Siyo Siri CHADEMA Imepata Jeraha


Inategemea huyo chura anaangukia wapi aweza kuangukia pua.
 
CHADEMA wanafanya kazi kwa kuongozwa na hisia sana. Kwa nchi zilizoendelea hata kama mwanasiasa amethibitika anakihujumu chama, ila as long as ana impact ndani na nje ya chama, sometimes its normal to work with the devil!
Ushabiki mwingine unatia kinyaa!! Nyie ndo wale wanaowafumania wake zao na kuishia kulipwa fidia na mgoni. Kwa maana nyingine Mkeo anagegedwa halafu unahongwa wewe. Nyie watu wa pwani vip?
 
Hakuna hata mchubuko ni neema tu, ni sawa na kuchota maji baharini kikombe kimoja!!! CHADEMA inazidi kunawili masaliti yametoka.
 
Hawawezi kuendelea kupata hizo pesa maana JK anamaliza muda wake, wanaokuja hawawezi kuendelea kumpa pesa maana hawana deal naye.
 
katika hilo niwakumbushe tu hakuna cha maana zaidi usaliti uliofanywa na yule waliyekuwa wakidhani ni mmoja wao kwahiyo hakuna cha kuogopa zaidi ya kusonga mbele,msaliti ni msaliti tu siku zote na kama ataamua kuyatangaza ya chadema huko aliko au kule anakutumwaga basi itakuwa ni muendelezo wa yale aliyokuwa akiyafanya hata alipokuwa ndani ya chadema,hakuna jipya hapo..!!
 
akiba ipi kamanda, zaidi ya Halima mdee, tundu lisu na mnyika (ingawa zitto kawaacha kwa mbali)....kuna jembe gani limebaki chadema?? ni lema au sugu???!!!
 
Ukweli uko wazi, yawezekana jeraha lisionekane sasa hv but najua muda ukifika mtajua tu
 
Karibia viongozi wengi wa Cdm walikuwa CCM kwahio wanajua udhaifu wa Magamba.

Ni kweli ndio maana wanaipeleka puta ccm angalia na chadema wasipelekwe puta na ACT maana hali ilivyo vyama vya upinzani bada la ya kuwa marafiki sasa ni maadui
 
Alipoondoka Kafurila ndio CDM kikapata wabunge na Madiwani wengi. Na Ameondoka Msaliti Tumepata vitongoji na Wenyeviti wa Mtaa wengi. Cdm ni Dume.
Na bado tulieni dawa iwaingie mlifikili togwa hiyo mnajiuliza nakujijibu wenyewe teh teh teh huo ni moto wa gesi mtaisoma namba.
 
Umeongea kitu cha msingi sana lakini wale wanaomezeshwa cha kuongea na Mbowe hawatakuelewa unazungumzia nini
 

kwa ujumla wewe hujafanya tafakuri vizuri ujiulize hapa nani kaumbuka,

chadema waliwasimamisha na hatimae kuwafukuza uanachama viongozi wao watatu ambao ni kitila mkumbo proffesa na mkufunzi wa chuo kikuu cha daresalaam,samson mwigamba aliyekuwa kiongozi wa chama hicho mkoani arusha na aliyekuwa naibu katibu mkuu cdm taifa kwa tuhuma za kuunda mtandao wa usaliti ndani ya chadema.

nyaraka na ushahidi wa wazi uliwekwa hadharani na wawili kati ya hao walikiri isipokuwa aliyekuwa katibu mkuu naibu ndugu ZZk,hatimae waliokiri kufukuzwa ndani ya chama kwa usaliti huku zzk yeye akikimbilia mahakamanikuzuia chama kisimjadili uanachama wake.jambo ambalo lilimfanya kuwa mbunge wa mahakama.hadi hukumu ya shauri lake ilipotolewa wiki chache zilizopita.jambo lililopelekea zzk kutangaza rasmi kuachia ubunge wake ikiwa ni baada ya kauli ya mwanasheria wa cdm Tundu lissu kutoa tamko la chama kwamba zzk alikwisha jifukuzisha chamani tangu alipokiuka katiba ya cdm,kwa kukishitaki chama mahakamani.

wakati wote hayo yakijili kwa upande wa zzk,huku kina mwigamba,kitila na nyakarungu wakajiunga na chama kilichokuwa kikisubiri usajili cha ACT.lakini muda mfupi nako kukatifuka kwa kile kilichotajwa na aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho bwana limbu kama ni kuvamiwa na kuporwa madaraka na kina mkumbo jambo lililowapeleka mahakamani na kuamriwa kinyemela kwa sintofahamu na msajili wa vyama nchini,jambo ambalo bwana kadawi limbu analilaamikia hadi sasa na akiwa na shauri mahakamani.
mojawapo ya madai yake akiongea na vyombo vya habari na kunukuriwa na vyombo kadhaa vya habari nchini ni pamoja na akaunti ya ACT kuingiziwa fedha na vyanzo asivyovifahamu ikiwamo pamoja na vifaa kama magari nk.

imemchukua zzk siku nne tu kuteuliwa kuwa kiongozi mkuu wa ACT,cheo ambacho ni kipya katika medani ya siasa nchini mwetu.madaraka ya kiuongozi yaliyoainishwa kwa kiongozi mkuu ni pamoja na kushauri chama,msemaji mkuu wa chama na pia mteuzi wa moja kwa moja wa nyadhifa mbalimbali za kiuongozi ndani ya chama chake.

tafakuri
kama chadema walikuwa waongo ni kwa vp haya yametokea?
tena amemteua mama kwa kisingizio cha kuwaenzi kina mama,wakati kiuhalisia amemuweka pale kutomuweka mtu anayeweza kumletea pingamizi kwenye baadhi ya maamuzi na au anayeweza kukaa kimya pale atakapoona baadhi ya mienendo isiyokubalika ndani ya chama chake.
ile janja ya kutaja mali anazodai kuziweka na madeni tunahitaji kuliona na lile la fedha za nssf alizowaamuru kuilipa kampuni ya lekadutigite anayoimiliki pamoja na magari aliyopewa na nimrod mkono,pia atutajie zile alizowekewa na TISS kwenye akaunti za nje kama alivyowahi kutuhumiwa na cdm.

kwa hiyo hapa amewasaidia cdm kwenye macho ya jamii kuzielewa mbichi na mbivu kwa usaliti wake:juggle:
pia tunashangaa kitila mkumbo kuendelea kuhama na kuvuruga vyama vya upinzani huku akiwa ni mtumishi wa serikali bila serikali kuchukua hatua zozote,wakati watu kama kina baregu yaliwafanya wapoteze ajira zao toka vyuo hivyo hivyo vya serikali
 

chadema hii inayoifanya ccm hailali tena viongozi wakuu kinana na huyu mpuuzi nape wanazunguuka tanzania nzima,leochadema itishwe na mtu anaitwa zito au mvuta bangi mchafu afande sele!?hapana aisee,chadema inawaza kuitoa ccm madarakani ili watanzania wafaidi rasilimali za taifa lao.sio kumuwaza zito
 
Mimi pamoja na familia yangu pamoja na marafiki wangu watano tumechoma kadi za uachama wa chadema pamoja na nguo zao, chama gani cha ukabila na ukoo namna ile.
kutoka watu 12 ndani ya chadema ni pengo, huoni kwamba ni hasara?

Kila uchwao Chadema Ina Wanachama Wapya 20 Hivyo Ukitoka wewe sio Pengo tu! Hakuna Hata Mwanya mkuu Na Chadema Inazidi kuneemeka Napia nikama Unaamka Asubuh na Kufanya Usaf ndani Zile Takataka ndo nyinyi Wasaliti Tunaenda Kuwamwaga Jalalani.... Jalala nadhani unalijua nalenyewe likijaa zinahamishiwa Jalala Kuuu Hilo Pia Unalijua.
 

Na siku zote ukitumbua Jipu siku ya kwanza na yapili Tayari kidonda Kinapona. Hilo Jeraha la Jipu hata halitusumbui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…