Nilikuwa na mpenzi aliyenipenda sana. Ila tatizo lake alikuwa anakunywa sana pombe mpaka kufikia kunikera. Asipokunywa pombe siku hiyo atahakikisha anatafuta hata kwa kukopa kwenda kunywa.
Nilizoeana na familia yake hasa mama yake ingawa wao walihisi tunamahusiano ila mimi nilizoea kuwaambia ni marafiki tu.
Siku ya tukio mwenzangu alinikera kweli hata mama mkwe alijua hilo. Alikaa nami chini na kunihoji. Of course nilikuwa na hasira na niliwaza sana nimfanyeje ili ajue kuwa nimekasirika. Nikamwambia mama mkwe " sasa atakuwa sehemu anakunywa, sijui nimfate huko huko...
Cha ajabu yule mama alichukua hayo na kugeuza. Akamwambia mwanae " chunga mwenzako anataka kukuua" aisee sina hamu na huyu mama, ingawa anakuja kila siku kuniona na nikiumwa ananihangaikia sana lakini uhusiano kati yangu na mwanae umekuwa mbaya sana. Leo tunapatana kesho tunaachana. Yan ni watu tunaopendana sana lakini tuna vitu vingi sana mioyoni vinatusumbua moja wapo ikiwa ni huyu mama.
Sent using
Jamii Forums mobile app