  Akifafanua kuhusu ajira kwa vijana, Sioi alisema kwa kushirikiana na serikali na wadau wa maendeleo ikiwemo sekta binafsi, atabuni mikakati itakayosaidia kuwapatia vijana ajira na kupunguza ukubwa wa tatizo kwa kutegemea rasilimali zilizopo ndani ya jimbo hilo.

  Kuhusu maji, mgombea huyo alisema kwa kutambua kwamba maji ndio kiini cha uhai,
  atalichukulia suala hilo umuhimu mkubwa, kwa kuhakikisha kila Kata na vijiji vinapata maji ya uhakika ili kuboresha na kustawisha maisha ya wananchi.
   
 2. JOB SEEKER

  JOB SEEKER Senior Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naona umeamua kumuweka wasira kwanye avatar yako !!!!!!
  baba yake ameshikilia jimbo akiwa naiburi waziri !!!!!!
  akashindwa kutatua kero hizo !!!!!!
  kutokana na akili yako haina na tofauti na masaburii!!!!!!!!!!!!!!!!
  unashinadwa kuelewa toa ***** aaaaaaaaaaaaaaaaaa
  WIKI moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki, sasa mgombea wa ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Sioi Sumari anaelekea kushusha
  presha, kwani ameibuka na kujigamba kuwa na jeuri ya kushinda uchaguzi kwa zaidi ya asilimia 85.

  Amewahakikishia pia wananchi wa jimbo hilo kwamba atapambana kwa nguvu zote kutatua kero za maji na ardhi mara moja baada ya kuwa mbunge.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Usa River mgombea huyo aliweka wazi
  imani yake hiyo huku akiwaomba wananchi na viongozi wa dini kuombea amani siku hiyo.

  Alisema ana imani atapata ushindi mkubwa kutokana na maandalizi mazuri na sera zinazotekelezeka za CCM.

  Akifafanua sababu za kuamini kushinda katika uchaguzi huo, Sioi ambaye kitaaluma ni
  mwanasheria alisema, kwanza analijua vyema jimbo hilo pamoja na changamoto zinazolikabili.

  Alisema uamuzi wa kujitokeza na kugombea ndani ya CCM ulitokana na ukweli kwamba yeye
  kama Mtanzania alikuwa na haki ya Kikatiba na Kichama.

  Alisema changamoto zilizoko ndani ya jimbo hilo anao uhakika wa kuzitafutia ufumbuzi
  kupitia kwa marafiki zake waliopo ndani na nje ya nchi.

  Akitilia mkazo suala la tatizo la maji alisema kwamba mkazo mkubwa utakuwa ni uboreshaji
  wa huduma za maji, ajira kwa vijana na kuupatia ufumbuzi mgogoro wa ardhi unaowakabili
  wananchi ndani ya jimbo hilo.

  Alisema mpaka sasa baadhi ya matatizo ndani ya jimbo hilo yalishaanza kufanyiwa kazi
  kupitia Serikali Kuu, Mkoa na wilaya.

  Akifafanua kuhusu ajira kwa vijana, Sioi alisema kwa kushirikiana na serikali na wadau wa maendeleo ikiwemo sekta binafsi, atabuni mikakati itakayosaidia kuwapatia vijana ajira na kupunguza ukubwa wa tatizo kwa kutegemea rasilimali zilizopo ndani ya jimbo hilo.

  Kuhusu maji, mgombea huyo alisema kwa kutambua kwamba maji ndio kiini cha uhai,
  atalichukulia suala hilo umuhimu mkubwa, kwa kuhakikisha kila Kata na vijiji vinapata maji ya uhakika ili kuboresha na kustawisha maisha ya wananchi.[/QUOTE]
   
 3. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Acha ashushe kwa sasa asubiri siku ya kutangazwa matokeo atakapopandisha hadi kufa
   
 4. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Asije akagoma tu kusaini maana hawachelewi mpaka Lowasa amwambie saini au asisaini!!!
   
 5. R-CHUGA

  R-CHUGA Member

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Maendeleo gani anataka kuleta kama waziri alishindwa kwani yeye ni nani? Anataka amsaidie lowwasa kuendeleza ufisadi wake.
   
Loading...