Siyo maajabu, Sanitizer ya bacteria vs Virus Sanitizer

Siyo maajabu, Sanitizer ya bacteria vs Virus Sanitizer

Nashukuru mkuu kwa kuleta mada hii ambapo hat a mimi nimekua nikijiuliza maswali mengi sana, kuhusu hizi hatua tulizoshauriwa tuzichukue, Muda mrefu sana nimeuliza maswali mengi kuhusu matumizi ya sabuni na maji tiririka kwenye udhibiti wa Virus, lakini nimekua nukijibiwa kirahisi tu wewe nawa.

Lakini ukweli tukirudi hata kwenye biology ya form two, hatujawahi kufundishwa kuwa virusi wanaweza kuuwawa na sabuni isipokuwa bacteria, na ndo maana hata matangazo ya sabuni kama dettol yanasisitiza kuwa sabuni inasaidia kuuwa bacteria na si virus. Kwa uwelewa wangu wa hovyo hovyo ni kuwa bacteria wanauwawa kutokana na kiasi fulani cha joto na ndo maana vifaa vinavyotumiwa kwa magonjwa ya virus ushauri ni kuvichemsha na sio kuviosha na sabuni au maji tiririka.

Naomba kama humu ndani kuna manguli wa mambo ya korona na virusi watusaidie kwenye hili kitaalamu ili na sisi mabush doctor tupate uelewa wa hili.
1588843187939.png

Ulichokijifunza hiyo form two hata 4 au six ni kitu mbacho ni basic saana kwenye topic ya cytology. Lazima kabla hujajua virus anakufaje akiwa nje ya host na kwa nini sabuni lazima ujue angalau basic structure yake kaumbwaje...na tabia zake akiwa nje na ndani ya host nadhani huyo mwalimu wako hakukuambia hilo.

Kimsingi kirusi amejengwa kimaumbile katika sehemu kuu tatu ijapokuwa inaweza kutofautiana kutokana na aina. Sehemu kuu ambayo imebeba matatizo duniani ni ya kichwa ambayo ni DNA au RNA iliyozungukwa na kulindwa na Lipids(mafuta) na protein.

Kirusi akiwa nje ya host hawezi kutembea na metabolic activities hazifanyi kazi yaani ni nusu mfu lakini akipata mwanya wa kusafirishwa hadi ndani ya cell ya host balaa lake ndio utaliona. Atategemea DNA za ndani ya mwili wa host kupata uhai wa kuzaliana haraka sana na kupasuapasua cell za ndani ama kuzitoboa ( rejea notice zako za form twao za virus replication au cell replication uwakumbuke na akina mesenger RNA ribosomer RNA transifer RNA na zile lugha za code za Guamine, Cytocin, adenine na uracil.)

Sasa kama huyu virus viini tete vyake vinalindwa na mafuta ...unajua ukimwagia nguo mafua na ukaifua vizuri na sabuni yali mafuta yanasambaratika? sasa basi chukulia virus unanawa na sabuni na maji tiririka ukifanikiwa kuivunja lipid layer basi kirusi kinasambaratika maana DNA haiwezi kuwa virus kama haijalindwa na layer ya mafuta na hivyo unasambaratisha kabisa kwa kuvunja bond zake kichwa kule.....tail kule.... na vibre kule..... hapo kama umenewa vizuri uki poa

Ukishanawa vizuri namikonoimekauka kama una ka sanitizer chako paka tena uendelee kukupa ulinzi zaidi hapo kwa kufuata mashari mengine ya kutokushika mdomo pua , macho ..utakuwa umesalimika.

BARAKOA.....Mwanzoni wataalamu wa afya walitukanganya mara tusivae ya vitambaa mara sagikomara n95 mbwembwe tupu lakini katika hali ya uelewa wa kawaida barakoa hata za vitambaa zinasaidia sana mambo yafuatayo ambayo ni hatari kwa maambukizi.

1.Barakoa inapunguza mtu kuongea ongea hovyo hivyo kuepusha kurusha mate na majimaji mengine kwa watu wengine au kuja kwake....majimaji hayo ndio husafirisha vijidudu hivyo

2. Barakoa yoyote husaidia kupunguza watu wanaopenda kutematema mate hovyo kama nyoka aina ya swila .....hivyo hata mate yakimjia mtu huyo huyameza na kutokuleta madhara kwa watu wengine.

3. Barakoa ya aina yoyote hupunguza kuruka kwa vijidudu pale mtu anapokuhoa akiwa ameivaa na hivyokusaidia kutokusambaa umbali mrefu.

4. Barakoa ya aina yoyote husaidia kupunguza kushikashika mdomo, pua au macho kwa mikono kwa sababu itakuwa imezibwa na kitambaa hivyo kusaidia kutokupeleka virusi mdomoni puani au machoni
 
View attachment 1442471

Hahahaha nimekubali uchambuzi wako wa Barakoa na ulivyouwasilisha.Hahahah Salute mkuu
 
Nadhani nimeielewa kiaina fulani, tuendelee kujifunza elimu haina mwisho.
 
Sijijui
Mkuu najua zile multipurpose sanitizer za kuua bacteria/virus wengi hatuwezi kuzimudu, mfano 100mil inauzwa 14000/-, pamoja na kuwepo hizo za bei juu ilitakiwa elimu iwepo kwa raia ila tumeachwa tunanunua na kuoga hizo za bacteria wakati nothing to virus.

FRANCIS DA DON
Mkuu sijatoa kichwani hii kitu na nimekaa almost one month kufuatilia na kuuliza baadhi ya wataalam, sijui hiyo germs uliyosema ila nimeongelea bacteria na virus.

Francis angalia hapo kwa picha chini labda unaweza kuelewa zaidi kilichopo hapa...
1588856358756-1221432158.jpg
 
Virusi sio viumbe hai, isipokuwa ni kipande (molecule) cha DNA kilichoZUNGUKWA au kinacholindwa na mafuta mafuta mazitoo (fat) ambacho hunyonywa kwa urahisi zaidi kinapokutana na ile ngozi laini (mucous membrane) mfano, ngozi ya mdomoni, ndani ya pua, ndani ya macho au mkunduni.

Kirusi ni kitu kilaini sana kuharibika, isipokuwa tu haya mafuta yanayokizunguka ndio hukipa ulinzi na kiburi cha kusavaivu na kuishi popote kinapoangukia, kwa hiyo ili sisi tuweze kukiharibu hiki kirusi tunatakiwa tudeal na hili koti lake la nje ili kishindwe kuishi katika mazingira yetu haya ya nje kabla hakijaingia ndani.

BAADHI YA VITU VINAVYOWEZA KUMHARIBU KIRUSI KORONA

Sabuni/Mapovu (Amfifilo) ya aina yoyote ile yana uwezo mkubwa wa kuyeyusha mafuta haya yanayokizunguka kirusi endapo tu utakisugua sugua kwa muda walau wa sekunde 40 na zaidi ili kutengeneza povu jingi mkononi litakaloyeyusha yale mafuta mazito yanayokilinda kirusi, ndio maana tunaambiwa kunawa maji na sabuni kwa sekunde kadhaa.

Kitu kingine kinachoweza kuyeyusha lile futa zito linalolinda kirusi ni POMBE au mchanganyiko wowote wenye POMBE ya kiwango cha asilimia 65 na zaidi, tena hii ndo inayeyusha kiurahisi zaidi, sasa hapa wakulungwa wangu ndio tunakutana na kitu cha kuitwa KITAKASA MIKONO lakabu SANITIZER, ili kitakasa mkono chako kiwe sahihi kuweza kummaliza huyu dogo korona hakikisha kina POMBE(alcohol) zaidi ya asilimi 65.

SASA DOGO KORONA ANAKUFAJE AKIKUTANA NA SANITAIZA
Baada ya kufanikiwa kuliyeyusha lile futa zito ambalo ndio koti linalomlinda huyu dogo K, yeye kwake atakosa ulinzi na kubakiwa na DNA peke yake ambayo haiwezi kufanya chochote, yaaan kama wewe hapo sasa hivi tukuvue hyo ngozi yote halafu tukuache uende sokoni, nafikiri unaelewa itakavyokua basi ndivyo hivyo dogo korona atakavybaki na kushindwa kukudhuru wewe.

KUMBUKA; kile kitakasa mikono cha bacteria sio lazima kiwe POMBE ya kiasi kikubwa hivi.

Ndio mchango wangu mdogo katika hili, mnisamehe kwa uandishi na mapungufu mengine.

NAWA MIKONO KWA SABUNI (POVU JINGI) NA UPAKAE KITAKASA MIKONO
Asante sana kwa kutuelimisha,katika vita ukijua tu, adui unaepambana nae yako vipi, basi ni matumaini makubwa ya ishindi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom