Simba Mkali
JF-Expert Member
- Jan 31, 2012
- 620
- 243
Mkuu zimejaa tele, kutokana na jamii kuharibika kimaadili kila Kitchen Party nyingi ni sehemu ya kutukana huku kukiwa na mchanganyiko wa jinsi katika shrehe hizo.Hizo kitchen party za matusi ulihudhuria wapi ndugu? Manake nilizohudhuria mimi naona ni za kidini zaidi.
Naamini ulichokisema lakini kuna haja ya kufanya kile kitu ambacho dini yako inakutuma kufanya kama unafanya sherehe ya kuoza binti yako tofauti na kwenda kinyume na maadili au kutomfanyia kabisa. vibaya ni kukiuka maadili au labda usiwe na uwezo wa kufanya, naamini ukifanya chenye maana na maadili ya dini ni jambo la maana.Ningekuwa naoza leo hii kitu mara kitchen mada mara party ni marufuku. Kama mtoto hakulelewa na kukuzwa kwa maadili na wazazi na waliomzunguka usitegemee eti siku moja unaweza kumbadilisha!!! samaki mkunze angali mbichi na mti ukunze ungali mbichi. Wanasema, mtoto umleanvyo ndivyo akuavyo!!! Mfunze njia njema hata asiisahau wakati wa uzee wake!!!